Ina maana kubwa Papa kuelezea juu ya manyanyaso dhidi ya watoto Ina maana kubwa Papa kuelezea juu ya manyanyaso dhidi ya watoto 

Greg Burke:Kwa mujibu wa Papa unyanyasaji kingono ni uhalifu !

Bwana Burke anasema, kwa mchakato wakipindi cha miaka, Papa amekuwa akiwasikiliza wathirika, kwa maana hiyo inajionesha katika barua yake. Yeye anasisitiza kuwa majeraha yaliyo sababishwa na manyanyaso ya kingono hayatapona kamwe. Na hivyo anasisitiza kuwa ni dharura na ulazima wa kuwajibika kwa kiasi kikubwa katika kuchuka hatua ya waliotenda uhalifu

Sr. Angela Rwezaula  - Vatican  

Tunazungumzia juu ya Ireland Marekani na Chile: Lakini si nchi hizi tu,  Papa Francisko kwa dhati ameandikia watu wote  Mungu na ndiyo maana yake. Hii ina maana kubwa ya Papa kuelezee juu ya manyanyaso  na uhalifu huo, si tu kuungama dhambi, lakini pia hata kuomba msamaha;  vilevile yeye anatambua kwamba hakuna nguvu yoyote ya kibinadamu inaweza kufunika ubaya ulotendeka, hata nguvu yoyote ya kibinadamu kuweza kutosheleza wathirika na ambao bado wanaishi.

Ndiyo ufafanuzi wa Bwana Greg Burk Msemaji wa habari za Vatican mara baada ya kutangazwa kwa Barua ya Baba Mtakatifu Francisko kwa watu wa Mungu Jumatatu 20 Agosti 2018 mjini Vatican. Bwana Greg Burke anaanza  kuthibitisha juu ya Barua hiyo na matokeo ya unyanyaswaji kingono uliotendewa watoto kwa upande wa makleri na watu waliowekwa wakfu.

Bwana Burke anasema, kwa mchakato wakipindi cha miaka, Papa amekuwa akiwasikiliza wathirika, hiyo inajionesha katika barua yake. Yeye anasisitiza kuwa majeraha yaliyo sababishwa na manyanyaso ya kingono hayatapona kamwe. Na hivyo anasisitiza kuwa ni dharura na ulazima wa kuwajibika kwa kiasi kikubwa,  si tu kwa upande wa kuchukulia hatua  waliotenda  uhalifu huo, lakini hata kwa upande wa wale waliofunika uhalifu huo mbaya,mahali ambapo kwa upande wa kesi nyingi za kufunika zinawakumba maaskofu.

Zaidi ya kuhamasisha Kanisa katoliki kuchukua hatua muhimu za kulinda watu, katika taasisi zake, pia  Kanisa  linapaswa kujifunza  somo  gumu kutoka  yale  yaliyopita, kuwajibika kwa  wale  waliotenda na hata  wale  ambao waliruhusu  unyanyasaji  huo  kutokea. Papa Francisko aidha anaomba hata waamini wote kila mmoja nafsi yake kwa kutumia zana za kiutamaduni ili  kupambana na ubaya kama zile za sala na kuomba toba.

 

 

 

 

21 August 2018, 15:23