Cerca

Vatican News
Askofu Mkuu Vincenzo Zani wakati wa Mkutano wa kimataifa kuhusu dini na changamoto za sasa nchini Rwanda. Askofu Mkuu Vincenzo Zani wakati wa Mkutano wa kimataifa kuhusu dini na changamoto za sasa nchini Rwanda. 

Elimu Katoliki ni chombo cha amani na huduma kwa watu wote

Askofu Mkuu Zani anasema umakini zaidi kati ya ulimwengu na nchi mahalia ni lazima ushinde na kuelimisha wazalendo wa dunia hii, bila kupoteza mizizi yao; umakini wa kujiwekea misingi ya ulimwengu na kutunza thamani binafsi; kuhifadhi tamaduni binafsi ambazo haziwezi kubadilishwa na yoyote,badala yake lazima ziendeleze mzizi wake

Sr Angela Rwezaula – Vatican News

Elimu ina nguvu zaidi ya kuhamasisha mazungumzo, usikivu na thamani ya mshikamano ili kuweza kukua kwa pamoja, kujenga uhusiano, inasikindikiza na  kutoa uwezo wa kuwa  na uvumilivu wa mmoja na mwingine kwa ajili ya maendeleo.

Ni  katika  mantiki zote za kila nafsi na kusaidiana kutika kusahihisha  mitazamo ya maisha ambayo inashikilia sana masuala binafsi ya  mali, uchumi na itikadi. Kwa njia hiyo haiwezekani kufikiria kujenga maisha ukiwa na mategemeo yakuwa na furaha milele wakati huo unakwenda kinyume chake , maana inahitajika kutazama hali halisi na hisia nyeti  zenye uwezo wa kuwa na amani na mapatano. Amani inajengwa kwa kazi ya kila siku kwa uvumilivu kupitia moyo ambao uko tayari kukubali mahitaji ya mwingine, kushirikishana shughuli, uwajibikaji, kutoa matumaini na kujenga madaraja. Haya yote ni kwa mujibu wa maandishi ya  Askofu Mkuu Vincenzo Zani,  Katibu wa Braza la Kipapa la Elimu Katoliki.

Katika Gazeti la Osservatore Romano, Askofu Mkuu Zani  anaandika kuwa, tangu mwanzo wa karne hii umeonesha picha ya mabadiliko ya kina ambayo imesababisha msukumo mkubwa na wa haraka katika mabadiliko ambayo yanaonekana katika ulimwengu wa nchi za mashariki kama vile hata nchi zinazopiga maendeleo.  Utandawazi, uwekezaji wa uchumi, mchanganyiko wa tamaduni za kijamii zilizoongezeka kutokana na matukio ya uhamiaji, teknolojia pamoja na mantiki mbalimbali ambazyo yamebadili mambo mengi ya kizamani kama vile ya  kiuchumi, kijamii  na  hata kwa elimu.

Mashirika ya kimataifa kama vile Unesco, kwa miaka kumi wamekuwa wakifikiria njia mbalimbali ambazo zinasababisha  mchakato hasi wa mafunzo duniani kote na kwa kipindi hicho wameweza kutoa mapendekezo ya ripoti ambayo inasaidia mtazamo kwa ujumla juu ya changamoto za elimu. Kwa upande wake, zinaonesha utambuzi wa hatari na hasa itokanayo na ubinafsi wa mafunzo ambayo kwa ujumla yanatakiwa ndiyo yatoe  jibu kwa njia ya mipango ya elimu ambayo inatazama ukuu wa binadamu na jumuiya ya jamii .

Haki msingi za watoto na vijana zinatakiwa kuzingatiwa na kupewa kipaumbele hasa umakini kwa serikali na hivyo kutoa uchaguzi wa kisiasa, kiuchumi na fedha ambapo kama sera za kisiasa ni lazima ziwekezwe kwa ajili ya kitengo nyeti cha elimu na zaidi kujikita katika elimu ambayo inatambua na kuona upeo wa juu kwa ajili ya kuondoa vikwazo ambavyo wakati mwingine vinasabishwa na itikadi kali.

Askofu Mkuu Zani  anasema kuwa umakini zaidi kati ya ulimwengu na nchi mahalia , inabidi kushinda na kuelimisha wazalendo wa dunia hii, bila kupoteza mizizi yao; umakini kati ya kujiwekea misingi ya ulimwengu na kutunza thamani binafsi; umakini kati  ya kuhifadhi tamaduni binafsi ambazo haziwezi kubadilishwa na yoyote, na badala yake lazima ziendeleze mzizi wake na kusaidia na  wakati huo huo mazungumzo na maono mengine; umakini kati ya dharura za mali na zile za kiroho.

Ili kuweza kushinda changamoto hizi, ripoti ya Unesco inaelekeza misingi mikuuu minne ya kujenga mtindo wa mazungumzo ya wakati endelevu, mahali ambapo shule katoliki inautambuzi huo. Msingi wa kwanza ulio elekezwa ni ule wa kujifunza kujitambua; wa pili ni ule wa kujifunza kutenda; watatu ni ule unaotazana kujifunza kuishi kwa pamoja katika  kuendeleza ule ulewa na watu wangine,  hata wa tamaduni na kufanya uzoefu wa kujitegemea ikiwa ni pamoja na kuhamasisha  na kuruhusu kutengeneza mipango kwa pamoja, kubuni  na kujufunza namna ya kukabiliana na migogoro, katika roho moja ya heshima kwa ajili ya thamani ya wingi wa utamaduni na tamaduni, aidha  uwelewa wa pamoja na amani; na msingi wa nne ni ule wa kujifunza uwepo, kwa maana ya kujiendeleza binafsi ukiwa na uwezo wa kutenda daima na kujitegemea kwa kijitathimini na uwajibikaji binafsi.

Elimu haipaswi kwa maana hiyo kudharau yoyote katika ukuu wa binadamu: Katika hili elimu inachangamotishwa na thamani zake za kina ambazo hawali ya yote ni ukuu wa binadamu, thamani ya jumuiya, utafutaji wa ustawi wa  pamoja, mshikamano na ushirikiano, utunzaji wa wadhaifu, umakini kwa wale ambao hawana bahati.

Katika kufikiria misingi hiyo minne ambayo inaongezewa na kupewa kiina hasa cha binadamu katika mchakato wa elimu, matarajio ya thamani ya kikristo inaalika kutoa kipaumbele katika nyanja kuu ya elimu ya maadili ambayo inaongeza ubinadamu mpya yaani kujikita kwa kina katika upendo kama ndiyo kigezo cha hali halisi ya kwanza katika kuelimisha na ambayo ni nguvu ya kumfanya binadamu akue na kuwa na uwezo wa kubadilisha hali halisi hiyo inayo mzunguka.

Pamoja na hayo yote katika kuendeleza hali halisi na usawa kwa mijibu wa nchi ziwe tajiri au maskini ni lazima kukubaliana  na mawazo mapya , ambayo ni mapinduzi na yenye uwezo wa mabadiliko, kwamba elimu siyo mfumo wa utendaji tu badala yake ni kiungo cha madiliko ya mfumo na ambayo inafungua nafasi na  uwezekano mpya.

Kanisa la Millennia ya tatu, kwa uwepo wake kwa njia ya mashule na vyuo Vikuu Katoliki, lakini pia hata huduma zake mbalimbali za walimu wanazotenda katika mashule ya umma, inapyaisha kwa kiasi kubwa elimu kwa ajili ya wema wa  kizazi cha vijana na kuwasaidia wakue na siyo tu kwa ajili ya akili, lakini pia zaidi kwa ajili ya ubinadamu! Na mwisho elimu inasaidia kuona kila binadamu anahisi uhalisia  wa kushiriki ujenzi wa jamii mpya , kuanzia katika maadiili na sheria za kushirikishana. Kwa mtazamo huo inabidi daima kuendeleza mbele mchakato ambao unapaswa uendelezwe ukiwa unafikiria familia nzima ya kibinadamu.

Askofu Mkuu Vincenzo Zani, katibu wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki anahitimisha  kuwa, kwa maana hiyo ni lazima kuandaa, kuchagua, kusasisha na kusaidia kwa upande wa mtazamo kiuchumi pamoja na matatizo yaliyopo na ili kuweza  kuwekaza ubora wa elimu ambayo daima ni mkakati muhimu na ambayo inahakikisha wema wa Kanisa na Jamii!

12 August 2018, 09:07