Cerca

Vatican News
Maaskofu wa Gambia, Liberia na  Sierra  Leone, wakiwa na Baba Mtakatifu wakati wa hija yao ya kitume ! Maaskofu wa Gambia, Liberia na Sierra Leone, wakiwa na Baba Mtakatifu wakati wa hija yao ya kitume !  (© Vatican Media)

Askofu Mkuu Dagoberto CAMPOS SALAS balozi wa kitume - Gambia

Askofu Mkuu Dagoberto CAMPOS SALAS alizaliwa Puntarenas, kisiwani Costa Rica kunako tarehe 14 Machi 1966 huko Campos Salas. Alipata daraja Takatifu la Upadre mnamo tarehe 22 Mei 1994 na wenye Shahada ya Sheria

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 17 Agosti 2018  Baba Mtakatifu Francisko amemteua Balozi wa kitume katika nchi ya Gambia Askofu mkuu  Dagoberto CAMPOS SALAS wa Forontiniana, ambaye alikuwa Balozi wa kitume nchini Liberia.

Askofu Mkuu Dagoberto CAMPOS SALAS alizaliwa Puntarenas, kisiwani Costa Rica kunako tarehe 14 Machi 1966 huko Campos Salas. Alipata daraja Takatifu la Upadre mnamo tarehe 22 Mei 1994  na mwenye uzamivu wa Shahada ya Sheria.

Alianza shughuli za kidiplomasia Vatican tangu tarehe 1 Julai 1999. Katika shughuli hiyo ameweza  kushika nafasi ya ubalozi wa kitume Vatican katika nchi za Sudan, Chile, Sweden, Uturuki, Mexico na wakati wa kuteuliwa kwake alikuwa  ni Balozi wa kitume huko Tilarán-Liberia. Anafahamu vizuri ligha ya kihispania, kingereza na kiitaliano.

18 August 2018, 09:54