Askofu Mkuu Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican Katika Ofisi za Umoja wa Mataifa New York Askofu Mkuu Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican Katika Ofisi za Umoja wa Mataifa New York 

Askofu Mkuu Auza:Mazungumzo yanasaidia kusuluhisha migogoro!

Kwa Mujibu wa Askofu Mkuu Bernadito Auza anasema: Kanisa Katoliki linaalikwa kujikita katika kusaidia kuondokana na migogoro kati ya Taifa na taifa, watu. Inabidi kusikiliza na kuwa karibu na waathirika wa nguvu na ambao wanakosa haki kutokana na migogoro.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Upatanisho wa dhati unaweza kuleta suluhisho la migogoro na ambayo ni shughuli inayohitaji ushiriki wa sehemu zote zinazohusika, kwa maana si tu zile zinazo jihusisha na kuongoza, lakini hata jumuiya nzima, kwa namna ya pekee wale ambao wameteseka katika migogoro. Hayo yamethibitishwa na Askofu Mkuu Bernadito Auza Mwalikishi wa kudumu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini zilizoko New York  Marekani, tarehe 29 Agosti 2018 katika Mkutano wa mjadala kuhusu Usalama ambao umeongozwa na kauli mbiu “ Upatanisho na suluhisho la migogoro”.

Ukaribu na waathirkia wa nguvu na ukosefu wa haki

Katika uzoefu wake wa moja kwa moja, anasema, Kanisa Katoliki linaalikwa kujikita katika kusaidia kuondokana na migogoro kati ya Taifa na taifa, watu. Inabidi kusikiliza na kuwa karibu na waathirika wa nguvu na ambao wanakosa haki kutokana na migogoro.

Katika hotuba yake amekumbuka hata kesi ya kiongozi wa Argentina na Chile mwaka 1978 waliokuwa wanarumbamba kati, lakini pia hata hatua waliyoichkua na kujikita katika mafaikio ya amani kati yao, shukrani kwa wito kutoka kwa Mtakatifu Yohane Paulo II ambaye aliwaomba wasikatisha kamwe mchakato mapatano ili kufikia lengo kamili.

Kadhalika Askofu Mkuu Auza amekumbuka hata mktaba wa  makubaliano ya nchi mbili zilizokuwa na waasi wa kutumia  silaha huko Msumbiji barani Afrika na wa hivi karibuni nchini Colombia. Hii ni mifano ambayo inaonesha ni jinsi gani kuna ulazima wa kuacha njia wazi za mapatano ili kuweza kutoa suluhisho dhidi ya malumbano , na kwamba kamwe mchakati wa uvumilvu na mazungumzo husiachwa kwa maana inaweza kuleta suluhisho kwa njia ya amani ya kweli kwa watu walio staarabika.

Utamaduni wa makutano katika moyo wa upatanisho.

Hata hivyo Askofu Mkuu anaonesha jinsi gani hata Baba Mtakatifu Francisko wakati wa ziara yake nchini Colombia Septemba 2017: kutafuta amani ni kazi ili wazi: kiini cha upatanisho kwa dhati ni utamaduni wa makutano ambao unatoa mwafaka anathibithsa Askofu Mkuu Auza , na kuongeza kusema kuwa hesima ya pamoja na uelewa si kwamba ni katika kusaidia kutoa suluhisho lakini pia namna ya maelewana na wengine, hasa katika kazi isiyokuwa na ukomo kwa ajili ya kutafuta amani na mapatano katika moyo wa kila maisha kwa kila siku.Utamduni wa Makutano Baba Mtakatifu anathibitisha , unahitaji kuwekwa kiini cha kila aina ya matendo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yak ila mtu , , hadi yake na heshima ya wema wa pamoja.

Ushiriki wa kujenga wakati ujao wa amani

Ushiriki katika mchakato wa amani unafanyika kwa mitindo mingi , kuanzia katika meza ya mduara hadi vyanzo vidogo kabisa. Migogoro inaacha daima majeraha ya kina. Ni mchakato ambao unahitaji kushiriki kwa njia ya mapatano na kutafuta suluhisho dhidi ya malumbano. Kadhalika ni jambo msingi hatua ya mchakato wa kuponesha na ambayo inaendelea kwa muda mrefu mara baada ya uwanja wa maji kukauka, amethibitisha Askofu Mkuu Auza na kusisitizia juu ya kusini mikataba. Mpatanishi mwema, wakati anafanya kazi ya kusuluhisha malumbano, anajenga wakati endelevu wa amani, Mpatanishi ni mfanyakazi wa kawaida na chombo cha amani ambapo, lazima kushukuru kwa dhati juhudi nyeti na yenye tunu ya huduma ambayo imetendeka kwa binadamu.

31 August 2018, 15:58