Ulinzi na usalama wa wakimbizi na wahamiaji daima uko mashakani. Ulinzi na usalama wa wakimbizi na wahamiaji daima uko mashakani. 

Ulinzi, usalama na ubora wa maisha bado ni tete kwa wahamiaji na wakimbizi

Ujumbe wa Vatican unasikitika kusema kwamba, Tume ya Kimataifa juu ya Idadi ya watu na maendeleo imeshindwa kufikia malengo yake ya kuhakikisha hali nzuri na afya bora kwa wahamiaji na katika miji wanamopata hifadhi, kwa kuzingatia Mkataba wa Kimataifa wa usalama wa wahamiaji.

Na Padre Celestine Nyanda. - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko anasema: mshikamano lazima uonekane katika kila hatua kwa kuwajali wahamiaji kuanzia kuondoka kwao kutoka nchi zao asilia, muda wote wakati wa safari yao mpaka wanapotua nchi hifadhi na pale watakaporejea tena katika nchi zao. Huu ni wajibu mkubwa kwa wanaume na wanawake wote wenye mapenzi mema kujibu changamoto za wahamiaji kwa ukarimu, utayari, hekima na mwono kadiri ya uwezo wa kila mmoj

Askofu mkuu Bernadirto Auza, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa anakumbusha jinsi gani ushiriki wa Jumuiya ya Kimataifa ulivyo muhimu katika kutafuta afya bora na hali njema ya kila mwanadamu ili kudumisha amani na usalama kwa sasa na kwa siku za usoni. Hata hivyo ujumbe wa Vatican unasikitika kuona kwamba, Tume ya Kimataifa juu ya Idadi ya watu na maendeleo imeshindwa kufikia malengo yake ya kuhakikisha hali nzuri na afya bora kwa wahamiaji na katika miji wanamopata hifadhi, kwa kuzingatia Mkataba wa Kimataifa wa usalama wa wahamiaji.

Askofu mkuu Auza anasema, inaonekana sababu za kushindwa kufikia malengo hayo ni kutokana na kutozingatia utayari wa wajumbe wakati wote wa mchakato, kwani mafanikio ya Tume hiyo hutegemea sana kuridhia kwa mataifa na kuheshimu misimamo yao hasa kwenye mambo nyeti. Inasikitisha kuona kwamba mchakato huu haukutilia maanani masuala nyeti yanayohusiana na afya ya jinsia na uzazi, pamoja na haki za uzazi kadiri ya nchi husika.

Mkutano wa Kimataifa juu ya idadi ya watu na maendeleo, ambao kutoka kwake Tume hiyo inapata msingi wake, uliweka wazi kwamba utoaji mimba unapaswa kuzingatia taratibu za kitaifa za utungaji sheria na kwamba kila nchi ina haki ya kufanyia kazi mapendekezo ya Mkutano wa Kimataifa juu ya idadi ya watu na maendeleo kwa namna inayoendana na sheria za nchi, na kwa kuheshimu tunu za dini, imani, maadili na tamaduni.

Tume ya Kimataifa juu ya idadi ya watu na maendeleo imekuwa ikisuasua kusimamia maamuzi hayo na hivyo kupelekea kutofikia malengo yake ya afya na usalama wa wahamiaji na miji wanamojikuta. Ujumbe wa Vatican unaendelea kusimama kidete kutetea haki msingi za kila binadamu bila kujali hali yake kijamii, kisiasa wala kidini, na kwamba ni matumaini ya Vatican kwamba Tume itaweka wazi na kusimamia maamuzi hayo ili kuhakikisha inafikia malengo yake kwa mwaka ujao.

Baba Mtakatifu Francisko anasema: mshikamano lazima uonekane katika kila hatua kwa kuwajali wahamiaji kuanzia kuondoka kwao kutoka nchi zao asilia, muda wote wakati wa safari yao mpaka wanapotua nchi hifadhi na pale watakaporejea tena katika nchi zao. Huu ni wajibu mkubwa kwa wanaume na wanawake wote wenye mapenzi mema kujibu changamoto za wahamiaji kwa ukarimu, utayari, hekima na mwono kadiri ya uwezo wa kila mmoja.

Askofu mkuu Bernadirto Auza, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa anakumbusha jinsi gani ushiriki wa Jumuiya ya Kimataifa ulivyo muhimu katika kutafuta afya bora na hali njema ya kila mwanadamu ili kudumisha amani na usalama kwa sasa na kwa siku za usoni. Hata hivyo ujumbe wa Vatican unasikitika kuona kwamba, Tume ya Kimataifa juu ya Idadi ya watu na maendeleo imeshindwa kufikia malengo yake ya kuhakikisha hali nzuri na afya bora kwa wahamiaji na katika miji wanamopata hifadhi, kwa kuzingatia Mkataba wa Kimataifa wa usalama wa wahamiaji.

Askofu mkuu Auza anasema, inaonekana sababu za kushindwa kufikia malengo hayo ni kutokana na kutozingatia utayari wa wajumbe wakati wote wa mchakato, kwani mafanikio ya Tume hiyo hutegemea sana kuridhia kwa mataifa na kuheshimu misimamo yao hasa kwenye mambo nyeti. Inasikitisha kuona kwamba mchakato huu haukutilia maanani masuala nyeti yanayohusiana na afya ya jinsia na uzazi, pamoja na haki za uzazi kadiri ya nchi husika.

Mkutano wa Kimataifa juu ya idadi ya watu na maendeleo, ambao kutoka kwake Tume hiyo inapata msingi wake, uliweka wazi kwamba utoaji mimba unapaswa kuzingatia taratibu za kitaifa za utungaji sheria na kwamba kila nchi ina haki ya kufanyia kazi mapendekezo ya Mkutano wa Kimataifa juu ya idadi ya watu na maendeleo kwa namna inayoendana na sheria za nchi, na kwa kuheshimu tunu za dini, imani, maadili na tamaduni.

Tume ya Kimataifa juu ya idadi ya watu na maendeleo imekuwa ikisuasua kusimamia maamuzi hayo na hivyo kupelekea kutofikia malengo yake ya afya na usalama wa wahamiaji na miji wanamojikuta. Ujumbe wa Vatican unaendelea kusimama kidete kutetea haki msingi za kila binadamu bila kujali hali yake kijamii, kisiasa wala kidini, na kwamba ni matumaini ya Vatican kwamba Tume itaweka wazi na kusimamia maamuzi hayo ili kuhakikisha inafikia malengo yake kwa mwaka ujao.

Sikiliza kwa raha zako mwenyewe!
30 July 2018, 15:47