Vatican News
Papa Francisko akizungumza na Maaskofu wa Gambia, Liberia na Sierra Leone wakati wa hija yao ya kitume mjini Vatican. Papa Francisko akizungumza na Maaskofu wa Gambia, Liberia na Sierra Leone wakati wa hija yao ya kitume mjini Vatican.  (Vatican Media)

Monsinyo Dagoberto Salas ateuliwa kuwa Balozi, Liberia.

Monsinyo Dagoberto Campos Salas aliyezaliwa kunako mwaka 1966 na kupewa Daraja ya Upadre mwaka 1994 na kuanza utume wake katika diplomasia ya Kanisa hapo tarehe 1 Julai 1999 ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Liberia.

Na Padre Richard A Mjigwa. C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Dagoberto Campos Salas kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Liberia na wakati huo huo amempandisha hadhi na kuwa Askofu mkuu. Askofu mkuu mteule Dagoberto Campos Salas alizaliwa kunako tarehe 14 Machi 1966 huko Puntarenas, nchini Costa Rica. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, kunako tarehe 22 Mei 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 1 Julai 1999 akaanza utume wake katika diplomasia ya Kanisa kwa kutoa huduma ya kitume nchini: Sudan, Chile Sweden, Uturuki na Mexico.

 

28 July 2018, 15:41