Beta Version

Cerca

Vatican News
The Rosary (© Biblioteca Apostolica Vaticana)

Matendo ya Rozari Takatifu

Matendo ya furaha
(Jumatatu na Jumamosi)

1.     Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kwamba atakuwa Mama wa Mungu

Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.

2.     Maria anakwenda kumtembelea Elizabeti

Tumwombe Mungu atujalie mapendo kwa jirani

3.     Yesu anazaliwa Betlehemu.

Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara.

4.     Yesu anatolewa hekaluni

Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo

5.     Maria anamkuta Yesu hekaluni

Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
 

Matendo ya mwanga
(Alhamisi)

1.     Ubatizo wa Yesu mtoni Yordani.

Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.

2.     Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana.

Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya Injili.

3.     Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu

Tumwombe Mungu atujalie kuupokea ufalme wake kwa toba ya kweli.

4.     Yesu anageuka sura.

Tumwombe Mungu atujalie neema ya kung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.

5.     Yesu anaweka sakramenti ya Ekaristi

Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.

 

Matendo ya uchungu
(Jumanne na Ijumaa)

1.     Yesu anatoka jasho la damu

Tumwombe Mungu atujalie sikitiko timilifu

2      Yesu anapigwa mijeledi

Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu

3.     Yesu anatiwa miiba kichwani

Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.

4.     Yesu anachukua msalaba.

Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.

5.     Yesu anakufa msalabani.

Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria

 

Matendo ya utukufu
(Jumatano na Jumapili)

1.     Yesu anafufuka.

Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu

2.     Yesu anapaa mbinguni.

Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.

3.     Roho Mtakatifu anawashukia mitume

Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.

4.     Bikira Maria anapalizwa mbinguni.

Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.

5.     Bikira Maria nawekwa Malkia mbinguni.

Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.