Beta Version

Cerca

Vatican News
The Regina Caeli (© Biblioteca Apostolica Vaticana)

Malkia wa mbingu

Malkia wa mbingu, furahi, Aleluya.
Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya.
Amefufuka alivyosema, Aleluya.
Utuombee kwa Mungu, Aleluya.
Furahi shangilia, ee Bikira Maria, Alaluya.
Kwani hakika Bwana amefufuka Aleluya.
Tuombe
Ee Mungu, uliyependa kuifurahisha dunia
kwa kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristo, Mwanao:
Fanyiza, twakuomba, kwa ajili ya Bikira Maria,
tupate nasi furaha za uzima wa milele.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.