Beta Version

Cerca

Vatican News
The Magnificat (© Biblioteca Apostolica Vaticana)

Utenzi wa Bikira Maria, Magnificat

Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,

na roho yangu imemfurahia

Mungu, Mwokozi wangu.

Kwa kuwa ameutazama

unyonge wa mjakazi wake.

Kwa maana, tazama, tokea sasa,

vizazi vyote wataniita mbarikiwa.

Kwa kuwa mwenye nguvu amenitendea makuu,

na jina lake ni takatifu.

Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi

kwa hao wanaomcha.

Amefanya nguvu kwa mkono wake;

amewatawanya walio na kiburi

katika mawazo ya mioyo yao.

Amewaangusha wakuu kutoka viti vyao vya enzi;

na wanyonge amewakweza.

Wenye njaa amewashibisha mema,

Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu.

Amemsaidia Israeli, mtumishi wake,

ili kukumbuka rehema zake;

kama alivyowaahidia baba zetu,

Ibrahim na uzao wake hata milele.

Atukuzwe Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

Kama mwanzo, na sasa na siku zote, na milele. Amina.