Beta Version

Cerca

Vatican News
The Benedictus (© Biblioteca Apostolica Vaticana)

Utenzi wa Zakaria, Benedictus

Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli,

kwa kuwa amewajia, na kuwakomboa watu wake.

Ametupatia Mwokozi shujaa,

mzawa wa Daudi, mtumishi wake.

Aliahidi hapo kale,

kwa njia ya manabii wake watakatifu;

kwamba atatuokoa mikononi mwa adui zetu,

na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.

Alisema atawahurumia wazee wetu,

na kukumbuka agano lake takatifu.

Alimwapia Abrahamu babu yetu,

kwamba atatujalia sisi,

tukombolewe kutoka mikononi mwa adui zetu,

tupate kumtumikia bila hofu,

tuwe wanyofu na waadilifu mbele zake,

siku zote za maisha yetu.

Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa Mungu aliye juu,

utamtangulia Bwana, kumtayarishia njia yake;

kuwatangazia watu kwamba wataokolewa,

kwa kuondolewa dhambi zao.

Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma.

Atatuchomozea jua la haki kutoka juu,

na kuwaangazia wote wanaokaa,

katika giza kuu la kifo,

aongoze hatua zetu katika njia ya amani.

Atukuzwe Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

Kama mwanzo, na sasa na siku zote, na milele. Amina.