Beta Version

Cerca

Vatican News
Hail Holy Queen (© Biblioteca Apostolica Vaticana)

Salamu Malkia

Salamu Malkia,mama mwenye huruma,

uzima, tulizo na matumaini yetu salamu.

Tunakusihi hapa ugenini sisi wana wa eva.

Tunakulilia tukilalamika

na kuhuzunika bondeni huku kwenye machozi.

Haya basi mwombezi wetu,

utuangalie kwa macho yako yenye huruma

na mwisho wa ugeni huu,

utuonyeshe Yesu mzao mbarikiwa wa tumbo lako,

ee mpole, ee mwema, ee mpendelevu Bikira Maria.