Papa:Sikukuu ya Kutolewa Bwana hekaluni na Watawa,ninyi ni chachu ya Kanisa!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ameongoza masifu ya jioni, Jumamosi tarehe I Februari katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, katika mkesha wa Siku Kuu ya Kutolewa kwa Bwana Hekaluni, sanjari na Siku ya XXIX ya Watawa Ulimwenguni 2025. Kanisa Kuu lilijaa Maaskofu, makardinali, watawa kike na kiume wameseminari na waamini watu wa Mungu katika masifu hayo. Baada ya zaburi na somo, Baba Mtakatifu alianza tafakari yake kuwa “Tazama, nimekuja kufanya mapenzi yako, Ee Mungu” (Heb 10:7). Kwa maneno haya mwandishi wa Waraka kwa Wahebrania anadhihirisha mshikamano kamili wa Yesu kwa mpango wa Baba. Leo tunayasoma katika Sikukuu ya Kutolewa kwa Bwana hekaluni, sanjari na Siku ya Watawa Ulimwenguni, katika Jubilei ya Matumaini, katika muktadha wa kiliturujia unaotambulika kwa alama ya mwanga.
Papa Francisko aliendelea kusema kuwa wao wote ambao walichagua njia ya mashauri ya kiinjili, wamejiweka wakfu kama “Bibi-arusi mbele ya Bwana-arusi [...] waliyofunikwa katika nuru yake”(Mtakatifu Yohane Paulo II, Mashirika ya Kitume,15); mmejiweka wakfu kwa mpango ule ule unaong'aa wa Baba ambao ulianzia kwenye asili ya ulimwengu.” Kwa njia hiyo itakuwa na utimilifu wake kamili mwishoni mwa wakati, lakini tayari sasa mnajidhihirisha kupitia “maajabu ambayo Mungu anafanya katika ubinadamu dhaifu wa watu walioitwa”(VC20). Katika hilo Papa ameongeza kusema “Hebu tutafakari basi jinsi gani, kupitia viapo vya nadhiri za umaskini, usafi wa moyo na utii ambao wamekiri, pia wanaweza kuwa wabebaji wa nuru ya wanawake na wanaume wa wakati wetu.
Kipengele cha kwanza: mwanga wa umaskini. Huu una mizizi yake katika maisha yenyewe ya Mungu, zawadi ya milele na ya upatanisho kamili wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu (VC 21). Kwa kutumia umaskini kwa njia hiyo, mtawa, akiwa na matumizi ya bure na ya ukarimu wa vitu vyote, anakuwa mtoaji wa baraka kwao: anadhihirisha wema wake kwa utaratibu wa upendo, anakataa kila kitu kinachoweza kuficha uzuri wao na ubinafsi, uchoyo, utegemezi, matumizi ya jeuri na mauti na badala yake anakumbatia kila kitu ambacho kinaweza kuimarisha: usawa, ukarimu, kushirikiana na mshikamano. Na Paulo anasema: “Kila kitu ni chako! Bali ninyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu” (1Kor 3:22-23). Huo ni umaskini.
Kipengele cha pili ni mwanga wa usafi wa moyo. Papa Francisko alibainisha kuwa na hii pia ina chimbuko lake katika Utatu na inadhihirisha “mwelekeo wa upendo usio na mwisho unaowafunga, Nafsi tatu za Kimungu” (VC,21). Taaluma yake, katika kukataa upendo wa ndoa na katika njia ya kujizuia, inathibitisha ukuu kamili, kwa mwanadamu, wa upendo wa Mungu, kukaribishwa kwa moyo usiogawanyika na mwenzi (rej 1Kor 7:32-36) na anaionesha kama chanzo na kielelezo cha upendo mwingine wote. Papa Francisko katika hilo aliongeza kusema kuwa: “Tunajua, jinsi ambavyo tunaishi katika ulimwengu ambao mara nyingi una alama za aina potofu za upendo, ambapo kuna kanuni ya “kile ninachopenda” na kanuni hiyo, inatusukuma kutafuta kingine zaidi cha kuridhisha mahitaji yetu, badala ya kuwa na mkutano wa furaha wa kuzaa matunda. Hii ni kweli. Hii inazalisha, katika mahusiano, mitazamo ya kijuujuu na hatari, ubinafsi, ukosefu wa ukomavu na kutowajibika kwa maadili, ambapo mume na mke wa maisha yote hubadilishwa na mwenzi wa sasa, watoto wanakaribishwa kama zawadi na wale wanaotarajiwa kama haki au kuondolewa kama “usumbufu.”
Papa Francisko alisisitiza kuwa, katika muktadha wa aina hiyo, wanaokabiliwa na haja inayoongezeka ya uwazi wa mambo ya ndani katika uhusiano wa kibinadamu" (Vita consecrata, 88) na ubinadamu wa vifungo kati ya watu binafsi na jumuiya, usafi wa moyo wa mtawa unatuonesha kwa wote ' kike na kiume wa karne ya ishirini na moja, njia ya uponyaji kutoka katika uovu wa kujitenga, katika matumizi ya njia ya bure na ya ukombozi wa kupenda, ambayo inakaribisha na kuheshimu kila mtu na haina nguvu au kukataa mtu yeyote. Ni dawa iliyoje kwa roho ya kukutana na wanaume na wanawake watawa wenye uwezo wa aina hii ya uhusiano uliokomaa na wenye furaha! Wao ni onesho la upendo wa Mungu ( Lk 2:30-32).
Kwa maana hiyo, Papa alisisitiza ni muhimu, katika jumuiya zetu, kutunza ukuaji wa kiroho na kihisia wa watu, kuanzia malezi ya awali, hata katika malezi yanayoendelea, ili usafi wa kweli uoneshe uzuri wa upendo unaotolewa; na hauchukui matukio mabaya kama vile kuuma kwa moyo au utata wa uchaguzi, chanzo cha huzuni, kutoridhika na sababu, wakati mwingine, katika mafunzo dhaifu zaidi, ya maendeleo ya “maisha ya ndumila kuwili. Mapambano dhidi ya majaribu ya maisha ya ndumila kuwili mbayo ni ya kila siku. Ni kila siku,” Papa Francisko alionya.
Katika kipengele cha tatu ambacho ni mwanga wa utiifu ambapo Papa Francisko alisema: Andiko ambalo lilisikika lilizungumza nasi pia kuhusu hili, likituonesha, katika uhusiano kati ya Yesu na Baba, “uzuri wa ukombozi wa utegemezi wa kimwana na sio wa utumwa, tajiri katika hisia ya uwajibikaji na unaohuishwa na kuaminiana”(VC, 21). Ni mwanga hasa wa Neno ambalo linakuwa zawadi na mwitikio wa upendo, ishara kwa jamii yetu, ambamo huwa tunazungumza sana lakini kusikiliza kidogo: katika familia, kazini na hasa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo unaweza kubadilishana maneno na picha bila hata kukutana, kwa sababu haujiweki kwenye mchezo wa mmoja na mwingine. Papa Francisko alitafakari kidogo kuhusu jambo hili kwamba: “Na hili ni jambo la kuvutia. Kwa sababu mara nyingi, katika mazungumzo ya kila siku, kabla ya mtu hajamaliza kuzungumza, jibu tayari linatoka. Hakuna kusikiliza! na kumbe ni kusikilizana kabla ya kujibu. Kukaribisha neno la mwingine," Papa alishauri.
Baba Mtakatifu alisema: Ningependa kuhitimisha kwa kukumbusha hoja nyingine: “kurudi kwenye asili”, ambayo inazungumzwa sana leo katika maisha ya watawa. “Lakini si kurudi katika asili kama vile kurudi katika makumbusho, hapana. Ina maana ya kurudi katika asili ya maisha yetu.” Kuhusiana na hili, Neno la Mungu ambalo tumesikia linatukumbusha kuwa, “kurudi kwa asili” mahali pa kwanza na muhimu zaidi kwa kila mtawa na kwetu sisi sote, ni kule kwa Kristo na “ndiyo” yake kwa Baba. Inatukumbusha kwamba kwa upya, kwamba kabla ya mikutano na “meza za miduara,” ambayo inapaswa kufanyika, ni muhimu ifanyike mbele ya Tabernakulo, katika kuabudu. Kwa kuongezea alieleza: “sisi tumesahau kidogo maana ya kuabudu. Sisi ni wa vitendo sana, na tunataka kufanya mambo, lakini… Kuabudu ni kidogo.