Tafuta

2025.02.03 Papa Francisko akutana na makumi elfu ya wanahija kutoka Mabaraza ya Maaskofu wa Nchi za Scandinavia. 2025.02.03 Papa Francisko akutana na makumi elfu ya wanahija kutoka Mabaraza ya Maaskofu wa Nchi za Scandinavia.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko kwa wanahija wa Scandinavia:Bwana daima ni mwaminifu kwa ahadi zake!

Katika nyakati hizi za vita,tunahitaji ushuhuda wa upatanisho.Yamo katika hotuba ya Papa akikutana na waamini wa Sweden,Norway,Denmark,Finland na Iceland,katika hija yao,Roma na kuhimiza wakirudi katika nchi zao,"kushirikisha ndugu wengine wa Kikristo,kukuza mazungumzo ya kidini, miale ya makaribisho na mshikamano wa kindugu na wahamiaji.”Kwa vijana,amekumbusha kutangaza kwa Carlo Acutis kuwa Mtakatifu tarehe 27 Aprili 2025

Na Angella Rwezaula – Vatican.


Ndugu Maaskofu na marafiki! Ninayo furaha kuwasalimu ninyi nyote kutoka nchini Sweden, Norway, Denmark, Finland na Iceland katika hafla ya hija yenu mjini Roma, iliyoandaliwa na Baraza la Maaskofu wa Kaskazini. Ninaomba kwamba, kupitia uzoefu huu wa kutembea pamoja kama kaka na dada katika Kristo, mioyo yenu itaimarishwa katika imani, tumaini na upendo, kwa sababu haya ni mambo matatu, muhimu ya maisha ya Kikristo, njia tatu ambazo Roho Mtakatifu hutuongoza katika safari yetu ya hija, kwa sababu sisi ni mahujaji (rej. Katekesi, 24 Aprili 2024). Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko alianza hotuba yake akikutana na kundi hilo mjini Vatican, Jumatatu tarehe 3 Februari 2025 mjini Vatican.

Baba Mtakatifu akiendelea alisema kuwa Kauli mbiu ya Jubilei hii, kama wanavyojua vyema, ni "Mahujaji wa Matumaini." Kwa njia hiyo basi aliomba kwamba tumaini lao liimarishwe katika siku hizi. Hakika tayari wamefahamu dalili za matumaini zilizopo katika nchi zao za asili, kwa sababu Kanisa, katika nchi zao, ingawa ni ndogo, linaongezeka kwa idadi. Na daima linakua. Tunaweza kumshukuru Mungu Mwenyezi, kwa sababu mbegu za imani, zilizopandwa na kumwagiliwa huko na vizazi vya wachungaji na watu wanaovumilia, zinazaa matunda. Wala hili halipaswi kutushangaza, kwa sababu Bwana daima ni mwaminifu kwa ahadi zake! Mnapotembelea sehemu mbalimbali takatifu za Mji wa Milele, hasa makaburi ya mitume watakatifu Petro na Paulo, ninawaombea pia kwamba imani yenu kwa Bwana Yesu na utambuzi wenu wa kuwa wake na wa mtu mwingine katika ushirika wa Kanisa utamwilisha kwa kina.”

Papa wa Roma alisisitiza kuwa “Kwa njia hii, kwa akili na moyo wako ukiwa umeshikamana kikamilifu zaidi na neema ya Kristo igeuzayo, utaweza kurudi katika nchi zako ukiwa umejawa na shauku ya furaha ya kushiriki zawadi kuu uliyopokea, kwa sababu, kama Mtakatifu Paulo asemavyo, sisi. waliumbwa katika Kristo kufanya matendo mema (rej. Efe 2:8-10). Kwa hakika, hakuna “kazi” kubwa zaidi ya ile ya kusambaza ujumbe wa wokovu wa Injili kwa wengine, na tumeitwa kufanya hivyo hasa kwa wale wanaojikuta pembezoni. Lakini sasa, "kazi" imekuja kuwaokoa, na Injili imechukua injini, na kinyume chake, injini imeacha kufanya kazi. Kiukweli, nakumbuka niliiona moja kwa moja wakati wa ziara yangu nchini Sweden mnamo 2016. (Na kwa sisi nchi za Amerika ya Kusini, wakati wa udikteta - Brazil, Uruguay, Chile, Argentina - kaka na dada zetu walikwenda huko ambao walikuwa wakikimbia udikteta. Kwa hiyo Papa amewaomba waendelee kuwa vinara wa ukaribisho na mshikamano wa kidugu!

Hatimaye, neno moja kwa mahujaji vijana walikuwa miongoni mwao. Papa alisema: kama sehemu ya matukio ya mwaka huu, tarehe 27 Aprili tutaadhimisha Kutangazwa Mtakatifu kwa Mwenyeheri Carlo Acutis. Walipiga makofu… Papa akawauliza je mnajua?... "Mtakatifu huyu kijana wa nyakati zenu na nyakati zetu anawaonesha ninyi na sisi sote jinsi inavyowezekana katika ulimwengu wa leo kwa vijana kumfuata Yesu, kushiriki mafundisho yake na wengine na hivyo kupata utimilifu wa maisha katika furaha, katika uhuru na katika utakatifu." Baba Mtakatifu amerudia kuwaomba vijana washirikishe wenzao nyumbani maneno ya Papa kuwa “Roho Mtakatifu awasukume, awasukume [...]Kanisa linahitaji shauku yenu mawazo yenu, imani yenu. Tunaihitaji! (Christus vivit, 299). Kwa njia hiyo Papa Francisiko kwa kuhitimisha alisema pamoja na tafakari hizo fupi, aliwatakia kila la kheri katika hija na maisha yao, na aliwakabidhi kwa maombezi ya Maria, Mama wa Kanisa. Aliwabariki kutoka moyoni mwake na wakati huo huo akawaomb wasisahau kumuombea.

Papa akutana na wanahija kutoka makanisa ya Ulaya Kaskazini
03 Februari 2025, 12:23