Tafuta

2025.02.03: Viongozi wa kimataifa  Wahudhuria Kongamano la Haki za Watoto. 2025.02.03: Viongozi wa kimataifa Wahudhuria Kongamano la Haki za Watoto.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko:haki,ndoto na mahitaji ni kilio cha kimya cha Utoto uliokandamizwa!

Leo hii,zaidi ya watoto milioni 40 wamekimbia makazi yao kutokana na migogoro na takriban milioni 100 hawana makazi.Kuna janga la utumwa wa watoto:takriban watoto milioni 160 ni waathiriwa wa kazi za suluba,waathiriwa wa usafirishaji haramu ya binadamu,nyanyaso na unyonyaji wa kila aina,pamoja na ndoa za kulazimishwa.Ni katika hotuba ndefu ya Papa tarehe 3 Februari katika Uzinduzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu watoto:'Tuwalinde na tuwapende.'

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baada ya utuangulizi wa Askofu  Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mashirika ya Kimataifa, kama mratibu katika uzinduzi wa Kongamano la kimataifa kuhusu haki za watoto tarehe 3 Februari 2025 katika moja ya ukumbi wa makumbusho mjini Vatican, Baba Mtakatifu Francisko alianza na salamu kwa  Malkia Rania Al Abdulaha wa Jordan, kwa Makardinali na watu maarufu waliokuwapo katika fursa hiyo na ambayo inaongozwa na kauli mbiu: “Tuwapende na kuwalinda.” Papa Francisko aliwashukuru  kwa kukubali mwaliko huo na kuwa na imani kwamba, kwa kushiriki uzoefu na ujuzi wao, wataweza kufungua njia mpya za kuokoa na kulinda watoto ambao haki zao zinakanyagwa na kupuuzwa kila siku. Hata leo, maisha ya mamilioni ya watoto yametiwa alama na umaskini, vita, kunyimwa shule, ukosefu wa haki na unyonyaji. Watoto na vijana katika nchi maskini zaidi, au wale waliosambaratishwa na migogoro mibaya, wanalazimika kukabili majaribu mabaya. Hata ulimwengu tajiri zaidi hauzuiliwi na ukosefu huu wa haki. Ambapo, shukrani kwa Mungu, hakuna mateso kutokana na vita au njaa, hata hivyo kuna vitongoji vigumu, ambapo watoto wadogo mara nyingi ni waathirika wa udhaifu na matatizo ambayo hatuwezi kudharau.

Picha ya pamoja  watoto katika fursa ya Kongamano kuhusu haki za watoto
Picha ya pamoja watoto katika fursa ya Kongamano kuhusu haki za watoto

Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa kiukweli, kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko hapo awali, shule na huduma za afya zinapaswa kushughulika na watoto ambao tayari wanakabiliwa na matatizo mengi, na vijana wenye wasiwasi au huzuni, na vijana ambao wanageuka kwa uchokozi au kujidhuru. Zaidi ya hayo, kulingana na utamaduni wa ufanisi, utoto wenyewe, kama ilivyo uzee, "umewekwa pembezoni" ya uwepo wao. Mara nyingi zaidi na zaidi, wale ambao wana maisha yao mbele yao hawawezi kuyaangalia kwa ujasiri na mtazamo mzuri. Vijana, ambao ni ishara za matumaini katika jamii, hujitahidi kutambua matumaini ndani yao wenyewe. Hii inasikitisha, na inatia wasiwasi. "Kwa upande mwingine, wakati wa  mstakabali  ujao hauna uhakika na hauwezi kupenyeza kuwa ndoto, wakati kusoma hakutoi fursa yoyote na ukosefu wa kazi au kazi thabiti ya kutosha huhatarisha kuondoa matamanio, ni jambo lisiloweza kuepukika kwamba maisha ya sasa yanaishi kwa huzuni na kwa uchovu"(Spes non confundit, 12).

Kongamano kaLimataifa kuhusu haki za watoto mjini Vatican
Kongamano kaLimataifa kuhusu haki za watoto mjini Vatican

Jambo ambalo tumeona kwa bahati mbaya karibu kila siku katika siku za hivi karibuni halikubaliki: watoto wanaokufa chini ya mabomu, waliotolewa sadaka kwa sanamu za nguvu, itikadi, na masilahi ya kitaifa. Kiukweli, hakuna kitu kinachofaa maisha ya mtoto. Kuua watoto wadogo inamaanisha kukataa siku zijazo. Katika baadhi ya matukio, watoto wenyewe wanalazimika kupigana chini ya ushawishi wa madawa ya kulevya. Hata katika nchi ambazo hakuna vita, jeuri la magenge linakuwa hatari sawa kwa watoto na mara nyingi hwaacha mayatima na kutengwa. Hata ubinafsi uliopitiliza wa nchi zilizoendelea una madhara kwa watoto wadogo. Wakati fulani wanadhulumiwa au hata kukandamizwa na wale wanaopaswa kuwalinda na kuwalisha; ni wahanga wa kinzani, dhiki ya kijamii au kiakili na hutumiaji wa madawa ya kulevya wazazi wao. Watoto wengi hufa kama wahamiaji baharini, au jangwani au kwenye njia nyingi za safari za kukata tamaa za matumaini. Wengine wengi hushindwa na ukosefu wa matunzo au aina mbalimbali za unyonyaji.

Ni hali tofauti, lakini tunajiuliza swali moja: inawezekanaje kwamba maisha ya mtoto lazima yaishe hivi? Hapana. Haikubaliki na tunapaswa kupinga hali hii. Utoto ulionyimwa ni kilio cha kimya kinachokemea uovu wa mfumo wa kiuchumi, uhalifu wa vita, ukosefu wa huduma za matibabu na elimu ya shule. Kwa ujumla wa dhuluma hizi zina uzito hasa kwa wadogo na wanyonge. Ndani ya mashirika ya kimataifa huitwa "mgogoro wa kimaadili wa kimataifa."Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa leo tuko hapa kusema kwamba hatutaki hii iwe kawaida mpya. Hatuwezi kukubali kuzoea hili. Baadhi ya mienendo ya vyombo vya habari inaelekea kufanya ubinadamu kutojali, na kusababisha ugumu wa ujumla wa mawazo. Wana nia iliyofungwa. Tuna hatari ya kupoteza kile ambacho ni bora zaidi katika moyo wa mwanadamu: huruma na upole.  Papa amesisitiza kuwa zaidi ya mara moja imeezekana kushiriki pamoja wasiwasi huu na baadhi yao ambao ni wawakilishi wa jumuiya za kidini.

Kongamano la Kimataifa kuhusu haki za watoto
Kongamano la Kimataifa kuhusu haki za watoto

Leo hii, zaidi ya watoto milioni arobaini wamekimbia makazi yao kutokana na migogoro na takriban milioni mia moja hawana makazi. Kuna janga la utumwa wa watoto: takriban watoto milioni mia moja na sitini ni waathiriwa wa kazi za kulazimishwa, waathiriwa wa usafirishaji haramu ya binadamu, unyanyasaji na unyonyaji wa kila aina, pamoja na ndoa za kulazimishwa. Kuna mamilioni ya watoto wahamiaji, wakati mwingine na familia zao lakini mara nyingi wakiwa peke yao: hali ya watoto wasio na wazazi inazidi kuwa ya mara kwa mara na mbaya. Watoto wengine wengi wanaishi katika hali duni kwa sababu hawakusajiliwa wakati wa kuzaliwa. Inakadiriwa kwamba watoto milioni mia moja na hamsini "wasioonekana" hawajulikani uwepo wao kisheria. Hiki ni kikwazo cha kupata elimu au huduma ya afya, lakini zaidi ya yote kwao hakuna ulinzi wa sheria na wanaweza kudhulumiwa au kuuzwa kwa urahisi kama watumwa.

Na hii hutokea. Papa amesisitiza tena kuwa “Hii hutokea.” Tunawakumbuka watoto  wadogo wa  Warohinghya, ambao mara nyingi wanahangaika kuandikishwa, watoto wasio na hati katika mpaka na Marekani, wahanga wa kwanza wa msafara huo wa kukata tamaa na matumaini ya maelfu ya watu wanaokuja kutoka Kusini kwenda Marekani, na wengine wengi. Kwa bahati mbaya, historia hii ya ukandamizaji wa watoto inajirudia yenyewe: ikiwa tunawauliza wazee, babu na bibi, juu ya vita walivyopata walipokuwa wadogo, janga linalotoka kwenye kumbukumbu zao ni giza, kila kitu ni giza wakati wa vita, karibu rangi kutoweka, harufu ya kuchukiza, baridi; njaa, uchafu, woga, maisha ya upotovu, kufiwa na wazazi, kuachwa ujane na ugane, kila aina ya vurugu. Papa Francisko amebanisha kuwa“Nilikua na historia za Vita vya Kwanza vya Kidunia, zilizosimuliwa na babu yangu, na hii ilifungua macho na moyo wangu kwa hofu ya vita. Kutazama kwa macho ya wale ambao walipata vita ni njia bora ya kuelewa thamani isiyo na kifani ya maisha.”

Watoto  ni kiini  cha kongamano la kimataifa mjini Vatican.
Watoto ni kiini cha kongamano la kimataifa mjini Vatican.

Lakini kusikiliza watoto ambao leo hii wanaishi katika vurugu, unyonyaji au ukosefu wa haki pia husaidie kuimarisha ile yak sema "hapana" yetu kwa vita, kwa utamaduni wa kupoteza na faida, ambayo kila kitu kinanunuliwa na kuuzwa bila heshima au kujali maisha ya wengine walio wadogo na wasio na kinga. Kwa jina la mantiki hii ya upotevu, ambayo binadamu anakuwa muweza wa yote, maisha machanga hutolewa sadaka kwa njia ya mauaji ya kutoa mimba. Hutoaji  mimba huchukua maisha ya watoto na kukataa chanzo cha matumaini kwa jamii yote. Papa Francisko kwa washiriki hao wa kongamano aliwaeleza kuwa, “ni muhimu kusikiliza: lazima tutambue kwamba watoto wadogo wanazingatia, wanaelewa na kukumbuka. Na kwa sura zao na ukimya wao wanazungumza nasi. Hebu tuwasikilize!” Papa amewashukuru na kuwatia moyo kuwa watumie vyema, kwa msaada wa Mungu, fursa ya mkutano huo. Ameomba  kwamba mchango wao unaweza kusaidia kujenga ulimwengu bora kwa watoto, na kwa hivyo kwa kila mtu!Kwa Papa inampatia matumaini kwamba wako hapo, pamoja, kuweka watoto katikati, haki zao, ndoto zao, mahitaji yao ya siku zijazo. Amewashukuru wote na Mungu awabariki!

Hotuba ya Papa katika Kongamani kuhusu haki za watoto
03 Februari 2025, 09:59