Tafuta

Nia za Papa Francisko kwa mwezi Februari 2025:kuombea miito ya kipadre na kitawa!

Katika ujumbe kwa njia ya video wa Baba Mtakatifu wa nia ya maombi kwa mwezi Februari,uliochapishwa tarehe 4 Februari 2025 kwa njia ya Mtandao wa kimataifa,Papa anaomba kusali kwa ajili ya miito ya maisha ya upadre na kitawa.“Ikiwa tutawasindikiza katika safari zao,tutuona jinsi Mungu anavyofanya mambo mapya kwao.Na tunaweza kupokea wito wake kwa namna ambazo zinahudumia vizuri Kanisa na Ulimwengu wa leo hii.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

“Tusali ili Jumuiya ya kikanisa ipokee matamanio na mashaka ya vijana ambao wanahisi kuitwa kuhudumia katika utume wa Kristo katika maisha ya kikuhani na kitawa.” Ndivyo baba Mtakatifu anaomba kwa njia ya video iliyochapishwa tarehe 4 Februari 2025 na Mtandao wa Kimataifa kwa nia za Baba Mtakatu kila mwezi. Katika ujumbe wake kwa lugha ya kispanyola, Papa anelezea hata wito wake wa kuitwa binafsi kwamba: “Nilipokuwa na miaka 17 nilikuwa mwanafunzi na ninafanya kazi, nilikuwa na mipango yangu. Sikuwa najua kabisa kwamba nitakuwa kuhani. Na ni siku moja nilikwenda katika Parokia… hapo kulikuwa na Mungu, ananisubiri!”

Baba Mtakatifu Francisko aelezea juu ya wito kwamba “Mungu anaendelea kuita vijana hata leo hii, kwa mikitadha mingi, kwa mitindo ambayo hatuwezi kuifikiria. Wakati mwingine hatumsikilizi kwa sababu tunahangaikia na kujazwa na mambo mengi, mipango yetu, hadi kufikia mambo ya Kanisa letu. Lakini Roho Mtakatifu anatuzungumza nasi kwa njia za ndoto, na anazungumza nasi kupitia mahangaiko ambayo vijana wanahisi katika mioyo yao.”

Kwa upande wa Papa anatoa hata ushauri kwamba “Ikiwa tutawasindikiza katika safari zao, tutuona jinsi Mungu anavyofanya mambo mapya kwao. Na tunaweza kupokea wito wake kwa namna ambazo zinahudumia vizuri Kanisa na Ulimwengu wa leo hii.” Kadhalika Papa anaongeza kusisitiza kuwa “Tuwaamini vijana! Na hasa kwa kuamini katika Mungu kwa sababu Yeye anaita kila mmoja! Tusali kwa sababu jumuiya ya Kanisa ipokee matamanio na mashaka ya vijana ambao wanahisi wito wa kuishi utume wa Yesu katika maisha: iwe maisha ya kikuhani kama ilivyo maisha ya kitawa,” anahitimisha Papa

Askofu Mkuu wa Los Angeles:utume wa Kanisa ni kutembea na vijana

“Mungu wetu ni Mungu anayechukua maisha na zawadi za vijana kwa uzito." Haya ni maoni ya Askofu Mkuu José H. Gómez, wa Los Angeles kuhusiana na nia za Papa kwa mwezi huu. “Utume wa Kanisa ni kutembea pamoja na vijana ili kuwasaidia kukua katika imani na kujitahidi kuugeuza ulimwengu huu kuwa Ufalme ambao Mungu anatamani uwe kwa watu wake, aliendelea Askofu wa Jimbo kubwa zaidi nchini Marekani, ambaye alichangia utengenezaji wa video hii na wataalamu wa timu yake ya kidigitali.

Mkurugenzi wa Mtandao wa maombi ya Papa:sote tunaweza kusindikiza 

Na kwa upande wa Mkurugenzi wa Kimataifa wa Mtandao wa Maombi ya Papa Ulimwenguni Pote, Padre Cristóbal Fones, S.J., akimbuka kwamba “kutumaini vijana ni muhimu kwa ajili ya kuwahimiza kuchunguza kwa uhuru wito wao wenyewe na kuuitikia ujasiri. Mtazamo wa uchungaji wa ufundi ambao unathamini kweli mazungumzo na kusindikiza lazima pia kujumuisha wasiwasi, maswali na matarajio madhubuti ya vijana kama sehemu muhimu ya mchakato wa ufundi. Zaidi ya hayo, Papa anatukumbusha kwamba, kupitia maneno ya vijana – ambao wakati mwingine hutuchokoza na kutuweka katika matatizo - Mungu anaweza kutuonesha njia mpya
kwa ajili ya Kanisa leo, na hata kutupatia nafasi kwa ajili yetu wenyewe ile ya uongofu. Katika maisha ya kila siku sote tunaweza kusindikiza na utambuzi wenye mitazamo minne ya msingi: uwazi, kusikiliza, kujitoa bure, ukaribu na maslahi. Kwanza kabisa, lazima tujifungue kwa ajili ya utume wa kuhamasisha miito, bila kufunga njia ambazo Mungu mwenyewe hufungua.”

Hii ni muhimu hasa katika familia, aliendelea Padre Fones na kisha, ni muhimu kujenga mazingira katika jumuiya ambapo sauti ya Mungu inaweza kusikika, kuwakaribisha na kuwaheshimu wale wanaohisi hamu ya kumfuata Kristo katika maisha ya kuwekwa wakfu au ukuhani. Vivyo hivyo, tunapaswa kuwa karibu, kwa busara na mshikamano, tukitoa ushuhuda wetu. Hatimaye, kupendezwa kwa dhati kwa kila mtu husaidia kufungua mioyo. Na mitazamo yetu inaweza kuwa na maamuzi kwa vijana ambao wanataka kujibu Bwana katika safari hii na hawajui jinsi ya kuifanya." Hii ni thamani ya kukumbuka kwamba moja ya masharti muhimu ya kupata msamaha uliotolewa katika hafla ya Jubilei ya 2025 ni ya kuwaombea.

Mtandao wa Maombi ya Papa Ulimwenguni kote

Nia za Papa kwa mwezi Februari
04 Februari 2025, 16:39