Tafuta

Siku ya mababu,mabibi na wazee 2025 ni tarehe 27 Julai. Siku ya mababu,mabibi na wazee 2025 ni tarehe 27 Julai.  (Vatican Media)

Mada ya Siku ya Wazee Ulimwenguni 2025:Heri ambaye hajapoteza matumaini yake!

Matumaini ndiyo moyo wa Jubilei kwa 2025 ambapo pia yanakuwa njia iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu kwa ajili ya Siku ya V ya mababu na wazee Ulimwenguni itakayoadhimishwa tarehe 27 Julai 2025.Kauli mbiu ya siku hiyo inatoka katika Kitabu cha Sira ili kuonesha tumaini katika Bwana kama njia ya Mkristo na upatanisho na uzee.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baraza la Kipapa kwa ajili ya Walei, Familia na Maisha, limechapisha kauli mbiu inayoongoza Siku V ya Babu, bibi na Wazee Ulimwenguni itakayoadhimisha tarehe 27 Julai 2025. Katika taarifa hiyo inabainisha kuwa: “Baba Mtakatifu alichagua mada ya Maadhimisho ya Siku ya Tano ya Mababu na Wazee Ulimwenguni ambayo mwaka huu itaadhimishwa Dominika tarehe 27 Julai kwa kuongozana kifungu cha Biblia: “Heri ambaye hajapoteza matumaini yake” (taz Sir 14:2). Maneno haya, yaliyotolewa katika kitabu cha Sira, yanaonesha baraka za wazee na kuonesha katika tumaini lililowekwa kwa Bwana katika njia ya Mkristo na kupatanishwa na uzee.

Kila Parokia mahalia kuhakikisha inafanyika maadhimisho haya 

Siku ya wazee Duniani 27 Julai 2025
04 Februari 2025, 17:12