Tafuta

2025.01.25 Washiriki wa Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano(24-26 Januari 2025). 2025.01.25 Washiriki wa Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano(24-26 Januari 2025).  (Vatican Media)

Changamoto ya kuwa wawasilishaji wa matumaini

Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano imepita,lakini maombi ya Papa la kuhamasisha njia mpya za kuwasiliana zinakwenda zaidi ya tukio la Jubilei. Kwa upande wa Papa Fransisko,ni lazima tuweke historia za wema katikati na kushinda vishawishi vya uandishi fulani wa habari ambao huelekea kutoa nafasi ya uovu tu.

Alessandro Gisotti

Muwe wahamasishaji wa matumaini. Muwe wasimulizi wa historia nzuri. Baba Mtakatifu Francisko alizindua changamoto hii kwa wanamawasiliano ulimwenguni kote, waamini na wasioamini katika maadhimisho ya Jubilei inayotolewa kwa ajili yao. Kwa wawasilianaji wote, kwa hivyo, sio waandishi wa habari tu. Kwa upande wa  Papa, kiukweli, mawasiliano sio tu kwa taaluma muhimu ya uandishi wa habari. Mtazamo wake juu ya mawasiliano ni wa digrii 360, na sio wa "uzalishaji wa habari" tu , lakini ni mwelekeo muhimu wa mwanadamu, unaohusisha moyo na akili. Kwa sababu hiyo, mawasiliano ya matumaini ambayo Papa Fransisko aliitaka katika Jubilei hiyo  yanakuwa changamoto ya dharura  na si kwa waandishi wa habari tu, bali kwa wale wote ambao mioyoni mwao wanajali ubinadamu unaozidi kujeruhiwa na ghasia na dhuluma.

Kwa kuzingatia eneo la mawasiliano kuwa pana zaidi ya lile la habari, Papa Fransisko kwa hakika anajiunganisha na yule ambaye, baada ya Mtaguso, alikuwa mhamasishaji wa Siku ya Kimataifa ya Hupashanaji habari, yaani: Mtakatifu Paulo VI. Kwa hakika, Papa Montini, ingawa alifahamu vyema jinsi vyombo vya habari vilivyoathiri maisha ya watu na Kanisa lenyewe,  alitaka maadhimisho ya kila mwaka yawekwe  kwa ajili ya wafanyakazi wote wa mawasiliano,  na sio wanataaluma wa habari tu. Kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake mpendwa, mawasiliano kwa  mujibu wa Papa Francisko  sio kitendo cha utendaji tu . Ni “malighafi” ya kuwepo kwa mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni kiumbe anayependwa na Mungu, ambaye huwasiliana naye tangu mwanzo. Kutoka moyoni hadi moyoni. Kila mawasiliano ya mwanadamu, kwa hiyo, yanaingizwa katika mzunguko wa mawasiliano ya kimungu. Hakika, tangu mwanzo wa upapa wake, Jorge Mario Bergoglio daima amekuwa akisisitiza umuhimu wa mawasiliano ya “ moyo".

Katika jumbe zake za hivi karibu za  Siku ya Hupashanaji Habari Ulimwenguni, alirudia mtindo wa: kusikiliza, kuzungumza, kutazama, lakini pia kila wakati kufanya hivyo kwa moyo. Hata katika Ujumbe wake kwa Siku ya Hupashanaji kunako 2024, uliojikita juu ya Akili Mnemba , alitaka kusisitiza kwamba hata kama mashine zitasonga mbele katika maendeleo yake  ya kiteknolojia, hakuna kitu kinachoweza kuchukua nafasi ya moyo wa mwanadamu unaowaonea huruma wanadamu wenzake. Zaidi ya  yote, katika Biblia tunaposoma "moyo" haturejei chombo, na sehemu tu, bali katikati ya mwanadamu, mahali ambapo hisia, ndoto na hofu huzaliwa. Kwa hivyo moyo ni mtu mzima na  siyo kipande. Katika Ujumbe wake wa kwanza  wa Siku ya Hupashanaji habari  Ulimwenguni Papa Francisko alionesha Msamaria Mwema kama kielelezo cha mwasilianaji  mwema. Nguvu kubwa ya mfano huo, aliandika:  “ni nguvu ya ukaribu,” yaani, kujua jinsi ya kuwafikia wengine, hasa wale wanaoteseka, bila ubaguzi. Na kwa hivyo kujihatarisha kwa ajili yao.

Katika Mawasiliano ambayo huzaa matumaini, Papa anatuambia kwa wito wa kujitolea, kuwa hauwezi kujiwekea kikomo katika kusambaza habari, lakini lazima uwe na uwezo wa kuingia katika uhusiano wa kina na wengine, kuleta neno la faraja na matumaini. Kwa kifupi, haitoshi kuwasilisha ukweli, aliwaambia waandishi wa habari kutoka ulimwenguni  kote katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican kuwa lazima pia tuwe wa kweli. Lakini Papa alimaanisha nini alipozungumzia matumaini? Kwanza kabisa, si udanganyifu wa kutufanya tujisikie vizuri au dawa ya ganzi ili kutuzuia tusiteseke. Hii siyo hata mtazamo wa matumaini. Tumaini, ambalo kwa Mkristo lina uso na moyo wa Yesu, hutupatia mwelekeo, hutufanya kutazama juu kwa ujasiri kuelekea kile ambacho bado hatuwezi kuona.

Akimnukuu Václav Havel: mwenye kutumaini anafikiri kwamba kila kitu kitakuwa sawa, wakati mwenye matumaini anajua kwamba,  hata kama kila kitu hakiendi vizuri, lakini  kila kitu kina maana. Kuwa na mwelekeo wa kweli. Kwa hiyo tumaini, kwa Papa Francisko, ni zawadi inayotoka kwa Mungu, lakini pia ni kazi, kama Madeleine Delbrêl alivyosisitiza, ambaye anatutaka kuchukua jukumu la waliotupwa. Kwa hivyo tumaini la Kikristo,  kama Papa alivyokumbuka kwa shauku katika Misa ya mkesha wa  Noeli , mara tu baada ya kufungua Mlango Mtakatifu katika Kanisa la Mtakatifu Petro - hutufanya tusiwe na utulivu, hututikisa kutoka katika uvivu wetu, na huvunja maeneo yetu tunayofikiri ni mazuri.  Ni fadhila "hatari."Ni kitendo cha kuwajibika kwa wengine. Je, wawasilianaji wanaweza kufanya nini basi, kuanzia na wale wa maongozo ya Kikristo, kueneza tumaini hili ambalo, kama Charles Peguy angetuambia, kuwa hatuwezi kufanya bila  hilo ikiwa tunataka kuishi maisha yetu kikamilifu kama Wakristo?

Katika Ujumbe wake kwa Siku ya Hupashanaji habari Ulimwenguni  kwa  Mwaka huu  2025 wa Jubilei, Baba Mtakatifu Francisko anaakisi jinsi gani, katika ulimwengu uliojawa na upotovu wa taarifa, mawasiliano yanapaswa kuwa njia ambayo matumaini hupita. Katika Sala ya Malaika wa Bwana  tarehe 26 Januari 2025 wakati akisalimiana na wana mawasiliano waliokuwepo uwanja wa Mtakatifu Petro , aliwataka wawe "wasimulizi wa matumaini." Na siku iliyofuata, tarehe 27 Januari 2025 akikutana na wakuu wa mawasiliano wa Mabaraza ya Maaskofu wa nchi mbalimbali, duniani, aliongeza kipande kingine cha uzuri huo  aliposema kuwa “kila Mkristo anaitwa kuona na kusimulia historia za mema ambazo uandishi wa habari mbaya hujaribu kufuta kwa kutoa nafasi kwa maovu tu.” Kwa upande wa Papa, kuwasilisha matumaini ni hivi: kutafuta na kusimulia historia  za mema. Kuzingatia uzoefu wa tumaini wanaoishi kila siku na watu wa kawaida, na wale watakatifu wa karibu ambao wanazungumza nasi mara nyingi katika miaka ya hivi karibuni.

Katika wakati ambao unaonekana kusahau hata kidogo, Papa anatualika kutoa sauti kwa wale waliokata tamaa na kutoa cheche hizo za mwanga zinazoangaza hata katika pembe za giza zaidi za ubinadamu. Papa anatuhimiza kuzitafuta hizo cheche za matumaini hata kama zimewekwa kwenye Matope. Ni ahadi kwa Mwaka Mtakatifu, lakini lazima iendelee baadaye. Kwa sababu, kama alivyosema wakati mmoja kuwa, "kila historia ni nzuri na ya kustahili, na hata ikiwa ni mbaya, ikiwa heshima itafichwa, inaweza kutokea kila wakati."

Gisotti: Kutangaza habari zenye matumaini
04 Februari 2025, 10:59