Tafuta

Watu nchini Ukraine wanateseka na baridi na hawana umeme. Watu nchini Ukraine wanateseka na baridi na hawana umeme.  (ANSA)

Papa:Tusisahau Ukraine,fikirieni watoto na vijana wanaoteseka kwa baridi na nchi Takatifu

Mwishoni mwa Katekesi ya Papa Francisko,tarehe 27 Novemba 2024 mawazo yake bado ni kwa wanaoteska nchi za Mashariki mwa Ulaya kutokana vita na kukosa joto. Papa aliwaomba hata watoto wasali kwa ajili ya wenzao wanaoteseka.Alitoa wito wa amani katika Mashariki ya Kati ambako watu wanateseka sana na kutangaza tafsiri katika lugha ya Kichina katika katekesi ya Jumatano.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika salamu mbali mbali kwa mahujaji kutoka sehemu mbali mbali za dunia, walioudhuria Katekesi yake, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumatano tarehe 27 Novemba 2024, aliwakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano. Hasa, ninawasalimu Waabuduo wa Kudumu wa Sakramenti Takatifu, waamini wa Madhabahu ya  Mtakatifu Rocco huko Grisolia, vikundi kutoka Mtakatifu  Ferdinando wa Puglia na washiriki katika Siku za Mafunzo  kuhusu Mtakatifu Yohane Paulo II. Papa amewakaribishwa  kwa moyo mkunjufu wanafunzi wa shule, hasa wale kutoka Corato, Barletta, Andria na Mtakatifu Antonio Abati. Na aliwasalimu kwa namna ya pekee watoto waliokuwapo mbele yake na kuwashukuru kwa uwepo wao. Hatimaye, mawazo yangu yaliwaendea vijana, wagonjwa, wazee na wenye ndoa wapya Papa amesema: “Majilio ya Dominika ijayo yanaanza, kwa maandalizi ya Kuzaliwa kwa Kristo. Ninawasihi nyote muishi “wakati huu wenye nguvu” kwa maombi ya utii na tumaini motomoto.”

Lugha ya Kichina katika Katekesi ya Papa

Papa Francisko alitoa tangazo kuhusu  tafsiri ya lugha ya Kichina katika  katekesi ya Jumatano kwamba “Juma lijalo, katika kipindi cha majilio  tafsiri katika  lugha ya Kichina ya muhtasari wa Katekesi itaanza,”Papa ameeleza.

Kuombea Ukraine nchi Takatifu

Papa Francisko akiendelea amebainisha kuwa :“Na tusisahau watu wa Kiukreine wanaoteswa. Wanateseka sana. Akiwageukia kundi la watoto kutoa Shule ya Mtakatifu Michel huko Batignolles mjini Paris, Ufaransa  waliokuwa wameketi karibu naye, alisema “Na ninyi watoto, vijana, fikirieni watoto wa Kiukraine na vijana ambao wanateseka wakati huu, bila joto, na baridi kali sana. Waombee watoto na vijana wa Kiukraine. Je, mtafanya hivyo? Je, mtaomba? Nyinyi nyote. Msisahau. Papa Francisko kisha alitoa wito kwa ajili ya amani katika Mashariki ya Kati ambako alisema: “Na pia tuombee amani katika Nchi Takatifu; Nazareti, Palestina, Israeli… Amani iwe na amani. Watu wanateseka sana. Tuombe amani sote kwa pamoja.”

Bada ya Katekesi
27 November 2024, 11:48