Tafuta

Papa Francisko:furahini na furaha ya Yesu mioyoni mwetu!

Sisi sote lazima tuwe na upendo,wavumilivu,wanyenyekevu,watendao amani na sio vita.Wakati mwingine kutakuwa na wakati wa huzuni,lakini kuwe na amani kila wakati.Kwa Yesu kuna furaha na amani.Furaha ya kweli inashirikishwa na wengine.Kwa hiyo tuwe na furaha na furaha ya Yesu kati yetu.Ndiyo ushauri wa Papa wakati wa Katekesi ya Jumatano tarehe 27 Novemba 2024.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika mzunguko wa Katekesi, kuhusu mada ya “Roho na Mchumba. Roho Mtakatifu anaongoza Watu wa Mungu kukutana na Yesu Tumaini letu” Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 27 Novemba 2024 amejikita na sehemu ya 15 kuhusu Matunda ya Roho Mtakatifu ambayo ni 'Furaha.' Kabla ya kuanza tafakari,  Somo lilisomwa katoka Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Wafilipi lisemalo: “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”(Fil 4,4-7). Baba Mtakatifu Francisko amenaza kutafakari kwamba baada ya kuzungumza juu ya neema ya utakaso na kisha juu ya karama, alipenda kujikita na ukweli wa tatu. “Neema ya kwanza ni kutakasa; pili, karama na ya tatu ni ipi? Ukweli” unaohusishwa na utendaji wa Roho Mtakatifu  wa  “matunda ya Roho ambayo ni mambo ya ajabu.

Tunda la Roho ni nini? Aliuliza swali na kuendelea kusema kuwa “ Mtakatifu Paulo anatoa orodha yake katika Waraka kwa Wagalatia. Yeye anaandika kuwa  “Muwe makini  mwangalifu: “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi” (5,22). Maneno tisa haya ni matunda ya Roho. Lakini“tunda la Roho ni nini? Tofauti na karama, ambazo Roho humpatia yeyote atakaye na anapotaka kwa manufaa ya Kanisa, matunda ya Roho kwa msisitizo ni upendo, furaha, amani, uungwana, fadhili, uaminifu, upole, utu wema na kiasi ambavyo ni  matokeo ya ushirikiano kati ya neema na uhuru wetu. Matunda haya daima yanaonyesha ubunifu wa mtu, ambamo “imani hutenda kazi kwa njia ya mapendo” (Gal 5:6), wakati mwingine kwa njia ya kushangaza na ya furaha. Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa si kila mtu katika Kanisa anaweza kuwa mtume, si kila mtu anaweza kuwa nabii, si kila mtu anaweza kuwa mwinjili, si kila mtu; lakini kila mtu bila ubaguzi anaweza na lazima awe mfadhili, mvumilivu, mnyenyekevu, mpatanishi na kadhalika. Lakini sisi sote, ndiyo, lazima tuwe wafadhili, wavumilivu, wanyenyekevu, watendao amani na sio vita.”

Miongoni mwa matunda ya Roho yaliyoorodheshwa na Mtume, Papa Francisko amependa pia kuakisi moja akikumbuka maneno ya ufunguzi ya Waraka wa Kitume wa  Evangelii gaudium(Injili ya furaha): “Furaha ya Injili inajaza mioyo na maisha yote ya wale wanaokutana na Yesu. Wale wanaojiruhusu kuokolewa naye wanawekwa huru kutokana na dhambi, huzuni, utupu wa ndani na kutengwa. Pamoja na Yesu, furaha daima huzaliwa na kupyaishwa”( 1). Papa ameongeza kusema “Lakini wakati mwingine kutakuwa na wakati wa huzuni, japokuwa  kuna amani kila wakati. Kwa Yesu kuna furaha na amani.” Furaha, na tunda la Roho,  kwa pamoja na kila furaha ya mwanadamu mwingine hisia fulani ya utimilifu na kuridhika, ambayo hutufanya tuitake idumu milele. Tunajua kutokana na uzoefu, hata hivyo, kwamba hii haifanyiki hivyo  kwa sababu kila kitu hapa duniani  kinapita haraka. Kila kitu kinakwenda haraka. Hebu tufikirie pamoja: vijana, hupita haraka, afya, nguvu, ustawi, urafiki, upendo ... Tutaishi miaka mia moja, lakini basi ... hakuna cha zaidi. Vyote vinapita upesi.

Papa amesema kwamba zaidi ya hayo, hata kama mambo haya hayatapita hivi karibuni, baada ya muda hayatoshi tena, au hata kuwa ya kuchosha, kwa sababu, kama Mtakatifu Agsotino alivyosema akimwambia Mungu: “Ulituumba kwa ajili yako, Bwana, na mioyo yetu haina utulivu mpaka itakapotulia ndani yako.” Kwa njia hiyo kuna kutotulia kwa moyo ili kutafuta uzuri, amani, upendo, furaha. Furaha ya Injili, furaha ya kiinjili, tofauti na furaha nyingine yoyote, inaweza kupyaishwa kila siku na kuwa ya kuambukiza. “Shukrani pekee kwa kukutana au kukutana tena  na upendo wa Mungu, ambao unageuka kuwa urafiki wa furaha, tunakombolewa kutoka katika dhamiri yetu iliyotengwa na kujirejea. [...] Ni sifa mbili za tunda la furaha la Roho: sio tu kwamba haziko chini ya uchakavu usioepukika wa wakati, lakini zinazidisha kwa kushirikishana na wengine! “Furaha ya kweli inashirikishwa na wengine; huambukizwa pia. Katika karne tano zilizopita, aliishi Mtakatifu hapa Roma aitwaye Philip Neri. Yeye alijulikana  katika historia kama mtakatifu wa furaha.  Papa ameomba kusikiliza kwa makini kuwa alikuwa “mtakatifu wa furaha.” Kwa watoto maskini na walioachwa katika Kituo chake aliwambia kuwa: “Watoto, changamkeni; Sitaki aibu au huzuni; Inatosha kwangu kuona hutendi dhambi.”  Na tena: “Muwe wema, kama mtaweza.”

Hata hivyo, haijulikani sana ni chanzo gani ambacho furaha yake ilitoka. Mtakatifu Filipo Neri alikuwa na upendo wa namna hiyo kwa Mungu kiasi kwamba wakati mmoja alionekana kama moyo wake unataka kupasuka kifuani mwake. Furaha yake ilikuwa, kwa maana kamili, tunda la Roho. Mtakatifu alishiriki katika Jubilei ya 1575, ambayo aliiboresha kwa mazoezi, ambayo alidumisha baadaye, ya kutembelea Makanisa Saba. Katika wakati wake, alikuwa Mwinjilishaji wa  kweli kupitia furaha. “Na ilikuwa hiyo hasa  ya Yesu ambaye alisamehe kila wakati, alisamehe kila kitu. Labda baadhi yetu wanaweza kufikiri: "Lakini nilifanya dhambi hii, na hii haitasamehewa ..."Papa ameomba wasikilize kwa makini kwamba “Mungu husamehe kila kitu, Mungu husamehe daima. Na hii ni furaha: kusamehewa na Mungu, lakini kusamehe kila kitu na siku zote." Neno “Injili” linamaanisha habari njema." Papa alikazia.

Kwa hiyo mtu hawezi kuwasiliana na uso uliokunyata na nyuso za giza, lakini kwa furaha ya wale ambao wamepata hazina iliyofichwa na lulu ya thamani. Hebu tukumbuke himizo ambalo Mtakatifu Paulo aliwaambia waamini wa Kanisa la Filipi, ambapo anatuambia sisi sote leo hii kama tuliyoyasikia hapo mwanzo kwamba: “ Furahini katika Bwana sikuzote, nawaambieni tena: furahini. Fadhili zako na zijulikane kwa wote” (Wafilipi 4:4-5). Papa Francisko amahitimisha kwa kukazia juu ya furaha kwamba: “Wapendwa kaka na dada, furahini na furaha ya Yesu mioyoni mwetu.”

Katekesi ya Papap
27 November 2024, 11:47