Tafuta

2024.11.25 Kardinali Miguel Angel Ayuso Guixot 2024.11.25 Kardinali Miguel Angel Ayuso Guixot 

Imam Mkuu wa Al-Azhar atoa rambi rambi kwa Papa kwa kifo cha Kard.Ayuso Guixot

Imamu Mkuu wa Al-Azhar, Al-Sharifalimtumia pole kwa Papa Francisko kwa kuondokewa na Kardinali Miguel Ángel Ayuso,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini,kilichotokea tarehe 25 Novemba 2024.Imam alisema Kardinali Ayuso alikuwa kielelezo mashuhuri cha huduma iliyojitolea kwa ubinadamu,akikubali juhudi kubwa katika kukuza uhusiano na Waislamu kwa ujumla,huko Al-Azhar na Baraza la Wazee la Waislamu (MCE).

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika salamu za Rambi rambia, kutoka kwa Profesa Ahmad At-Tayyeb, Imamu Mkuu wa Al-Azhar, HH  kwa Papa Francisko na kwa Kanisa lote Katoliki kufuatia na  kifo cha Kardinali Miguel Ángel Ayuso, Mwenyekiti  wa Baraza la Kipapa la Majadiliano kati ya Dini, kilichotokea tarehe 25 Novemba 2024, kiongozi huyo anatoa pole na kumwomba Mwenyezi Mungu awapatie subira na faraja familia, jamaa na wapendwa wa marehemu.” Imamu Mkuu alisema kwamba Kardinali Ayuso alikuwa kielelezo mashuhuri cha huduma iliyojitolea kwa ubinadamu, akikubali juhudi kubwa za Marehemu  katika kukuza uhusiano na Waislamu kwa ujumla, na Al-Azhar na Baraza la Wazee la Waislamu (MCE) hasa. Kiongozi huyo aidha aliakisi jukumu kuu la Kardinali Ayuso katika kukuza na kusambaza Hati ya Udugu wa Kibinadamu (HFD) wakati wa huduma yake  mjini Vatican na michango yake kwa Kamati ya Juu ya Udugu wa Kibinadamu.‎

Alikuwa mwenye burasa na mkarimu

Kwa hakika Mtu mwenye busara, mkarimu, mwenye akili nyingi na maarifa na imani kubwa. Mara nyingi alionekana akitembea kupitia Njia ya  Conciliazione akiwa na nia ya kuomba kwa sauti ya chini huku akielekea ofisini kwake. Hivi ndivyo wengi wanavyomkumbuka Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, ambaye alizimika  akiwa na umri wa miaka 72. Alikuwa amelazw katika hospitali Kuu ya Gemelli . Hata hivyo tarehe 25 Novemba  Papa, wakati wa hotuba yake kwa ujumbe wa kimataifa wa Jain ambapo wawakilishi wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini walikuwapo alikuwa amemtaja Kardinali wa Hispania kuwa: “Afya ni mbaya sana, yuko mwisho wa maisha yake.”

Patriaki wa Wakatoliki wa Kikoptiki ametoa rambirambi

Kwa niaba ya Baraza la Mapatriaki na Maaskofu nchini Misri, taasisi na mashirika yote ya Kikatoliki na kwa niaba yangu binafsi, ninapenda kutoa rambirambi zangu za dhati kwa kuondokewa na Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, Mwenyekiti wa  Baraza la Majadiliano ya Kidini huku nikihakikisha kwamba tunatoa rambirambi, kwa  muungano wangu katika maombi katika wakati huu wa matumaini makubwa ya Ufufuko. Kanisa linainua sala kwa Bwana ili kumkaribisha katika Ufalme wake wa amani na furaha ya milele. (Pariaki Anba Ibrahim Isaac SEDRAK, Patriaki wa Alexandria wa Wakatoliki wa  kikoptic, Rais wa Baraza la Mapatriaki na Maaskofu nchini Misri.)

Mazishi 27 Novemba 2024

Mazishi ya Kardinali Ayuso yatafanyika tarehe 27 Novemba  2024 saa 8 alasiri katika  Madhabahu ya Kanisa Kuu la  Mtakatifu Petro. Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya Liturujia imeabainisha kwamba maadhimisho yataongozwa na  Kardinali Giovanni Battista Re, Decano wa Makardinali pamoja na Makardinali, Maaskofu wakuu na Maaskofu. Na hatimaye Ibadan a sala za mwisho zitaongozwa na  Papa Francisko (Ultima Commendatio na Valedictio.)

Rambi rambi kuondokewa na Kard.Ayuso
26 November 2024, 15:52