Tafuta

Mama Yetu ni Aparecida. Mama Yetu ni Aparecida. 

Papa,Brazil:Ulimwenguni bado kuna vivuli vingi dalili za kujifungia binafsi

Katika Ujumbe kutoka kwa Papa Fransisko kwa ajili ya kampeni inayohamaishwa na na Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Brazil kuhusu mada:“Udugu na Urafiki wa Kijamii”,iliyoanza tarehe 14 Februari, katika siku ya kwanza ya kipindi cha Kwaresima:“Duniani bado kuna vivuli vingi na kujifungia.Lazima tuendeleze upendo kwa kila kiumbe hai, kushinda vizuizi vya jiografia.”

Vatican News

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya Kampeni ya Udugu, mpango wa kila mwaka wa mshikamano unaohamaishwa kila mwaka wakati wa kipindi cha Kwaresima  na Baraza la Maaskofu nchini Brazil  (Cnbb). Katika Ujumbe huo, Papa Francisko anawageukia kaka na dada wa Brazil kuwa wakati tunaanza na kufunga, toba na sala katika safari ya Kwaresima amaungana na Kaka zake wa Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Brazil katika wimbo wa kushukuru neema kwa aliyejuu kwa mwaka wa 60 wa Kampeni ya Udugu mchakato wa uongofu ambao unaunganisha imani na maisha, kiroho na jitihada za kidugu, upendo kwa Mungu na upendo kwa jirani, hasa kwa yule aliye mdhaifu na mwenye kuhitaji umakini.  Mchakato huo umependekezwa kila mwaka na Kanisa nchini Brazil na kwa watu wote wenye mapenzi mema katika taifa pendwa hilo.

Baba Mtakatifu Francisko katika Ujumbe huo amesema kwamba “Mwaka huu, mada iliyochaguliwa “ Udugu na Urafiki Kijamii na  kauli mbiu, “ Ninyi nyote ni kaka na dada (Mt 23,8), maaskofu wa Brazil wanaalika watu wote wa Brazil kutembea , kipindi cha Kwaresima katika safari ya uongofu unaojikita juu ya Waraka wa Fratelli tutti, ambao niliutia saini huko Assisi tarehe 3 Oktoba 2020, katika mkesha wa kumbu kumbu ya Liturujia ya Mtakatifu Francis.” Kama kaka na dada, Papa anasema tunaalikwa kujenga udugu wa kweli wa ulimwengu kwa kusaidia maisha yetu ya kijamii na kuhishi kwetu katika Ardhi Nyumba Yetu ya Pamoja , bila kupoteza mtazamo wa Mbinguni mahali ambapo Baba atatupokea wote kama wana na binti zake.

Baba Mtakatifu Francisko amekazia kusema kuwa “lakini kwa bahati mbaya, katika ulimwengu tunaona bado kuna vivuli vingi, dalili za kujifunga binafsi. Kwa njia hiyo, ninakumbusha hitaji la kupanua mzunguko wetu ili kufikia wale ambao kwa hiari hatujisikii kuwa sehemu ya ulimwengu wetu wa masilahi(rej. Ft, 97), kupanua upendo wetu kwa “ kitu kilicho hai”(Ft 59), kushinda mipaka na kushinda “vizuizi vya jiografia na nafasi”(Ft, 1).

Ni matarajio ya Baba Mtakatifu kwamba Kanisa nchini Brazil litaweza kupata matunda mazuri katika safari hii ya Kwaresima na anawatakia matashi mema  ili Kampeni ya Udugu, kwa mara nyingine tena, iwasaidie watu na jumuiya za taifa hilo pendwa katika mchakato wao wa kuongoka kwa Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo, kushinda kila mgawanyiko, kutojali, chuki na vurugu. Baba Mtakatifu Francisko, anamkabidhi matakwa haya kwa utunzaji wa Mama Yetu wa Aparecida,  na kama ahadi  ya neema nyingi za mbinguni, anawakirimia kwa hiari wana na mabinti wote wa taifa pendwa la Brazil, hasa wale wanaojizatiti katika udugu wa wote, Baraka ya Kitume,  huko akiwaomba waendelee kumuombea.

Ujumbe wa Papa kwa Kanisa la Brazil: katika Kampeni ya Kwaresima.
14 February 2024, 16:40