Papa na Ushirika wa Italia waishi kwa upendo ulio hai&bila moyo hakuna maarifa ya mwanadamu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 5 Januari 2024 akikutatana na Wanachama wa Unicoo na Mfuko wa “Il cuore si scioglie” wa Firenze nchini Italia katika fursa ya miaka 50 ya huduma kwa wanajamii wanaohitaji sana na kumi ya kuundwa kwa mfuko, alianza kumshukuru Rais na wote. Papa amefurahi kukutana nao, kwa wingi wao kwani walikuwa karibia 3,500 hivi, katika mkesha wa Tokeo la Bwana Epifania. Papa amesema kuwa: “Sikukuu hii, kama kipindi kizima wa Noeli inatuita kusherehekea fumbo la Umwilisho wa Bwana: katika Mtoto Yesu tunaona jinsi Mungu alivyokuwa karibu nasi katika umaskini wetu (Rej. Fp 2:6-7), akionesha kama njia iliyobahatika kukutana naye. Na muktadha huu wa kiroho pia ni muhimu kwa ahadi yao, ambayo kwa miaka 50, kama Ushirika, na kwa zaidi ya kumi, kama Mfuko imekuwa ikilenga watu wenye uhitaji zaidi, katika maeneo mbalimbali ya huduma: kutoka umaskini wa kiuchumi hadi mahitaji, kwa ajili ya utamaduni, kwa walio upweke hadi hitaji la elimu, kutumia, pamoja na njia za kawaida za msaada wa kifedha na chakula, zana zingine nyingi, kama vile kupanda mlima, fasihi, sanaa na muziki.” Kwa njia hiyo amewashukuru kwa hilo.
Kwa kunukuu katika Mkataba wao Papa Francisko alisema: “Unicoop-Firenze ilianzisha ili kulinda maslahi ya watumiaji, afya zao na usalama pia kwa kuongeza na kuboresha taarifa zao na elimu” (n. 2). Kwa kufanya hivyo, mnamo mwaka wa 2010 alitoa uhai kwa Wakfu wa Mfuko wa “Il cuore si scioglie”, uliokusudiwa kuwatia moyo watu kufanya jambo fulani kwa ajili ya wengine” na kwa hiyo “ tunaweza kusema, kwa kutumia usemi wa kibiblia, kuhimiza uundaji wa “mioyo ya nyama” badala ya “mioyo ya mawe: (rej. Ez 36,36). Na hili ni jambo zuri sana: moyo ni chanzo cha maarifa. Mtu ataniambia: “Lakini, hapana, Padre, tunajua kwa akili, kwa akili". Hii, peke yake, ni ujuzi usio kamili.” Papa aliongeza. “Bila moyo hakuna maarifa ya mwanadamu. Ili kujua, lazima tujue kwa akili, kwa moyo na kisha kufanya kwa mikono: mssisahau lugha tatu ... Akili iunganishwe na moyo na mikono, moyo uunganishwe na roho na mikono, kwa kufanya na kwa akili; na kwamba mikono iwe kwenye huduma ya moyo na akili. Msisahau hili, ninyi katika matendo yenu ...”
Papa Francisko amependa kujikita na kutafakari na juu ya thamani ya safari hiyo. Kiukweli, kwa kuzingatia ulinzi wa watumiaji juu ya kipengele chake rahisi cha kibiashara tangu mwanzo, wamefikia kufahamu mwelekeo wa kimsingi wa kibinadamu: ule wa kusaidia kila mtu kufanya jambo kwa ajili ya wengine, yaani, kuishi hisani, upendo ulio hai (Rej. Fratelli tutti, 87). Kwa njia hiyo, kukumbuka kulinda wema wa mtu haimaanishi kutunza baadhi ya masilahi ya kisekta tu, bali kukuza utambuzi wao kamili na hadhi. Na katika ngazi hiyo mkutano kati ya wale walio na uwezekano mkubwa zaidi na wale ambao wako katika umaskini, mbali na kupunguzwa kwa uhisani tu, daima hufanya fursa ya riziki ya kutajirishana. Kwa hivyo wanapendekeza mfano wa ulinzi ambao unaunganisha watu binafsi na sio sana dhidi ya tishio la adui wa kawaida, bali kwa ajili ya ujenzi wa uhusiano mzuri wa kusaidiana (rej. FT, 215). Na Wanafanya haya yote kwa ubunifu mwingi, kama inavyotokea wakati wanafanya kazi pamoja kwa kuhuishwa na ndoto ya kawaida za pamoja.
Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa “Kuwa karibu na watu tunaowasaidia: ametoa mfano: “Mimi, wakati, wa maungamo, wakati mwingine huwauliza watu: “Je unatoa sadaka, unasaidia?” “Ndiyo, ndiyo” Papa a,eomgeza: “Na niambie, je unapotoa sadaka, unamtazama mtu huyo machoni, unamgusa mkono, au unatupa pesa hizo hapo kisha unafanya hivyo”. Kwa ushauri Papa ameongeza: "Gusa, gusa umaskini, kwa mguso, moyo unaogusa; kwa kutazama na kuelewe. Msisahau hili.” Papa amewashukuru kwa kile wanachofanya, nchini Italia na nje ya nchi; hasa, katika wakati huu wa kushangaza, kwa kuunga mkono Ukraine inayoteswa: ni ya kutisha, nini kinatokea huko! Asante kwa ushirikiano wao na Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo ambao wao wamesaidia shughuli zake kwa muda. Waendelea kulenga, katika kazi yao, katika maendeleo fungamani ya mtu, ukuaji wa jamii katika ugawanaji wa rasilimali na ujuzi, kwa kujumuisha kwa kuimarisha kile ambacho kila mtu analepta, kwa manufaa ya wote. Papa amewabariki na kuwatakia kila la kheri kwa mwaka ulioanza hivi karibuni. Na tafadhali, wasisahau kumuombea lakini sio dhidi ya, eh?”