Tafuta

Mwisho wa Mwaka 2023 ni muda muafaka kumwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shukrani kwa mema mengi ambayo amewakirimia wanadamu katika maisha yao, kipindi chote cha mwaka mzima wa 2023. Mwisho wa Mwaka 2023 ni muda muafaka kumwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shukrani kwa mema mengi ambayo amewakirimia wanadamu katika maisha yao, kipindi chote cha mwaka mzima wa 2023.   (ANSA)

Heri na Baraka Tele Kwa Mwaka 2024: Neno la Mungu

Mwisho wa Mwaka 2023 ni muda muafaka kumwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shukrani kwa mema mengi ambayo amewakirimia wanadamu katika maisha yao, kipindi chote cha mwaka mzima wa 2023. Ni wakati wa kushukuru pia hata kwa matendo yaliyosababishwa na binadamu, kiasi kwamba, kuna idadi kubwa ya waathirika wa vita sehemu mbalimbali za dunia. NI muda kwa waamini kujizatiti katika Sala, Tafakari ya Neno la Mungu na Matendo ya huruma.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 27 Desemba 2023 ameanza mzunguko mpya wa Katekesi kuhusu fadhila na mizizi ya dhambi mambo msingi katika kuulinda moyo. Katika katekesi yake amekazia kuhusu dhambi na vishawishi vya dhambi, usithubutu kamwe kufanya majadiliano na Shetani, Ibilisi na kwamba, kila mwamini anapaswa kuulinda moyo wake. Anasema, maadhimisho ya Sherehe ya Fumbo la Umwilisho yanasaidia kukuza na kuimarisha imani kati ya wabatizwa, ili hatimaye, waweze kuwa ni vyombo na mashuhuda wa amani sanjari na upendo wa Mungu ulimwenguni.  Kuzaliwa kwa Kristo Yesu, Mwana wa Mungu aliye hai ni mwanzo wa Injili ya matumaini ambayo Mwenyezi anawakirimia waja wake na kwamba, mwisho wa siku upendo utashinda nguvu za giza na dhambi!

Vita inasababisha mateso na mahangaiko kwa watu wa Mungu
Vita inasababisha mateso na mahangaiko kwa watu wa Mungu

Baba Mtakatifu anakaza kusema, Mwisho wa Mwaka 2023 ni muda muafaka kumwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shukrani kwa mema mengi ambayo amewakirimia wanadamu katika maisha yao, kipindi chote cha mwaka mzima wa 2023. Ni wakati wa kushukuru pia hata kwa matendo yaliyosababishwa na binadamu, kiasi kwamba, kuna idadi kubwa ya waathirika wa vita sehemu mbalimbali za dunia. Waamini wasichoke kumwomba, Kristo Yesu, Mfalme wa amani, ili aweze kuwakirimia: Matumaini, upendo na amani ya kweli. Waendelee kujiaminisha mbele ya Mungu, kwani anawapenda upeo na anawatakia mema ya nchi.

Kristo Yesu Mfalme wa amani daima anatembea na waja wake
Kristo Yesu Mfalme wa amani daima anatembea na waja wake

Sherehe hizi ziwe ni kielelezo cha furaha kwa kutambua kwamba, Mwenyezi Mungu yuko daima kati kati yao, na anatembea pamoja nao! Waamini waendelee kutunza ndani mwao furaha ya Noeli kwa sala, tafakari ya Neno la Mungu na matendo ya huruma kwa Mungu ambaye kwa njia ya Fumbo la Umwilisho, amekuwa karibu sana na binadamu wote. Baba Mtakatifu Francisko anawatakia waamini na watu wote wenye mapenzi mema heri na baraka tele kwa Mwaka 2024, uwe ni mwaka wa baraka ya Mtoto Yesu. Neno la Mungu liwe ni taa na mwongozo wa maisha ya waamini katika kipindi chote cha Mwaka 2024. Kamwe waamini wasichoke wala kusahau kuwakumbuka na kuwaombea waathirika wa vita sehemu mbalimbali za dunia.

Baraza za Mwaka 2024
27 December 2023, 13:20