Tafuta

Papa Francisko wakati anasalimia umeti katika Uwanja wa  Velodrome huko Marsiglia nchini Ufaransa Septemba 23,2023. Papa Francisko wakati anasalimia umeti katika Uwanja wa Velodrome huko Marsiglia nchini Ufaransa Septemba 23,2023.  (Vatican Media)

Papa:Wakatoliki wahamasike kwa uwazi na azma katika nyanja ya kijamii

Katika ujumbe wake uliotiwa saini na Kardinali Parolin,Papa Francisko akiwahutubia washiriki wa Kongamano la Jula la Kijamii,Ufaransa,linaloendelea mjini Lyon,ameonesha“hofu ya muktadha unaotia wasiwasi wa kukosekana kwa utulivu wa kimataifa na kutoa wito wa kujitolea kuunda mafungamano ya kijamii,udugu na upatanisho kati ya vikundi na jamii."

Vatican News

Muktadha wa wasiwasi wa ukosefu wa utulivu wa kimataifa unaonesha haja ya uwiano wa kijamii, udugu na upatanisho kati ya makundi na jumuiya. Hayo ndiyo tunayosoma katika ujumbe kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko, uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican  uliotumwa kwa washiriki wa mkutano wa Juma za  Kijamii Ufaransa, unaoendelea mjini Lyon hadi tafungamani, kulingana na mafundisho ya Papa Francis, ambayo wakati huo huo yanashughulikia migogoro ya kijamii na kimazingira na yanatuhimiza kutotenganisha kile ambacho kina uhusiano wa karibu, ujumbe huo unasomeka.

Kulinda kazi ya uumbaji ni kazi ya kila mtu

Katika ujumbe huo unanukuu vifungu kutoka katika Waraka wa  Laudate Deum, ambapo Papa anakumbusha kwamba "kujitolea kwa kibinafsi kwa ulinzi wa uumbaji" peke yake hakutoshi "kushughulikia mgogoro wa hali ya tabianchi tunayokabiliana nayo sasa." Kinachohitajika ni mchakato mpya ambao siasa pia inahusika, pamoja na watendaji mbalimbali wa kijamii na vyombo vya kati. Kwa hiyo mwaliko unaotoka katika Waraka wa Kitume wa Fratelli tutti "kujenga jamii iliyohuishwa na hisia za urafiki na udugu unakuwa pendekezo thabiti la kuchunguza aina mpya za ushirikiano."

Wakatoliki wanapaswa kuhamasishwa katika nyanja ya kijamii

Uwepo wa Papa katika  Mkutano wa COP28 huko Dubai ni ushuhuda, kama tunavyosoma zaidi, "wa ahadi yake ambayo inawahimiza Wakatoliki wote kuhamasisha kwa uwazi na uamuzi katika nyanja ya kijamii". Ni imani inayowafunga “wanafunzi wa Bwana kwa undani zaidi kwenye hatima ya wanadamu, ya viumbe vyote hai na ya nyumba yetu ya pamoja”. Shauku  kwa wale waliohudhuria mkutano huo ni kwamba mtazamo wao  "usaidie Kanisa la Ufaransa katika utume wake", na kwamba tumaini lao linaweza kuwa kubwa kama "upya wa Bwana Yesu" ambao "unang'aa hasa kati ya maskini, walio mbali sana, kutoka katika mantiki ya nguvu, ambapo Ufalme wa Mungu tayari unabadilisha mawazo na mioyo na kuandaa maisha yetu ya baadaye".

24 November 2023, 15:51