Papa:ukatili na maumivu katika Ukraine,karibu na watu ambao wanatetea utambulisho wao
Vatican News
Jioni ya Jumanne tarehe 21 Novemba 2023, Baba Mtakatifu Francisko alifika kwenye Ukumbi mpya wa Sinodi saa 12.30, wakati wa tukio la onesho ya filamu yenye kichwa, “Freedom on Fire: Ukraine’s fight for freedom,” yaani Uhuru juu ya moto. Ukraine inapambania huru, ya mtunzi Evgeny Afineevsky, ambayo ilifanyika mbele ya baadhi ya wanadiplomasia, miongoni mwao akiwemo Mwanadiplomasia, Balozi wa Ukraine anayeakilisha nchi yake mjini Vatican, wageni wa Italia na wageni wengine wa kimataifa. Ni habari zilitotolewa na Msemaji wa Vyombo vya habari mjini Vatican, Dk. Matteo Bruni.
Kwa mujibu wa Msemaji huyo kwa waandishi alisema kuwa Papa alikaa hadi mwisho wa onesho hilo baada ya kimya cha dakika moja katika sala kwa ajili ya waathiriwa wa mzozo huo na hotuba fupi ya mkurugenzi, alihutubia baadhi ya maneno ya salamu kwa washiriki, na kuwashukuru kwa kutoa ushuhuda huo.
Kwa njia hiyo maumivu mengi hayo alisema tena"Vita ni kushindwa kila wakati" alikumbuka kuwa na sisi, ambao tumeona ukatili huo, watu hawa wanaotetea utambulisho wao, lazima tuwe karibu na mateso mengi na kuwaombea watu hawa, tuombe amani ifike". Kabla ya kuondoka, Baba Mtakatifu kwa hiyo aliwasalimia baadhi ya wageni mmoja mmoja na kisha akarejea Nyumba ya Mtakatifu Marta.