Papa Francisko Pango langu.Ninawasimulia wahusika wa Noeli
Na Angella Rwezaula, -Vatican.
Tarehe 21 Novemba 2023 kimechapishwa kitabu cha Papa Francisko chenye kichwa Pango langu. Ninawasimulia wahusika wa Noeli ambacho kinapatika katika Duka la vitabu la Vatican. Kitabu zaidi ya kuwa katika lugha ya kiitaliano pia ni katika lugha nyingine za kifaransa, kiingereza na kireno. Vile vile hata lugha nyingine zitatoloewa za toleo la Kihispania, kijerumaini na kislovenia. Kitabu hicho chenye utangulizi wa Papa Francisko ni moja ya mfululizo wa vita vya tafakari, hotuba na mahubiri ambayo Baba Mtakatifu amejikita nayo kuelezea pango na wahusika wake katika miaka hii ya Upapa wake. Ufuatayo ni utangulizi wa kitabu hicho kutoka kwa Papa Francisko.
Francisko
Mara mbili nilitamani kwenda kutembelea Greccio. Kwa mara ya kwanza ilikuwa ni kwenda kufahamu mahali ambapo Mtakatifu Francis wa Assis alibuni utengenezaji wa pango, jambo ambalo liligusa hata utoto wangu kwani katika nyumba ya wazazi wangu huko Buenos Aires hapakukosekana kamwe ishara hii ya Noeli, mapema kabla ya mti wa Noeli. Kwa mara ya pili nilirudi kwa utashi katika mahali hapo, leo hii ni Wilaya ya Rieti ili kutia saini ya Barua ya Kitume ya Admirabile signum juu ya maana na pango leo hii lina maana gani. Fursa zote hizi mbili nilihisi kufunguliwa kwa namna ya pekee hisia ya groto mahali ambapo unashangaa michoro ya Enzi za Kati ambazo zilikuwa zinaonesha usiku wa Betlehemu na ile ya Greccio, iliyochorwa na msanii sawa na hiyo. Hisia zile za kutazama zilinisikuma kujikita kwa undani fumbo la kikristo ambaye anapenda kujificha ndani ya kile ambacho ni kidogo sana. Kiukweli, kufanyika mwili kwa Yesu Krito, kunabaki moyo wa onesho la Mungu hata kama kunasahuliwa kirahisi kwamba kuinama ni unyeti hivyo hadi kupita bila kuzingatiwa. Udogo, kwa hakika ni njia ya kukutana na Mungu.
Katika moja ya andiko epitaph katika kaburi la Mtakatifu Ignatius wa Loyola tunakuta wameandika: Non coerceri a maximo, sed contineri a minimo, divinum est, yaani Usiogope mambo makubwa, lakini wakati huo huo kuzingatia madogo. Ni ya kimungu kuwa na wazo ambalo haliwezi kuzuiwa na kitu ambacho kipo, lakini wazo ambalo kwa wakati huo huo lipo na limeishi katika mambo madogo zaidi ya maisha. Kwa njia hiyo hatupaswi kuogopa mambo makubwa, inahitajika kwenda mbele na kuzingatoa mambo ambayo ni madogo zaidi. Na tazama sababu ya kuwa na utunzaji wa roho ya pango inageuka kuwa afya ya kina iliyo katika uwepo wa Mungu ambaye anajiionesha katika wadogo, na zaidi yasiyozingatiwa na matendo yaani mambo ya kila siku. Kujua kukataa kile ambacho kina adaa, lakini kinapeleka katika njia mbaya, ili kueleka na kuchangua nji za Mungu ni kazi ambayo inatusubiri. Katika mapendekezo hayo, ni zawadi kubwa ya utambuzi na sio lazima kamwe kuchoka kumuomba katika sala. Wachungaji katika pango ni wale ambao walipokea kwa mshangao wa Mungu na wakaishi kwa mshangao wa kukutana naye, wakumuabudu, katika udogo wakajua uso wa Mungu. Kibinadamu, wote tumeinamia kutafuata makubwa, lakini ni zawadi ya kujua kuupata kweli, kujua kutafuta ukuu katika ule udogo ambao Mungu anaupenda sana.
Mnamo Januari 2016 nilikutana na Vijana wa Rieti hasa pale katika kijito cha Mtoto Yesu, juu karibu sana na Madhabahu ya Pango. Kwa vijana hao na leo hii wote, niliwakumbusha kuwa katika usiku wa Noeli kuna ishara mbili ambazo zinatuongoza katika kumjua Yesu. Ya kwanza ni ile ya mbingu iliyojaa nyota. Ni nyingi sana, ni idadi isiyoisha, ile ya nyota, lakini kati yao inajitokeza nyota maalum, ile ambayo ilisukuma Mamajusi kuondoka kutoka katika nyumba zao na kuanza safari, mwendo ambao wao walikuwa hawajuhi ni wapi wangeweza kuelekea. Inajitokeza hivi hata katika maisha yetu. Wakati mwingine nyota maalum inatualika kuchukua maamuzi, kufanya uchaguzi, na kuanza mwendo. Kwa Mungu tunapaswa kwa nguvu zote kumuomba atufanye kuona ile nyota ambayo inatusukuma kuelekea jambo fulani zaidi zaidi ya mazoea yetu, kwa sababu ile nyota itatupelekea kutafakari kwa kina Yesu, yule mtoto ambaye anazaliwa huko Betlehemu na ambaye anataka furaha yetu timilifu.
Katika usiku ule Mtakatifu wa kuzaliwa Mwokozi, tunapata ishara nyingine ya nguvu, ile ya udogo wa Mungu. Malaika walielekeza wachungaji mtoto aliyezaliwa katika holi la wanyama. Sio ishara ya nguvu, ya kujitosheleza au ya kiburi. Hata, Mungu wa milele anajifanya kuwa binadamu asiye na ulinzi, mpole na mnyenyekevu. Mungu alijishusha kwa sababu sisi sote tupate kutembea na Yeye na kwa sababu yeye aweze kukaa nasi kandoni mwetu na siyo juu na mbali na sisi. Kustaajabu na mshangao ni hisia mbili ambazo watu wote, wadogo kwa wakubwa, mbele ya Pango kama ambavyo Injili inaishi na liyojaa kurasa nyingi za Maandiko Matakatifu. Sio muhimu jinsi gani ambavyo pango linapambwa, linaweza kuwa daima linafanana au kubadilishwa kila mwaka, kile kinachozingatiwa ni kuzungumza katika maisha.
Katika Wosia wa Kwanza wa Mtakatifu Francis wa Assisi tunamwona mwandishi Tommaso wa Celano anaelezea usiku wa Noeli wa mnamo 1223 ambapo mwaka huu tunaadhimisha miaka 800. Francis alipofika alitafuta makonde ya majani ya wanyama, na punda. Watu walimkimbilia na kuonesha furaha isiyoelezeka, lakini iliyokuwa inaonjwa mapendo mbele ya tamasha la Noeli. Baadaye Padre katika hilo, aliadhimisha Misa Takatifu kwa kuonesha uhusiano kati ya kufanyika Mwili kwa Mwana wa Mungu na Ekaristi. Katika muktadha huo, huko Greccio, hapakuwap na sanamu yeyote ile, bali Pango likatengezwa na kufanya uzoefu kwa wale waliokuwa hapo. Nina uhakika kwamba Pango la kwanza, ambalo lilitengenezwa kwa kazi kubwa ya Uinjilishaji, inaweza hata leo hii kuwa fursa ya kukufua staajabisho na mshangao. Kwa namna hiyo kile ambacho Mtakatifu Francis alianzisha kwa urahisi wa ishara ile, kinabaki hadi leo katika siku zetu, kama aina halisi ya uzuri wa imani yetu.