Papa:Ninashiriki wasiwasi kuhusu maendeleo ya Kanisa nchini Ujerumani
Vatican News
Kwa "wasiwasi" uliooneshwa na wanawake wanne, wataalimungu na mwanafalsafa, juu ya maendeleo ya Kisinodi ya Weg, yaani njia ya Kisinodi ya Kanisa la Ujerumani, ambayo walikuwa wajumbe na kisha kuamua kuacha, Baba Mtakatifu alijibu kwa barua kwamba na Yeye pia ana wasiwasi "kuhusu hatua nyingi za sasa ambazo sehemu kubwa za Kanisa hilo mahalia la liendelea kutishia kusonga mbele zaidi na zaidi kutokana na njia ya kawaida ya Kanisa zima". Baba Mtakatifu aliandika hayo kwenye karatasi kuonesha wasiwasi wake, ambao tayari umeoneshwa katika matukio mengine yaliyotangulia, katika barua iliyotiwa saini , ambamo tarehe 10 Novemba, 2023 iliyoelekezwa kwa wataalimungu wa maadili Katharina Westerhorstmann, Marianne Schlosser, na mwanafalsafa Hanna-Barbara Gerl-Falkovitz na mtangazaji Dorothea Schmidt.
Wasomi hao wanne walimwandikia barua Papa mnamo tarehe 6 Novemba 2023 kueleza mashaka na hofu kuhusu matokeo ya mchakato wa sinodi ya Ujerumani uliohitimishwa katika miezi ya hivi karibuni. Safari iliyohusisha wajumbe 230, wakiwemo maaskofu, mapadre, walei wanaume na wanawake, waliogawanyika katika vikundi vya kazi na kujikita katika kujadili masuala na matatizo kama vile baraka kwa wapenzi wa jinsia moja, mabadiliko ya maadili ya ngono, useja wa kipadre, mamlaka ya ukasisi, migogoro ya ndoa, ubaya wa unyanyasaji, nafasi ya wanawake, kwa kuzingatia hasa ushemasi wa kike na uwezekano wa kuwekwa wakfu kwa wanawake katika ukuhani. Mada zote ziliunganishwa katika hati nne zilizowasilishwa mnamo Machi mwaka huu 2023.
Kuanzishwa kwa kamati ya sinodi
Kinachowatia wasiwasi wajumbe wanne wa zamani wa Sinodi ya Weg ni wazo hasa la kuunda kamati ya sinodi "inayolenga kuandaa kuanzishwa kwa baraza la usimamizi na maamuzi". Papa, akirejea katika barua yake, alisisitiza kwamba chombo hiki "katika hali iliyoainishwa katika maandishi husika ya uamuzi, haiwezi kuoanishwa na muundo wa kisakramenti wa Kanisa Katoliki". Kisha alikumbuka kwamba katiba yake "ilipigwa marufuku na Vatica na barua ya tarehe 16 Januari 2023, iliyoidhinishwa na mimi kwa mtindo maalum", ameaandika Papa Francisko.
Barua kwa Watu wa Mungu wa 2019
Waraka huo pia unawakumbusha Waraka wake kwa Watu wa Mungu ambao wako katia mchakato wa safari nchini Ujerumani, Lettera al Popolo di Dio che è in cammino in Germania, uliochapishwa tarehe 29 Juni 2019: kurasa zipatazo kumi zimegawanywa katika sehemu kumi na tatu, ambapo Askofu wa Roma aliwataka viongozi wa Kanisa nchini Ujerumani kutembea kuelekea njia sahihi, ile ya Injili, bila kuvuka katika mielekeo ya kiutendaji au kupnguiza katika kiitikadi. Barua hiyo pia ilinukuliwa katika tamko la Vatican la tarehe 21 Julai 2021, ambapo ilifafanuliwa kuwa njia ya sinodi haiwezi kufanya maamuzi ya mafundisho. Hiyo ni, haina "uwezo wa kuwalazimisha maaskofu na waamini" kwa "njia mpya za Kanisa na njia mpya za mafundisho na maadili", ilisema maandishi hayo, ambayo yalihitimisha kwa matumaini kwamba mapendekezo mchakato wa njia ya nchini Ujerumani inaweza kuungana katika njia ya sinodi ya Kanisa zima.
Sala, toba na kwenda kukutana na ndugu
Akikumbuka hati yake muhimu, Papa Francisko katika barua kwa wanawake hao wanne ameandika: "Badala ya kutafuta 'wokovu' katika kamati mpya daima na, kwa njia fulani ya kujitegemea, kujadili daima mada sawa, katika Barua yangu kwa Watu wa Mungu ambayo tuko safarini Ujerumani nilitaka kukumbusha hitaji la maombi, toba na kuabudu na kutualika tufunguke na kutoka nje ili kukutana na ndugu zetu, hasa wale ambao wameachwa kwenye kizingiti cha makanisa yetu, mitaani, katika magereza na hospitali, viwanja na miji". "Nina hakika: Bwana atatuonesha njia huko," amesema Papa Francisko. Alimalizia kwa kuwashukuru Westerhorstmann, Schlosser, Gerl-Falkovitz na Schmidt kwa kazi ya kitaalimungu na kifalsafa iliyofanywa na kwa “ushuhuda wao wa imani”: “Tafadhali endeleeni kuniombea na kwa ajili ya kujali kwetu kwa pamoja kwa umoja”. Kuhusu njia ya Sinodi, mkutano ulifanyika tarehe 26 Julai mjini Vatican kati ya Katibu wa Vatica, Kardinali Pietro Parolin, na baadhi ya wakuu wa Mabaraza ya Kipapa na wawakilishi wa Baraza la Maaskofu wa Ujerumani. Huu ulikuwa ni mwendelezo wa mazungumzo yaliyoanza kwa ziara ya kitume ya Maaskofu wa Ujerumani mwezi Novemba 2022, ambapo masuala ya kitaalimungu a na kinidhamu yaliyojitokeza katika Sinodale Weg yaani Sinodi ya Weg yalijadiliwa.
2022, Maaskofu 62 wa Ujerumani walikutana na Papa
Mwaka mmoja uliopita, kama ilivyotajwa, maaskofu 62 kutoka Ujerumani walikutana na Papa kwa muda wa wiki moja; wakati huo huo walikuwa wamekutana na Kadinali Parolin na wakuu wengine wa Mabaraza ya Kipapa kwa ajili ya mkutano wa siri wa kimataifa ambao haujawahi kutokea, uliofafanuliwa na rais wa Baraza la Maaskofu Ujerumani Askuf Georg Bätzing, kama "kesi ya dharura ya kisinodi". Askofu Bätzing mwenyewe, akikutana na waandishi wa habari katika Taasisi ya Augustinianum jijini Roma kuripoti juu ya kazi hiyo, alisema "alifarijiwa" na mazungumzo haya ambayo - alisisitiza - "kila kitu, kilikuwa kimewekwa mezani: ukosoaji, maombi, mapendekezo, kutoridhishwa “kwa Roma” na kuchanganyikiwa. Zaidi ya yote, mikutano na Papa na Curia Romana ilikuwa fursa ya kufafanua kwamba hakuna kukata tamaa kwa upande wa maaskofu wa Ujerumani kuanzisha "mgawanyiko". "Sisi ni Wakatoliki na hilo ndilo tunataka kubaki, alisema Bätzing.