Tafuta

2023.11.23 Tamasha la XIII la Mafundisho Jamii ya Kanisa huko Verona. 2023.11.23 Tamasha la XIII la Mafundisho Jamii ya Kanisa huko Verona. 

Papa:kuwasiliana ni kuhusisha akili,upendo na kusaidia wengine

Katika ujumbe wa uzinduzi wa toleo la 13 la Tamasha la Mafundisho Jamii ya Kanisa huko Verona Italia,Papa Francisko anatualika kutafsiri kwa dhati mafundisho ya Injili katika jamii."#soci@Imente liberi ,ndiyo mada y 2023 na matumaini ya Papa ni katika utamaduni wa kidijitali "hakuna mtu anayeendeleza mawasiliano ya fujo kupitia uenezaji wa jumbe za chuki na upotoshaji wa ukweli mtandaoni."

Na Angella Rwezaula, Vatican.

Mawasiliano hufikia ukamilifu wake katika mchango kamili wa mtu mwenyewe kwa mtu mwingine na ni katika uhusiano huo wa usawa ambapo mtandao wa uhuru unakua. Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko ameandika katika ujumbe wake kwa waandaaji na washiriki wa toleo la XIII  la Tamasha la Mafundisho  Jamii ya Kanisa  lililoanza tarehe 24 Novemba  2023 huko Verona nchini Italia. Siku tatu za mikutano zinazo wajumuisha wataalamu, wajasiriamali, maprofesa na walei waliojitolea kutafsiri kwa kina mafundisho ya Injili katika jamii, kama ilivyotarajiwa pia katika muhtasari wa kikao cha kwanza cha mkutano mkuu wa kawaida wa XVI wa Sinodi. Awali ya yote alimsalimia kwa moyo mkunjufu rais wa Taasisi ya Segni Nuovi, yaani Ishara Mpya, Bwana Alberto Stizzoli ambaye kwa miaka kadhaa, pamoja na kundi kubwa la walei, kamati ya kisayansi na marafiki wanaounga mkono kwa dhati mpango huo, wamekuwa wakiendelea na mpango muhimu wa Tamasha hilo la Mafundisho Jamii ya Kanisa.

Papa Francisko anaandika kuwa Ni nyinyi wataalamu wa kawaida ambao hamjiachi na kuwakilisha mojawapo ya muunganiko ulioonyeshwa katika Ripoti ya Muhtasari wa Kikao cha kwanza cha Mkutano Mkuu wa Kawaida wa XVI wa Sinodi ya Maaskofu (4-29 Oktoba 2023): Kama utume ni neema inayolihusisha Kanisa zima, waamini walei huchangia kwa njia muhimu kuitambua katika mazingira yote na katika hali za kawaida za kila siku. Ni wao juu ya yote wanaolifanya Kanisa lihudhurie na kutangaza Injili katika utamaduni wa mazingira ya kidijitali, ambayo yana athari kubwa duniani kote, katika tamaduni za vijana, katika ulimwengu wa kazi, uchumi na siasa, sanaa na utamaduni, utafiti wa kisayansi, elimu na mafunzo, katika utunzaji wa nyumba ya kawaida na, hasa, katika kushiriki katika maisha ya umma." 

"@", ni ishara ya ukaribu na kukaribiana

Mada waliyohagua  mwaka huu, "#soci@mente liberi", inakumbusha masuala ya sasa hasa ya utamaduni wa kidijitali ambayo huathiri uhusiano kati ya watu na, hivyo basi, washiriki, akili huru  kama ilivyoripotiwa na neno kijamii awali ilionesha kitengo cha kipimo na baadaye  cha kuchukua thamani kubwa  na hivyo kusababisha matumizi ya kawaida katika barua pepe kwa maana ya "@". Kwa hivyo, kutokana na historia ambayo ina ishara za kupata uhuru katika mitandao ya kijamii leo hii. Hii inaoneshwa na ile "ukaribu" ambayo inaonesha kukaribiana, mawasiliano, usemi wa ukaribu wa uhuru, na "kuwekwa" moyoni mwa kila mtu.

Msihamasishe utamaduni wa kutupa kupitia jumbe za chuki

Mtandao tunaotaka, kiukweli, haujafanywa kutega, bali kukomboa, kulinda ushirika wa watu huru. Kanisa lenyewe ni mtandao uliosukwa kwa Ushirika wa Ekaristi, ambapo muungano hautokani na ‘kupenda’, bali kwenye ukweli, juu ya ‘amina’, ambayo kwayo kila mtu anashikamana na Mwili wa Kristo, akiwakaribisha wengine. Ikilinganishwa na kasi ya habari, ambayo husababisha tetemeko la uhusiano, Papa, amesema "amina" kiukweli ni "aina ya uchochezi wa kwenda zaidi ya ujazo wa kiutamaduni ili kutoa utimilifu kwa lugha, kwa heshima kwa kila mtu. Mtu yeyote asiendekeze mawasiliano ya upotevu kupitia uenezaji wa jumbe za chuki na upotoshaji wa ukweli mtandaoni," kwa hiyo ndilo tumaini la Papa.

Yesu anapendezwa na mtu halisi katika utimilifu wake

Mfano wa mawasiliano ya kweli yaliyochochewa na upendo ni kifungu kutoka Injili ya Marko ambacho kinaelezea tukio la kuongezeka kwa mikate na samaki. Watu wapatao elfu tano walimfikia Yesu kwenye ufuko wa Ziwa Tiberia, wakitembea kilometa nyingi ili kumsikiliza. Alianza kuwafundisha mambo mengi na mamlaka yake, inatokana na ushiriki wake binafsi na kutoka kwake kuwa uso na neno la Baba katika mizunguko na zamu ya uwepo wa mwanadamu,  ana huruma kwa watu, yeye ana hisia sawa za watu walio mbele yake, yeye hawadharau, anajofanya matatizo yao kuwa yake, na  anayashughulikia" Papa ameandika. Na kisha anawalisha, kwa sababu "mafundisho yanafuatwa na zawadi ya mkate na chakula kwani Yesu anapendezwa na mtu mhalisi, yaani, mtu katika uadilifu wake. Papa anaandika, "

Kuelimisha katika utamaduni wa kujitoa

Kwa kufanya hivyo, Yesu hayuko peke yake, bali anaomba ushirikiano wa wanafunzi wake, ambao nao wanaombwa ushiriki wa kibinafsi. Huu ndio uhuru ambao mwanafunzi anaitwa kuwa na ule wa wale wanaojihusisha na akili na upendo kusaidia wengine kukua" Kwa hiyo, ni matumaini ya Papa kwamba wawe mashuhuda wa uhuru katika ulimwengu wa uhuru na matakwa kwa washiriki, kuanzia rais wa Segni Nuovi Foundation Alberto Stizzoli - ambaye pamoja na kundi kubwa la walei, kwa Kamati ya Kisayansi, ya kuunga mkono tamasha kikamilifu ni kutafsiri alama ya "soci@mente" katika mipango ya manufaa ya wote" na kuhusisha "katika elimu kuhusu utamaduni wa kutoa.

Papa kwa Toleo la mafundisho ya kijamii
24 November 2023, 17:33