Tafuta

Papa:Kuaminiana kunakomboa na hofu zinagandisha

Papa Franciskoametoa tafakari kuhusu Injili ya Siku inayohusu talanta ambazo amesema zizalishwe kadiri ya ubunifu wetu,bila kuogopa.Woga unagandisha na uaminifu kwa Mungu unaleta uhuru.Sisi sote pia tumepokea talanta za thamani zaidi kuliko pesa.Tusizichimbie ndani ya udongo.

Na Angella Rwezaula- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, ameto tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, baada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la  Mtakatifu Petro na kabla ya kuketi mezani na maskini katika Ukumbi wa Paulo VI, Dominika tarehe 19 Novemba 2023 katika Siku ya Maskini Duniani. Akianza tafakari hiyo amesema Injili ya leo inatuonesha mfano wa talanta (rej. Mt 25:14-30). Bwana anaondoka kwenda safarini na kukabidhi talanta zake, au tuseme mali yake, kwa watumishi wake: talanta zilikuwa kitengo cha pesa. Alizisambaza kulingana na uwezo wa kila mmoja ili atakaporudi aulize hesabu kwa waliyoyafanya. Wawili kati yao wameongeza maradufu yale waliyopokea, na bwana anawasifu, wakati wa tatu, kwa hofu, alizika talanta yake na aliweza kuirejesha hiyo tu,  kwa sababu ambayo alipokea karipio kali.

Siku ya Maskini Duniani
Siku ya Maskini Duniani

Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa kwa kutazama mfano huu, tunaweza kujifunza njia mbili tofauti za kumkaribia Mungu. Njia ya kwanza ni ile ya yule anayezika talanta aliyopokea: hamwamini bwana wake wala yeye mwenyewe. Kwa hakika, anamwambia bwana wake: “Bwana, nalijua ya kuwa wewe ni mtu mgumu, wavuna pasipo kupanda, na kukusanya pale ambapo hukupepeta” (Mt 25, 24). Alimwogopa. Hakuona heshima na imani ambayo bwana aliweka ndani yake, lakini matendo ya bwana ambaye alidai zaidi kuliko yeye alivyotoa, ya hakimu ambaye huweka kivuli cha adhabu zake kali juu ya kushindwa kwa wengine. Baba Mtakatifu Francisko amekazia kusema,  huu ndio mfano wake wa Mungu: mtu hakuweza kumwamini katika wema wake. Ndiyo maana anakwama na hajiruhusu kuhusika katika utume alioupata. Yeye hafanyi ukweli amri ya Mungu wake; kwa hakika, alirudisha kila kitu, akisema: “Hapa, chukua kilicho chako” (Mt 25, 25). Yeye alikuwa na  sura hiyo ya mbali na potofu kuhusu  Mungu.

Papa katikati ya watu na watoto mezani
Papa katikati ya watu na watoto mezani

Papa ameeleza pia njia ya pili, ambayo kwa wahusika wengine wawili, waliolipa kwa uaminifu wa Mungu  wao kwa kumtegemea yeye. Waliwekeza kila kitu ambacho wali pokea, ingawa hawakujua mwanzoni ikiwa kila kitu kitakwenda sawa: walikubali kujihatarisha  na kujiweka kwenye mstari wa mbele. Waliamini na kujihatarisha. Wanategemea ufahamu wa bwana aliyewachagua, juu ya wema wa zawadi iliyokabidhiwa kwao, juu ya ujuzi ambao wamepokea. Hivyo, wana ujasiri wa kutenda kwa uhuru, kwa ubunifu, kuzalisha mali mpya (taz. Mt 25, 20-23). Papa amebainisha  kusema kuwa hapo kuna njia panda tunazokabiliana nazo na Mungu kama zile za  woga au tumaini. Kama wahusika wakuu wa mfano huo, sisi sote pia tumepokea talanta, za thamani zaidi kuliko pesa. Lakini mengi ya jinsi tunavyoziwekeza hutegemea imani yetu kwa Bwana, ambayo huweka huru mioyoni mwetu, hutufanya tuwe watendaji na wabunifu katika wema. Kuaminiana kunaweka huru, hofu hupooza, yaani kugandisha. Hofu huzuia, uaminifu na huzuia uwezo wetu. Na inafurahisha moyo wa Baba, ambaye hufurahi kuona watoto wake ambao hawamwogopi, badala yake wanaompenda.

Jinsi ambavyo meza zilikuwa zimepangwa
Jinsi ambavyo meza zilikuwa zimepangwa

Papa ameongezakwamba lazima kukumbuka kuwa hofu hupooza mtu lakini, uaminifu humweka mtu huru. Na tujiulize: je, ninaamini kwamba Mungu ni Baba na ananikabidhi zawadi kwa sababu ananiamini? Na je, ninamtumaini Yeye hadi kufikia hatua ya kujiweka kwenye mstari, bila kukata tamaa, hata wakati matokeo si ya hakika wala ya kuchukuliwa kuwa ya kawaida? Je, ninaweza kusema kila siku katika sala, “Bwana, ninakutumaini Wewe!”? Na kisha, je, ninaweza kujihatarisha kwa wema au nijiruhusu nipooze kwa kutokuwa na uhakika? Hatimaye, kama Kanisa: je, tunakuza hali ya kuaminiana na kuheshimiana katika mazingira yetu, ambayo inawafungua watu na kuchochea ubunifu wa upendo kwa kila mtu? Na Bikira Maria atusaidie kushinda hofu - kamwe tusiogope Mungu! Hofu ndiyo, lakini kumuogopa hapana  na kumtumaini Bwana.

Tafakari ya Malaika wa Bwana 19 Novemba 2023
19 November 2023, 12:45