Papa Francisko:Mungu huchagua mtu kumfikia kila mtu,wito si upendeleo ni huduma
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 22 Novemba 2023 akiwa katika Katekesi yake kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, ameendeleza mada ya Shauku ya uinjilishaji: ari ya kitume ya mwamini katika kipingele cha 27 kuhusu Tangazo ni la kila mtu. Akianza Papa amesema kuwa Baada ya kuona, mara ya mwisho, kwamba tangazo la Kikristo ni furaha, hebu leo hii tuzingatie kipengele cha pili kinachohusu tangazo la Kikristo ni kwa kila mtu, na ni furaha kwa kila mtu. Tunapokutana na Bwana Yesu kiukweli, ajabu ya kukutana huku inaenea katika maisha yetu na inadai kuchukulikwa umakini zaidi yetu. Yesu natamani hili, kwamba Injili yake ni ya kila mtu. Hakika, ndani yake kuna “nguvu ya kibinadamu”, utimilifu wa maisha ambao umekusudiwa kwa kila mwanamume na mwanamke, kwa sababu Kristo alizaliwa, akafa, na kufufuka tena kwa ajili ya kila mtu na hakuna mtu aliyetengwa.
Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa katika Waraka wa Evangelii Gaudium yaani Injili ya Furaha, tunasoma kwamba kila mtu ana “haki ya kupokea Injili. Wakristo wanawajibu wa kutangaza Injili bila kumtenga mtu yeyote. Badala ya kuonekana kulazimisha majukumu mapya, wanapaswa kuonekana kama watu wanaotaka kushiriki shangwe yao, wanaoelekeza kwenye upeo wa uzuri na wanaowaalika wengine kwenye karamu ya kupendeza. Si kwa kugeuza imani kana kwamba Kanisa hukua, bali ni ‘kwa mvuto’” (Eg. 14). Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa tujisikie kwamba tuko kwenye huduma ya hatima ya Injili ya ulimwengu wote, na ni ya kila mtu; na lakini tujipambanue kwa uwezo wetu wa kutoka ndani yetu wenyewe. Na ili tangazo liweze kuwa kweli, lazima liache ubinafsi wa mtu na tuwe na uwezo wa kuvuka mipaka yote ya ubinafsi huo.
Wakristo hukutana kwenye eneo lililofungwa mbele ya Kanisa kuu au kanisa, kwa kawaida ambalo limezungukwa na nguzo au ukumbi na kwenda "barabara na vichochoro vya mji" (Lk14:21). Wanapaswa kuwa wazi na kupanua, Wakristo lazima wajieleze na tabia yao hii inatoka kwa Yesu, ambaye hufanya uwepo wake duniani kuwa safari ya kuendelea, yenye lengo la kufikia kila mtu, hata kujifunza kutokana na baadhi ya kukutana kwake. Kwa maana hii, Injili inaripoti kukutana kwa kustaajabisha kwa Yesu na mwanamke mgeni, Mkananayo ambaye alimwomba amponye binti yake mgonjwa (rej. Mt 15:21-28). Yesu alikataa, akisema kwamba alitumwa “kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” tu na kwamba “si vema kuchukua mkate wa watoto na kuwatupia mbwa” (rej Mt 15, 24, 26). Lakini mwanamke, kwa msisitizo wa kawaida rahisi, alijibu kwamba "hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka katika meza ya bwana wao" (rej. Mt 15, 27). Yesu alipigwa butwaa kwa hili na kusema, “Mama, imani yako ni kubwa! Na ifanyike kwako kama unavyotaka” (Mt 15, 28). Kukutana na mwanamke huyu kuna kitu cha kipekee juu yake. Sio tu kwamba mtu alimfanya Yesu abadili mawazo yake, na mwanamke, mgeni na mpagani, lakini Bwana mwenyewe alipata uthibitisho kwamba mahubiri yake hayapaswi kuwa kwa watu ambao yeye ni mali yao tu, lakini yaliyo wazi kwa wote.
Biblia inatuonesha kwamba Mungu anapomwita mtu na kufanya mapatano na baadhi yao, kigezo daima ni hiki: chagua mtu ili kufikia wengine, hiki ndicho kigezo cha Mungu, cha wito wa Mungu. Marafiki wote wa Bwana wanapata uzuri, lakini pia wajibu na mzigo wa "kuchaguliwa" naye. Na kila mtu alihisi kukata tamaa mbele ya udhaifu wake mwenyewe au kupoteza uhakika wake. Lakini pengine jaribu kuu zaidi ni lile la kuzingatia mwito uliopokelewa kama upendeleo. Baba Mtakatifu katika hilo ameonya na kusema kuwa, "Tafadhali, hapana, wito huo si fursa, milele. Hatuwezi kusema kwamba sisi ni tumependelewa ukilinganishwa na wengine, hapana. Bali wito huo ni kwa ajili ya huduma. Na Mungu huchagua mmoja ili kumpenda kila mtu, na kumfikia kila mtu. "
Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa pia hiyo ni kuzuia jaribu la kutambulisha Ukristo na utamaduni, na kabila, na mfumo. Kwa njia hiyo, ingawa, unapoteza asili yake ya kweli ya Kikatoliki, au tuseme kwa kila mtu, kwa ulimwengu wote, ukristo sio kikundi kidogo cha watu wa daraja la kwanza, waliochaguliwa. Na tusisahau: Mungu huchagua baadhi kwa kuwapenda wote. Na upeo huo ni wa ulimwengu wote. Injili si kwa ajili yangu tu, ni kwa ajili ya kila mtu; tusisahau hili. Papa amesisitiza na kuhitimisha akiwashukuru.