Papa Francisko anaonesha maskitiko kufuatia vifo vya watu huko Brazzaville
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko anaombea watu zaidi therathi waliofariki dunia katika umati wa watu katika uwanja wa michezo, wa mji mkuu wa Jamhuri ya Congo Brazzaville yaliyoonesha katika katika telegramu kwa rais wa Baraza la Maaskofu wa Congo Braza iliyotiwa saini na Kardinali Parolin, Katibu wa Vatican. Katika telegramu hiyo kwa Askofu Mkuu Bienvenu Manamika Bafouakouahouh, rais wa Baraza la Maaskofu wa Congo (CEC) na Askofu mkuu wa mji mkuu wa Brazzaville, ameeleza kusikitishwa na taarifa za ajali mbaya iliyotokea Jumatatu usiku tarehe 20 Novemba kwenye Uwanja wa Michezo wa Michel Ornano kutokana na umati kukanyagana kwenye tukio la kusajili kwa wanajeshi.
Maombi kwa roho za marehemu na ukaribu kwa familia
Katika maandishi hayo, Kardinali Parolini, anabainisha kuwa Papa Francisko anawahakikishia wapendwa wa waathirika ukaribu wake wa kiroho na "anamwomba Mwenyezi awape marehemu furaha ya milele na kusaidia familia katika maumivu yao". Baba Mtakatifu pia anatualika kuonesha mshikamano wa kidugu na kiroho kwa watu wanaohusika na kutoa shukrani kwa wale wote waliotoa msaada kwa vijana katika matatizo kufuatia tukio hilo.
Umati ulianza kusongamana kwa kuogopa kukosa nafasi
Siku ya Jumatatu usiku tarehe 20 Novermba takriban watu 37 walikufa na wengine wengi kujeruhiwa huko Jamhuri ya Congo Brazzaville, waliokandamizwa na umati wa watu katika uwanja wa michezo wakati wa hafla ya kusajiliwa katika jeshi. Juma lililopita, vituo kadhaa vilifunguliwa nchini kote ambapo iliwezekana kujiandikisha kwa ajili ya nafasi ya kusajiliwa. Kulingana na shuhuda umati huo ulianza kusongamana kwa sababu watu wengi walianza kuwasukuma wengine waliokuwapo, huku wakihofia wasingeweza kujiandikisha kabla ya usajili kufungwa.
Nafasi za Taasisi ya Jeshi nchini humo ni finyu
Jeshi ni mojawapo ya taasisi chache zinazoajiri watu katika Jamhuri ya Congo Brazaville. Kulikuwa na nafasi 1,500, lakini zaidi ya watu 5,000 walikuwa wametuma maombi yao. Kulikiwa na foleni ndefu zilikuwa zimeundwa kwa juma nzima nje ya uwanja wa Michel Ornano huko Brazzaville, ambapo ajali ilitokea, na katika maeneo mengine nchini. Kulingana na baadhi ya vyanzo, kulikuwa na maelfu ya vijana nje ya uwanja hukp siku ya Jumatatu. Ukosefu wa ajira nchini ni mkubwa sana, na watu wengi hawana mkataba wa kawaida, wamejiajiri na wana kipato cha chini.