Papa Francisko anaiombea Ukraine na Mashariki ya Kati:vita vinaleta mateso tu
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Tusisahau kudumu katika kuwaombea wale wote wanaoteseka na vita sehemu nyingi za dunia. Baba Mtakatifu Francisko kwa mara nyingine tena, katika salamu zake baada ya Katekesi yake tarehe 22 Novemba 2023, alizindua kwa upya wito wake wa amani kwa"watu wapendwa wa Ukraine, na kwamba Ukraine inayoteswa, Israel na Palestina". Papa Francisko baadaye alizungumza juu ya mikutano miwili aliyofanya kabla ya katekesi hiyo pamoja na wajumbe kutoka familia za Israle waliotekwa nyara huko Gaza na mmoja wa Wapalestina huko Gaza wanaoishi chini ya shambulio la mabomu ya kila siku. Papa amesema hawa wanateseka sana na alisikilizaa jinsi wote wawili wanavyoteseka kwamba: vita hufanya hivi, lakini hapa tumepita zaidi ya vita, hii sio vita, huu ni ugaidi.
Tafadhali tuombee sana amani
Tusonge mbele kwa amani, tuombe amani, tuombe sana amani, Papa Francisko ameomba tena, huku akiomba kwamba, Bwana aweke mkono wake hapo, kwamba Bwana atusaidie kutatua shida na sio kusonga mbele na tamaa na kwamba mwishowe wanaua kila mtu." Sala hiyo ni kwa ajili ya watu wote wawili, Wapalestina na Waisraeli "kwa ajili ya amani ifike haraka" amesisitiza.
Mikutano na Waisrael na Wapalestina
Baba Mtakatifu Francisko, kama ilivyothibitishwa katika siku za hivi karibuni na Msemaji wa Ofisi ya Habari ya Vatican Dk. Matteo Bruni, tarehe 22 Novemba 2023 aliwapokea katika mikutano miwili tofauti, "ya hali ya kipekee ya kibinadamu,",wajumbe wawili wa Waisrael na Wapalestina kwa ishara ya "ukaribu wa kiroho kwa sababu ya mateso ya kila mmoja wao."
Hata hivyo haya ni maaneno ya Papa:
Na tusisahau kudumu katika kuwaombea wale wanaoteseka kwa vita katika sehemu nyingi za dunia, hasa kwa ajili ya watu wapendwa wa Ukraine, Ukraine inayoteswa, na Israeli na Palestina. Asubuhi ya leo nilipokea wajumbe wawili, mmoja wa Waisraeli ambao wana jamaa zao mateka huko Gaza na mwingine wa Wapalestina ambao wana jamaa waliofungwa huko Israeli Wanateseka sana na nikasikia jinsi wote wawili wanavyoteseka: vita hufanya hivi, lakini hapa tumepita zaidi ya vita, hii sio vita, huu ni ugaidi. Tafadhali, tusonge mbele kwa amani, tuombe amani, tuombe sana amani. Mungu aweke mkono wake hapo, Mungu atusaidie kutatua matatizo na tusisonge mbele kwa tamaa ambazo hatimaye zinaua kila mtu. Tunawaombea watu wa Palestina, tunawaombea watu wa Israeli, amani ije.
Papa Francisko vile vile aliwasalimia mahujaji wote Wake kwa Waume kutoka nchi zote duniani. Na hatimaye aliwasalimia wazee, wagonjwa, wanandoa wapya na vijana, wa vikundi vingi vya shule.
Siku kuu ya Kristo Mfalme
Baba Mtakatifu amesema Dominika ijayo, katika hitimisho la kipindi cha Kawaida cha Mwaka tutasherehekea ukuu wa Kristo, Mfalme wa ulimwengu. Kwa njia hiyo Papa amewasihi waamini wote kumweka Yesu katikati ya maisha yao, na kutoka kwake watapokea nuru na ujasiri katika kila chaguo la kila siku. Na amewapatia baraka wote.