Papa anawapongeza maaskofu wa Visiwa vya Canari,Hispania
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Kwa kutambua matatizo ya hali mbazo visiwa vya Canari vinapitia kutokana na mgogoro wa wahamiaji, ninapenda kuelekeza baadhi ya maneno ya kuwatia moyo na ya ukaribu. Ndiyo maneno ya Baba Mtakatifu Francisko yanaanza katika barua aliyowatumia Maaskofu wa Visiwa vya Kanari huko Hispania, ambapo Baba Mtakatifu anaelezea shukrani za kwa juhudi zilizofanywa kujibu dharura. Unyeti na ukarimu wenye sifa za wakazi wa Visiwa vya Canari unajionesha hata kwa namna ambayo wanawakaribisha, wanawalinda, wanawahamasisha na kushirikisha kaka na dada ambao wanafika katika fukwe zao kwa utafutaji wa wakati bora ujao, Baba Mtakatifu anaandika katika barua kwa maaskofu wa Baraza la Maaskofu Hispania, iliyochapishwa katika Tovuti rasimi yao.
Kukaribisha wahamiaji ni changamoto
Baba Mtakatifu anasema, Asante kwa ajili ya kufungua milango na moyo yenu kwa wale ambao wameteseka. Mwaliko kwa Maaskofu ni kutokana tamanio mbele ya zoezi hilo la kichungaji la kujenga mitandao ya upendo na kuwa taa ya matumaini ili kukabaliana na changamoto za uhamiaji. Yote hayo ni katika matumaini kwamba yanatia nuru katika njia za ubinadamu mpya tayari wa kuinama, kama Msamaria mwema ili kuponya majeraha kwa yule aliyeanguka. Hatimaye Baba Mtakatifu anawashauri kutafuta katika nyuso za wahamiaji, mtazamo mmoja ambao unatamani wakati ujao wa amani na udugu. Kwa kuhitimisha anabainisha kuwa, Tuombe Mungu kwamba matamanio haya yaweze kutimia.