Papa ametuma ujumbe kwa njia ya video kuomba amani kwa Ulimwengu na Nchi Takatifu
Na Angella Rwezaula,- Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 22 Novemba 2023, ametuma ujumbe wake kwa njia Video kwa ajili ya amani. Katika ujumbe huo Baba Mtakatifu anasema, Sisi sote tinahisi uchungu wa Vita. Mnajua mwisho wa vita vya pili vya dunia vita ambavyo, vilishamiri sehemu mbalimbali duniani. Wakati vita vikiwa mbali, labda hatuhisi nguvu zake. Kuna vile ambavyo viko karibu naso ambavyo vinatufanya tetende: Ukraine na Nchi Takatifu. Ni vizito ambavyo vinatokea Nchi Takatifu. Ni vizito sana. Watu Wapalestina, Watu wa Israeli wana haki ya amani, wana haki ya kuishi kwa amani: watu wawili ndugu.
Baba Mtakatifu Francisko akiendelea ameongeza kusema kuwa Tuombe kwa ajili ya Amani katika Nchi Takatifu. Tuombe kwa sababu migogoro itatuliwe kwa njia ya mazungumzo na majadiliano na si kwa mlima wa vifo kwa pande zote mbili. Tafadhali tusali kwa ajili ya Amani katika Nchi Takatifu. Ujumbe kwa njia yaVideo wa Papa Francisko unahitimishwa.