Tafuta

Papa ameshiriki chakula na Maskini katika fursa ya siku yao

"Sote kwa pamoja,tuombe kwa Bwana atubariki,abariki milo na kubariki wakati huu wa urafiki,sote kwa pamoja,na kusindikizana nasi maishani.".Ndiyo maneno ya Papa Francisko akibariki chakula cha Mchana na Masikini katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican,Dominika 19 Novemba 2023.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameshiriki chakula cha Mchana katika Siku ya Maskini duniani katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, mara baada ya kuongoza ibada ya Misa takatifu, na hata sala ya Malaika wa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Dominika tarehe 19 Novemba 2023.

Kila maskini alipata nafasi kula na Papa
Kila maskini alipata nafasi kula na Papa

Kabla ya kuanza mlo huo,   Baba Mtakatifu amebariki kwamba, Sote kwa pamoja, tuombe kwa Bwana atubariki, abariki mlo na kubariki wakati huu wa urafiki, sote kwa pamoja, na kusindikizana nasi maishani. Bwana atubariki sisi sote, abariki chakula hiki, awabariki watu waliokiandaa; wabariki wale wanaosaidia sana katika maisha yetu, kuweza (kusonga) mbele: kwa jina la Baba, la Mwana, la Roho Mtakatifu.

Selfie zilionekana kwa kila mmoja na Papa Francisko
Selfie zilionekana kwa kila mmoja na Papa Francisko

Baba Mtakatifu mara baada ya chakula mwishoni kabla ya kuondoka amekuwa na ya kusema kwamba, Kabla sijaondoka, ningependa kusema kwaheri kwa ninyi nyote na asante kwa kampuni hii, asante kwa uwepo wenu na asante watu waliofanya kazi kwa hili: kwenu, ambao mmetumikia, asante. Na kwa Hilton Foundation, asante. Na kwa wale wote waliochangia hili: kwa makampuni, kwa watu waliosaidia kwa hali na mali kwa hili. Lakini pia kwa ninyi nyote, wale ambao walitoa roho, nzuri, kwa ajili ya chakula hiki cha mchana. Na sasa muwe na mlo mwema na endeleeni. Kisha kuna vitafunio, sijui (alicheka, walicheka) lakini, endelea mbele. Kabla ya kuondoka, ningependa kuwapa baraka zangu, kwenu, kwa familia zenu, na kwa kila mtu.

Baba Mtakatifu kwa hiyo ametoa baraza zake. Na kisha akasema asante sana kwa kila mtu: asante!

Walisubiri sala ya Malaika wa Bwana iishe ndipo wakakutana naye, wakamsalimu na kukaa naye mezani. Maskini na wenza wao, ambapo walikuwa zaidi ya watu 1200 kwa jumla, ambao walijaa katika Ukumbi wa Paul VI, uliogeuzwa kwa hafla hiyo kuwa mgahawa mkubwa na usio wa kawaida, kwa ajili ya chakula cha mchana cha kawaida na Baba Mtakatifu  Francisko, wakati wa kuadhimisha Siku ya Maskini Duniani.

Furaha ya Maskini kula chakula na Papa
Furaha ya Maskini kula chakula na Papa

Meza za mduara zilizowekwa, zilizopambwa kwa maua meupe na manjano, zilikuwa na msingi wa picha na selfies ambazo hazitasahaulika wakati wa kumkaribishwa, umakini, utunzaji na upendo kwa wale wote ambao kwa mwaka mzima wanaishi mitaani bila jiji kuwajali na amba oleo hii wameshiriki meza moja na Baba Mtakatifu. Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo kwa kutolewa mwaka huu na Hoteli za Hilton, pamoja na menyu iliyotolewa kwa kila mtu, hata wale ambao si wakristo na hivyo basi kuhitajika kufuata kanuni fulani za lishe kwa ajili ya dini yao.

Ukumbi wa Paulo VI uligeuka kuwa Hoteli kubwa
Ukumbi wa Paulo VI uligeuka kuwa Hoteli kubwa

 

19 November 2023, 15:54