Mikutano ya Papa imefutwa kutokana na mafua kidogo
Kwa mujibu wa Msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican Dk.Matteo Bruni amebainisha kuwa mikutano ya Papa iliyokuwa imepangwa Jumamosi 25 Novemba 2023 imefutwa kutokana na Papa kuwa na mafua kidogo.
Na Angella Rwezaura, - Vatican.
Mabadiliko ya hali ya tabianchi ambayo yanaathiri sehemu kubwa ya Italia ikiwa ni pamoja na jiji la Roma lenye joto la katikati ya majira ya baridi, pamoja na ongezeko la maradhi ya msimu, pia yamemuathiri Baba Mtakatifu. Jumamosi asubuhi tarehe 25 Novemba 2023 kama ilivyoarifiwa na Msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Dk. Matteo Bruni alibainisha kuwa, “Mikutano ya Baba Mtakatifu Francisko imehairishwa kwa sababu ya mafua kidogo.”
25 Novemba 2023, 13:43