Tafuta

Papa:kushuru,kubisha hodi na kuomba msamaha ni siri ya kuishi kama wanadamu

Papa Francisko akitafakari kuhusu Injili ya Dominika inayoelezea bwana wa shamba na wakulima,wameweka bayana juu ya ukosefu wa shukrani unavyoibua kiburi,uhalifu na vurugu.Amekazia kuwa siri ya kuishi kama binadamu ipo katika mambo matatu ya asante,kuomba msamaha na kubisha hodi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Dominika ya 27 ya Mwaka A wa kawaida tarehe 8 Oktoba 2023, Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari yake kwa mahujaji na waamini waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Akianza tafakari hiyo amesema, Injili ya leo inatuwakilisha mfano mgumu sana, kwa maelezo ya uchungu (cfr Mt 21,33-43). Mwenye shamba alikuwa amepanda shamba la mizabu na akilitunza vizuri, baadaye alikuwa asafiri na kulikabidhi wakulima. Wakati wa kuvuna ulipkaribia aliwatuma watumwa wake wapokee matunda.  Lakini wakulima wakawakamata na kuwaua, ,mwisho akamtuma mwanae, lakini wale pia wakamwua. Je ni kwa nini? Ni kitu gani kilienda vibaya? Kuna ujumbe wa Yesu katika mfano huu.

Papa wakati wa Angelus 8 Oktoba 2023
Papa wakati wa Angelus 8 Oktoba 2023   (Vatican Media)

Bwana wa shamba alifanya yote vizuri, kwa upendo, kwanza yeye alipata  ugumu, wa kupanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, na  akajenga mnara wa ulinzi. Baadaye akawakabidhi shamba la mizabibu wakulima, kwa kuwapangisha wao wema wake wa thamani na kwa hiyo kuwatendea haki, ili shamba la mizabibu liweze kupaliliwa vizuri na kutoa matunda.  Tarehe zilizotarajiwa za mavuno zilikuwa zinatimia kwa furaha, katika hali ya siku kuu na kwa ushirikishwaji wa haki ya mavuno kwa kutosheleza wote. Kinyume chake katika akili ya wakulima walikuwa na mawazo mabaya yasiyo na shukrani na pupa. Papa amesema tazameni, kwamba daima  mzizi wa migogoro unatokana na aina fulani ya kukosa shukrani, na mawazo ya pupa, ya kutaka kumiliki mambo kwa haraka. Hatuhitaji kumpatia lolote bwana. Mavuno ya kazi yetu ni yetu tu. Hatuna deni na mtu yeyote. Ndiyo yalikuwa maoni yao wakulima hao. Na hii si kweli, inatakiwa kuwa na shukrani kwa kile ambacho walipokea na kama vile walivyotendewa.

Waamini katika sala ya Malaika 8 Oktoba 2023
Waamini katika sala ya Malaika 8 Oktoba 2023   (Vatican Media)

Kinyume chake, kukosa shukrani kunaongeza pupa na kukuza ndani mwao uendelevu wa maana ya kiburi, ambacho kinawapelekea kuona hali halisi kwa namna mbaya, ya kuhisi wanastahili kuliko kuwa wadeni kwa bwana wa shamba ambaye alikuwa amewapatia kazi ya kufanya.  Walipomuona mwanae anafika walipata hata kusema kuwa huyu atakuwa mrithi. Haya na tumwue na tuutwae urithi wake Mt 21, 38. Papa ameongeza kusema na  kutoka kuwa  Wakulima wakageuka  kuwa wauaji. Yote hayo ni mchakato na mchakato huo mara nyingi inatokea katika moyo wa watu, hadi mioyoni mwetu, Papa amesisitiza. Kwa mfano huu, Baba Mtakatifu ameongeza kusema, Yesu anatukumbusha ni kitu gani kinatokea hasa mwanadamu anapojidanganya  kwa kujifanyia mwenyewe na kusahahu kutoa shukrani, anasahau hali halisi msingi wa maisha, ya kwamba wema unakuja kutoka katika neema ya Mungu na  kutoka katika zawadi yake ya bure. Inapotokea kusahau hili, inaishia kuishi hali binafsi na kizingiti binafsi ambacho huwezi kuwa na furaha ya kuhisi kupendwa na kukombolewa, lakini kwa huzuni wa udanganyifu wa kufikiria kuwa huna haja na wala ya upendo na wala  ya wokovu.  

Waamini wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 8 Oktoba
Waamini wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 8 Oktoba   (Vatican Media)

Unaishia kuacha kupenda na kujikuta mfungwa wa pupa binafsi na hitaji la kuwa na kitu zaidi kutoka kwa wengine, na kutaka kuwa juu ya wengine. Kutoka hapo ndiyo yanakuja mambo mengi ya kutridhika na uhalifu, kutokuelewana kwingine na wivu, na kusukumwa na hasira na mtu anaweza kuanguka katika kimbunga cha vurugu. Kwa hiyo, Papa ameongeza kusema ni kweli kwamba kukosa kutoa shukrani, kunazalisha vurugu, kunatuondolea amani na kutufanya tuhisi na kuzungumza kwa sauti ya juu,  bila amani, wakati kitu rahisi cha kutoa shukrani kinaweza kupelekea amani. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu  Francisko ameomba, kujiuliza maswali kadhaa, je mimi ninatambua ya kwamba nimepata zawadi ya maisha na ya imani, na kuwa mimi mwenyewe ni  zawadi? Ninaamini kwamba yote yanaanza na neema ya Bwana? Ninatambua kuwa ninapokea mema pasipo mastahili, kwani nimependwa, na kukombolewa bure? Na hasa, katika jibu la neema ninajua kusema Asante?

Je! ninajua jinsi ya kusema "asante"? Papa kwa kukazia zaidi amesema Maneno matatu ambayo ni siri ya kuishi pamoja kwa wanadamu ni: shukrani, kubisha hodi na kuomba msamaha. Je! ninajua jinsi ya kusema maneno haya matatu? Asante, kubisha hodi  na kuomba samahani?. Je ninajua jinsi ya kutamka maneno haya matatu: Asante, hodi, msamaha? Ni neno dogo, "asante,",ni neno dogo, "hodi," ni neno dogo  kuomba msamaha," linalotarajiwa kila siku kwa Mungu na kwa ndugu zetu. Hebu tujiulize ikiwa neno hili dogo, "asante", "kubisha hodi", "msamaha, samahani" lipo katika maisha yetu. Je! ninajua jinsi ya kushukuru, na kusema "asante"?,  Je! najua jinsi ya kuomba msamaha, nisamhehe? Je ninajua kubisha hodi au "ruhusa"? Kwa hiyo  maneno matatu  ambayo Papa amekazia tena ni  Asante, samahani, kubisha hodi au ruhusa. Maria, ambaye roho yake humtukuza Bwana, atusaidie kutoa shukrani iwe nuru inayochomoza kila siku kutoka moyoni. Papa Francisko amehitimisha.

Tafakari ya Papa wakati wa Angelus 8 Oktoba 2023
08 Oktoba 2023, 14:59