Papa Francisko:Mitindo ya uchumi inayojumuisha walio hatarini zaidi iendelezwe
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Fedha ni sanaa ambayo msingi wake ni uaminifu katika mahusiano ambayo inaweza kujengwa tu kupitia maendeleo ya utamaduni wa kukutana. Ni maneno kutoka Ujumbe wa Papa. Ujumbe huo umekuwa kama mwendelezo wa mada pendwa na mafundisho ya Mapapa katika zama za utandawazi wa masoko, uchumi na fedha unaoelekezwa kwa ajili ya manufaa ya wote na kuheshimu utu na hadhi ya binadamu. Kwa hiyo imekuwa hivyo kila mara kwa Baba Mtakatifu Francisko ambaye amerudia tena katika ujumbe uliotumwa kwa Carlo Messina, Mkurugenzi Mtendaji wa Bank ya Intesa , Italia, katika fursa ya tukio la Mkutano ulioongozwa na kauli mbiu: "Hakuna aliyetengwa. Kukua pamoja katika nchi iliyo sawa zaidi" uliofanyika tarehe 26 Oktoba 2023 na wakati huo huo Sr. Alessandra Smerilli, Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu alikuwa kati ya washiriki na ambaye alisoma ujumbe wa Papa.
Kuimarisha mchakato wa Ujumuishaji wa kiuchumi
Ushauri wa Papa Francisko kama tunavyosoma katika ujumbe huo, ni kuimarisha mchakato wa ujumuishaji wa kiuchumi na kijamii unaolenga umakini maalum kwa wahamiaji dhaifu na, wa kwanza kabisa, na kwa utekelezaji wa kushuka kwa idadi ya watu katika uendelevu wa mipango ambayo lazima wapate wahusika wakuu kama vijana na wazee,na wafanye kama dawa ya kuzuia utamaduni wa kutupa.”
Sababu za sanaa ya mikopo na fedha ni kutokana na imani na matumizi yake
Papa Francisko aidha katika ujumbe huo anakumbuka kwamba sababu za awali na motisha za sanaa ya mikopo na fedha zinatokana na imani na matumizi ya fedha kama maisha ya mfumo wa kiuchumi, ni kwa sababu kila mtu apate uwezekano wa kufanikiwa. Sanaa ambayo, inahitaji imani, mahusiano na ambayo Papa Francisko anatumaini kuwa itajengwa tu kupitia maendeleo ya utamaduni wa kukutana ambapo kila sauti inaweza kusikika na kila mtu anaweza kufanikiwa, kutafuta sehemu za pamoja za kuwasiliana, kujenga madaraja na kufikiria mipango shirikishi ya muda mrefu.”