Papa Francisko:Mashariki ya Kati,mazungumzo hujenga amani,si vita na ugaidi
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi Jumatano tarehe 11 Oktoba 2023, katika eneo ambalo linakabiliwa naa muibuko mkali wa vita, Papa Francisko amesema kuwa anaendelea kufuatilia kwa uchungu na kwa wasiwasi kile kinachotokea Israeli na Palestina na, mbele ya watu wengi kuuawa na wengine kujeruhiwa, ameziombea familia hizo ambazo zimeona siku ya sherehe ikigeuzwa kuwa siku ya kumbukumbu ya maombolezo".
"Ninawaombea wale familia ambao wameona siku ya sikukuu ikibadilishwa kuwa siku ya maombolezo, na ninaomba kwamba mateka waachiliwe mara moja. Ni haki ya wale wanaoshambuliwa kujilinda, lakini nina wasiwasi mkubwa juu ya mzingiro kamili ambao Wapalestina wanaishi huko Gaza, ambapo pia kumekuwa na waathiriwa wengi wasio na hatia. Ugaidi na misimamo mikali haisaidii kufikia suluhsiho la mzozo kati ya Waisraeli na Wapalestina, bali huchochea chuki, ghasia, kulipiza kisasi na kusababisha kila mmoja kuteseka. Mashariki ya Kati haihitaji vita, bali amani, amani iliyojengwa juu ya mazungumzo na ujasiri wa udugu."
Takriban watoto arobaini wauawa kibbutz
Na wakati Papa anakumbuka, katika katekesi yake kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro, watu wanaoishi vitani alitaja hali ya Sudan wakati wa kuelezea juu ya sura ya Mtakatifu Bakhita, kama vile kwa mara nyingine tena alikuwa hajasahau hata Ukraine inayoteswa , habari za kifo na uharibifu zinazoendelea huko Israeli na Palestina.
Hata hivyo Nchini Israel inasema kuwa imegundua takriban watoto 40 waliouawa kati ya takriban watu 200 waliouawa katika eneo la Kfar Aza kibbutz. Taifa hilo la Kiyahudi lina takriban watu 1,200 waliouawa kutokana na uvamizi wa Hamas na linatayarishamashambulizi kamili huko Gaza.
Ulinzi katika mipaka
Wanajeshi elfu 300 waliwekwa kwenye mpaka. Mkutano kati ya Netanyahu na Gantz ulitarajiwa Jumatano 11 Oktoba 2023 ili kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Uharibifu mkubwa umeripotiwa katika makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi wa Kipalestina huko Gaza. Jeshi la Israeli limesema lilifanya mashambulizi 70 ya anga katika eneo la Daraj Tuffah na kushambulia maeneo ya wanamaji wa Hamas katika Ukanda huo.