Tafuta

Israel yashambulia Gaza Israel yashambulia Gaza  (ANSA)

Papa atoa wito wa kuacha silaha huko Israeli,vita ni kushindwa

Ninafuatilia kwa hofu na uchungu kile kinachotokea nchini Israeli,ambako vurugu limelipuka kwa njia mbaya zaidi na kusababisha mamia ya vifo na majeruhi.Ninaelezea ukaribu wangu kwa familia za waathirika na ninawaombea na wale wote ambao wanapitia masaa ya hofu na uchungu.Ni Ombi la Papa mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana.

Na Angella Rwezaul;- Vatican.

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko, kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika trehe 8 Oktoba 2023 ametoa wito wa kusitisha mapigano. Katika mawazo yake amesema: 

Ninafuatilia kwa hofu na uchungu kile kinachotokea nchini Israeli, ambako vurugu zimelipuka kwa njia mbaya zaidi na kusababisha mamia ya vifo na majeruhi. Ninaelezea ukaribu wangu kwa familia za waathirika, ninawaombea na wale wote ambao wanapitia masaa ya hofu na uchungu. Tafadhali hacheni mashambulio na silaha na kuwa na uelewe kwamba ugaidi na vita havileti suluhisho lolote, bali ni kifo na mateso ya watu wengi wasio na hatia. Vita ni kushindwa: kila vita ni kushindwa! Tuombee amani katika Israeli na Palestina! Papa amesema.

Mwezi Oktoba wa kusali Rozari

Baba Mtakatifu akiendelea amsema Katika mwezi huu wa Oktoba, uliowekwa wakfu, sio kwa utume tu, bali pia kwa sala ya Rozari, tusichoke kuomba, kwa maombezi ya Maria, zawadi ya amani katika nchi nyingi za ulimwengu zilizo na vita, ghasia na migogoro; na tunaendelea kukumbuka nchi pendwa ya Ukraine, ambayo inateseka sana kila siku, inateswa sana.

Maombi yaendelee kwa ajili ya Sinodi

Baba Mtakatifu akigeukia upande wa tukio la Kisinodi linaloendelea mjini Vatican amesema:Ninawashukuru wale wanaofuatilia na zaidi ya yote kusindikiza kwa sala Sinodi inayoendelea, ambalo ni tukio la kikanisa la kusikiliza, kushiriki na ushirika wa kidugu katika Roho. Ninawaalika kila mtu kukabidhi kazi hiyo kwa Roho Mtakatifu.

Salamu kwa mahujaji kutoka pande za dunia

Baba Mtakatifu amewasalimu wote kuanzia na Warumi na mahujaji kutoka Italia na sehemu nyingi za dunia, hasa wanafunzi na walimu wa Kituo cha  Mafunzo cha  Stimmatini huko Verona, na Wajesuit kutoka nchi mbalimbali zinazoendeshwa na Chuo cha Mtakatifu Roberto Bellarmino kilichopo Roma. Akitazama bendera papa amesema Pole Nyingi: Ninaona bendera nyingi za Kipoland hapa. Salamu kwenu nyote na kwa watoto wa Parokia ya Moyo safi wa Maria.

Papa ameomba kusali Rozari kwa ajili ya amani ulimwenguni
Papa ameomba kusali Rozari kwa ajili ya amani ulimwenguni

Amehitimisha akiwatakia Dominika njema , na wasisahau kusali kwa ajili yake. Mlo mwema, mchana mwema na kwaheri ya kuonana.

Wito wa kuacha vita nchini Israeli
08 October 2023, 15:07