Tafuta

Papa Francisko wakati wa kukutana na vijana wa Harakati ya Kimataifa Scholas Occurrentes. Papa Francisko wakati wa kukutana na vijana wa Harakati ya Kimataifa Scholas Occurrentes.  (ANSA)

Scholas,Papa atuma ujumbe kwa Mkutano VI wa Vijana:harakati,bure na kukutana

Papa ametuma ujumbe kwa njia ya Video katika Mkutano wa VI wa Vijana Ulimwenguni ulioandaliwa na Scholas Occurrentes na World ORT kuhusu mada ya elimu kama chombo kwa ajili ya mazungumzo ya kidini na utamaduni wa amani.Mkutano ulifanyika huko Mtakatifu Paulo,Brazil kuanzia 23-26 Oktoba Ujumbe ulioneshwa Alhamis 26 Oktoba.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika fursa ya Mkutano wa VI wa Vijana Ulimwenguni  ulioandaliwa na Harakati ya Kipapa  Kimataifa ya  Scholas Occurrentes kwa ushirikiano na World ORT  huko Mtakatifu  Paulo  nchini Brazil kuanzia tarehe 23-26 Oktoba 2023, Baba Mtakatifu Francisko aliwatumia Ujumbe kwa njia ya Video ambao ulionesha siku ya Mwisho wa Mkutano huo tarehe 26 Oktoba 2023. Katika ujumbe wake kwa lugha ya kihispania alisema: “Ningependa kushukuru mamlaka ya ORT kwa kazi wanayofanya. Kazi ya kutafakari na pia ya ushuhuda, yenye maneno matatu muhimu: harakati, bure na kukutana. Ili kuwa mtu wa kweli na sio wa kibiashara, mkutano lazima uwe huru. Na ili kuwe na mkutano, lazima kuwe na harakati. Hiyo ni, kama mnavyoona, maneno haya matatu yanaoyesha kitu cha kibinadamu sana. Kwa namna hiyo Papa Fancisko ameongeza kusema: " Ninashukuru mamlaka ya shule za ORT wanaofanya kazi na Scholas, ni uvumbuzi ambao bado haujaonesha uwezo wake kamili, hata kama umekuwepo kwa muda mrefu. Ni jambo la baadaye sana, na kubwa sana. Na pia ninashukuru mamlaka ya Brazil ambayo iliruhusu na kuunga mkono aina hii ya mpango. Asante na Mungu awabariki.”

Mfuko wa Kipapa Kimataifa wa Scholas Occurrentes

Kuhusiana na harakati hii ya kimataifa, Baba Mtakatifu  Francisko alitoa idhini ya kisheria kwa kuanzisha Mfuko wa Kimataifa wa Scholas Occurentes. Katika barua yake aliandika kuwa: “Kwa kuzingatia kwamba Occurrentes'  leo  hii inaendelea kupanua utendaji wake kwa manufaa na umeundwa kama jumuiya za kijumuiya na harakati za elimu zenye tabia ya kimataifa, inahitaji mfumo mpya wa kisheria kulingana na ukweli huu mpya.” Kwa  njia hiyo Papa Francisko aliliridhia uwe Mfuko wa Kipapa wa  kimataifa  kwa  barua ya mkono wake  iliyotiwa saini mnamo  tarehe 19 Machi 2022. Msingi Mkuu wa  Scholas Occurrentes unapatikana katika mipango ya kielimu iliyoundwa kwa ajili ya watoto katika maeneo maskini katika jiji la Buenos Aires, Nchini Argentina kwa mpango wa  aliyekuwa Askofu Mkuu wa wakati huo, Kadinali Jorge Mario Bergoglio (Papa Francisko). Tangu kuanzishwa kwa chombo hiki, umekua na kuwa mtandao wa kimataifa wa shule zinazoshiriki mali zao, kwa malengo ya kawaida na uangalizi maalum kwa wale wanaohitaji zaidi. Dhamira yake kwa hiyo ni kujibu wito wa kujenga utamaduni wa kukutana na kuwaleta  pamoja vijana wa sehemu zote.

Vijana wa Scholas Occurrentes walikutana na Papa 25 /05/2023
Vijana wa Scholas Occurrentes walikutana na Papa 25 /05/2023

Kwa hiyo katika Barua ya Mkono wake, aliyotia saini, Papa Francisko alibainisha kuwa “kupata hadhi ya  halali  chini ya sheria ya kiraia, nchini Hispania, kama Mfuko usiona faida ambao ulienea kwa kasi katika zaidi ya nchi sabini, katika mabara matano, kwa mujibu wa sheria ya kisheria, na ilitambuliwa kama uhuru Mfuko wa Kipapa  wa  sheria ya kipapa. “Nikirejeea ombi lililokomazwa na Waanzilishi wake, ninatoa idhini yangu kwa Mfuko wa   Kipapa wa Scholas Occurrentes kuwa Muungano wa Kibinafsi wa Waamini wenye tabia za kimataifa... ulioanzishwa kama mfuko  binafsi ndani ya utaratibu wa kisheria,” kwa mujibu wa maandishi ya  Papa Francisko. Aidha katika barua hiyo alibainisha kwamba Sheria hizi zianze mara moja kutumika kuanzia tarehe 19 Machi 2022, na kuanzia tarehe hiyo, haki na wajibu wote wa Mfuko wa Kipapa wa Scholas Occurrentes unapatana na haki na wajibu wa chama cha namna hiyo.

Kuhusu World ORT  

Wakati huo huo kuhusu World ORT  ni shirikisho la mashirika ya kitaifa ya ORT yanayojiendesha. Mnamo mwaka 2005 bajeti ya kimataifa ya ORT ilizidi dola za Marekani milioni 250 kila mwaka. Kufikia 2016, bajeti yake ya kila mwaka ilikuwa dola za kimarekani 62.7 milioni. Shughuli za sasa za ORT ziko Israel, iliyokuwa Umoja wa Kisovieti (pamoja na Mataifa ya Baltic), Ulaya, Amerika Kusini, na Afrika Kusini. ORT pia inaendesha programu za Ushirikiano wa Kimataifa na kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi na kijamii yasiyo ya madhehebu katika sehemu ambazo hazijaendelea duniani, kwa mafunzo ya ufundi stadi na utoaji wa usaidizi wa kiufundi. Mnamo 2003 Israel ilikuwa eneo la operesheni kubwa zaidi ya ORT, ikiwa na wanafunzi 90,000 waliosoma au kufunzwa katika shule, vyuo na taasisi 159 za ORT, wakielimisha 25% ya wafanyakazi wa hali ya juu wa Israel. Hata hivyo, mwaka wa 2006 ORT Israel ilijiondoa kwenye ORT ya Dunia.ORT ya Ulimwengu inaendelea kufanya kazi nchini Israel chini ya jina la Kadima Mada-Educating for Life, ikifanya kazi na Wizara ya Elimu ya Israel, wizara zingine za Israel, mabaraza ya mikoa na hospitali zinazotoa rasilimali zilizoongezeka na vifaa vilivyoboreshwa na vifaa vya shule. World ORT huchangisha fedha kupitia mashirika yake ya uanachama katika nchi mbalimbali na kupitia Mashirikisho ya Kiyahudi ya Amerika Kaskazini(JFNA). ORT ya Dunia imeundwa kisheria nchini Uswiss, lakini inafanya kazi kutoka ofisi za London, nchini Uingereza. Ina hadhi ya kushauriana kwa madhumuni ya habari na elimu na UNESCO, na hadhi ya mwakilisho wa kudumu katika Shirika la Kazi la Kimataifa. Na zaidi ya hayo ORT ni mwanachama mwanzilishi wa Baraza la Kimataifa la Mashirika ya Hiari (ICVA).

Vijana wa Scholas Occurentes Harakati ya Kimataifa yenye hadhi ya Kisheria Ya Kipapa
Schola Occurrentes
27 October 2023, 10:14