Kimbunga Otis imeacha madhara makubwa katika Pwani za Pasifiki ya Mexico. Kimbunga Otis imeacha madhara makubwa katika Pwani za Pasifiki ya Mexico.  (ANSA)

Masikitiko ya Papa kwa waathirika na uharibifu uliosababishwa na kimbunga huko Acapulco

Katika Telegramu kutoka kwa Papa Francisko,iliyotiwa saini na Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican anatuma salamu za rambirambi kwa familia za marehemu na majeruhi kutokana na mkasa ulioikumba pwani ya kusini mwa Mexico katika siku za hivi karibuni.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko anasema kuhuzunishwa sana na kimbunga kilichopiga siku za hivi karibuni karibu na Acapulco, katika jimbo la Guerrero, pwani ya kusini mwa Mexico, na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali nyingi. Katika barua iliyotiwa saini na Katibu wa Vatican,  Kardinali Pietro Parolin, iliyoelekezwa kwa Askofu Mkuu Leopoldo González González wa Jimbo kuu la Acapulco, Papa Francisko "anatoa sala za dhati kwa ajili ya mapumziko ya milele ya marehemu, huku akimwomba B Pole kwa familia za marehemu. Maombi kutoka kwa Papa pia ya kuongeza hisia za upendo mkuu  katika jumuiya ya Kikristo ili kushirikiana katika ujenzi wa maeneo yaliyoathirika. Tena katika telegramu, Papa Francisko anatuma “rambirambi zake za dhati kwa jamaa na marefiki wa marehemu, pamoja na wasiwasi wake wa kibaba na ukaribu wa kiroho kwa waliojeruhiwa na waathitika  watu wapendwa wa Acapulco".

Majeruhi na uharibifu mkubwa

Kimbunga Otis, kilichoainishwa kama kitengo cha 5 (kiwango cha juu zaidi kwenye mizani ya Saffir-Simpson) kilifika kwenye pwani ya Mexico inayokabili Pasifiki kati ya Jumatano  tarehe 25 na Alhamisi 26 Oktoba 2023. Ni mojawapo ya vimbunga vikali kuwahi kufika kwenye pwani ya Mexico. Kwa sasa kuna karibu waathirika thelathini, kadhaa wamepotea na katika jiji la Pwani ya bahari huko Acapulco, kituo kikubwa zaidi katika eneo hilo, majengo na miundombinu imeharibiwa vibaya, na kwa hiyo:“Bwana awape faraja kwa wale wanaoteseka na madhara ya kimbunga."Papa amebainisha.

27 October 2023, 17:29