Tafuta

2023.09.18 Papa Francisko azungumza katika Mazungumzo ya Mpango wa  Kimataifa w CLINTON, huko New York, Marekani. 2023.09.18 Papa Francisko azungumza katika Mazungumzo ya Mpango wa Kimataifa w CLINTON, huko New York, Marekani. 

Papa:Matatizo yanaweza kuleta ubora au ubaya ndani mwetu

Papa alizungumza kwa njia ya mtandao katika Mpango wa Kimataifa wa Clinton,New York marekani Septemba 18.Katika hotuba lilihusu changamoto za dharura za wakati wetu.Alihimiza jukumu la kila mtu la kupambana na vita vya ubinafsi.Ni wakati wa mazungumzo na diplomasia.Utume wa Hospitali ya Watoto,Bambino Gesù ni ishara ya ushirikiano wa sayansi na ukarimu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko aliingilia kati kwa kusema hapana kufanya vita na kutoa wito wa kujitolea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kabla ya kuchelewa. Alisema hayo katika hotuba yake tarehe 18 Septemba 2023 kama sehemu ya Mpango wa Kimataifa wa Clinton ambao uliandaliwa kwa siku mbili 18-19 Septemba  2023 Jijini  New York,  Marekani ili kutambua na kubadilishana njia za kutekeleza uongofu wa kweli  wa maisha ya maendeleo pamoja, licha ya masuala muhimu yanayoathiri mataifa, katika hatua ndogo. Kabla ya hotuba ya Baba Mtakatifu, ilitangulia kuoneshwa video na Picha za Papa wakati wa safari zake za kimataifa na katika nyakati muhimu hasa katika kuwasiliana na watoto wadogo na wagonjwa na  hotuba ya Baba Mtakatifu iliyotolewa kwa lugha ya Kihispania.

Mpango wa Kimataifa wa Clinton 18-19 Septemba 2023
Mpango wa Kimataifa wa Clinton 18-19 Septemba 2023

Baba Mtakatifu wa kutazama changamoto nyingi za leo  hii zilizoorodheshwa na Rais wa zamani wa Marekani  Bwana Bill Clinton, kuanzia  mabadiliko ya Tabianchi hadi majanga ya kibinadamu yanayoathiri wahamiaji na wakimbizi,na hata utunzaji wa watoto, Papa alisisitiza kuwa ni kwa pamoja tu tunaweza kuponya ulimwengu kutokana na kutokujulikana ambayo ni utandawazi wa kutojali.  Papa alieleza  kile anachofafanua tena kama vita vya tatu vya dunia ambavyo vinatilia shaka dhana kuu na ya kawaida ya uwajibikaji. Kwa upande wake alisema hakuna changamoto kubwa sana ikiwa tutakabiliana nayo kuanzia uongofu binafsi wa kila mmoja wetu, kutoka katika mchango wa kibinafsi ambao kila mmoja wetu anaweza kuutoa ili kuushinda na kutoka katika ufahamu wa kile kinachotufanya kuwa sehemu ya hatima sawa. Aidha alisema kwamba hakuna changamoto inayoweza kukabiliwa kwa mtu  peke yake binafsi. Kwa sababi ni kwa  pamoja tu. Papa aliwahimiza wote kaka na dada watoto wa Mungu kuwa: “Kwa sababu hii mimi huwatia moyo kila mara wanawake na wanaume wote wenye mapenzi mema, na ningependa kufanya hivyo hapa pia, kutokata tamaa mbele ya magumu.” Papa alihimiza.

Bi Clinton akizungumza katika Mpango wa Kimataifa wa Clinton
Bi Clinton akizungumza katika Mpango wa Kimataifa wa Clinton

Baba Mtakatifu akiendelea alisema “matatizo yanaweza kuleta yaliyo bora au mabaya ndani yetu. Hapa ndipo penye changamoto. Kupambana na ubinafsi, kujikunja,  mgawanyiko ili kukarimu. Ni wakati wa kupata mabadiliko ya amani, mabadiliko ya udugu. Ni wakati wa kuacha silaha. Ni wakati wa kurudi kwenye mazungumzo na diplomasia. Ni wakati wa mipango ya ushindi dhidi ya  uchokozi wa kijeshi na  ukome. Ndiyo maana ninarudia kusema: hapana vita. Hapana kwa vita.” Papa alisema. Papa aligeukia mada nyingine ya janga la Ikolojia ambayo ni mpango wa Marekani kwa Bill Clinton, mwanzilishi wa Jukwaa hilo (CGI),  ambao unatilia mkazo mkubwa. “Ni wakati wa kufanya kazi pamoja ili kukomesha, kabla ya kuchelewa sana” Hili Papa alilirudia mara kadhaa huku akikumbuka Waraka wake wa  Laudato Si', na kusihi: “Wacha tusimame wakati bado tuna wakati, tafadhali”. Na alielezea wasiwasi wake wote, tena mwishoni mwa hotuba yake, wakati Clinton alipomkaribisha kutoa maoni juu ya mchango wake na wito wa mwisho kwa wanadamu wote kwamba: “hebu tuchukue hatua kabla ya kuchelewa.”

Viongozi wakuu wa nchi, wanasayansi hata waandishi wa habari wapo katika Mpango huo wa Kimataifa wa Clinton
Viongozi wakuu wa nchi, wanasayansi hata waandishi wa habari wapo katika Mpango huo wa Kimataifa wa Clinton

Dharura za uhamiaji, ambazo zipo karibu sana  moyoni mwa Papa, ni suala lingine lilizungumzwa. Kwa hiyo alikumbuka kuwa : “Hatuzungumzii juu ya idadi, lakini juu ya watu, wanaume, wanawake na watoto. Tunapozungumza kuhusu uhamiaji, tunafikiria macho ya watoto tunaokutana nao katika kambi za wakimbizi. Ni wakati wa kufikiria juu ya vijana, watoto, elimu yao na  utunzaji wao.” Papa Francisko alitaja utume na mipango ya Hospitali ya kipapa  ya Watoto, Bambino Gesu, ambayo katika miezi hii ya vita imetibu wagonjwa wadogo zaidi ya elfu mbili wa Kiukraine walioikimbia nchi yao pamoja na wazazi na jamaa zao. Papa alipendekeza kuwa afya ipatikane kwa wote kwa sababu hakuna watoto ambao wabaki bila kutibika. Na alisisitiza kipengele maalum ambacho kinatofautisha kazi ya muundo huo unaojulikana ulimwenguni kote kwamba: “Unakusudiwa kuwa ishara. Ushuhuda wa jinsi inavyowezekana (kati ya juhudi nyingi) kuchanganya utafiti mkubwa wa kisayansi, unaolenga kutunza watoto, na ukarimu wa bure kwa wale wanaohitaji. Sayansi na ukarimu: vitu hivi viwili mara chache hukutana katika kiwango fulani.

Mkutano huo wa Kimataifa wa Mpango wa Clinton unahudhuriwa na watu mashuhuri kimataifa, kuanzia kwa wanasayansi hadi waandishi wa habari, kwa wakuu wa taasisi za kisiasa na kimataifa hadi wanaharakati, wajasiriamali na wafadhili. Kila mtu analeta ushuhuda na mazoea mazuri ya kuongeza ufahamu kuhusu mada ya jumla inayotokana na “Jinsi ya kusonga mbele, licha ya matatizo yanayotokea, kujenga maisha ya baadaye yenye nguvu kwa wote?” Rais Mstaafu wa Marekani Clinton alikumbusha kwamba kila siku tunaitwa kufanya maamuzi madogo na rahisi. Mpango wake ulikuwa na wito kwa wajibu wa kila mtu kujaribu kuleta mabadiliko: Mpango huo ulioanzishwa mwaka 2005, ambao umekuwa na matokeo kwa maisha ya zaidi ya watu milioni 435 katika zaidi ya nchi 180. “Tunaweza kuboresha kila siku alisema. Kujumuishwa ni bora kuliko mgawanyiko. Kwa hiyo  kikao cha asubuhi tarehe 18 Septemba  (saa 3.15 nchini Marekani, wakati Ulaya ni jioni) ambacho kilimshirikisha Papa Francisko, kilikuwa sehemu ya jopo la mada kuanzia kilimo endelevu hadi huduma ya afya sawa, kuanzia mtna kutoka mada ya unyanyasaji wa kijinsia hadi  kufikia uhifadhi wa bahari.

Papa na Mpango wa Kimataifa wa Clinton 18-19 Septemba 2023
19 September 2023, 10:04