Tafuta

2023.09.18 Papa Francisko amekutana washiriki wa Mkutano wa mashirika mawili:Wa  Moyo wa Yesu na Binti wa Bidii ya Kimungu. (Waroganisti). 2023.09.18 Papa Francisko amekutana washiriki wa Mkutano wa mashirika mawili:Wa Moyo wa Yesu na Binti wa Bidii ya Kimungu. (Waroganisti).  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa Wanaroganisti:Wawe wataalam wa Mungu katika sala na upendo

Katika hotuba Papa kwa watawa wa kike na kiume wa Mashirikia ya Moyo wa Yesu na Binti wa Bidii ya Kimungu,alisisitiza umuhimu wa mazungumzo na Mungu,ambayo lazima yawe ya kudumu na ya kila siku kwa kuinua mikono kuelekea mbinguni na kunyooshwa kuelekea ndugu kama walivyofundishwa na mwanzilishi Mtakatifu Hannibal Maria wa Ufaransa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko akikutana na washiriki wa Mkutano ulioandaliwa na  Shirika la Waroganisti wa Moyo wa Yesu na Shirika la Mabinti wa Bidii za Kimungu mjini Vatican Jumatatu tarehe 18 Septemba 2023, amewaeleza furaha yake ya kukutana nao wakati wanafanya tafakari na kufanya kazi kuhusu njia za kufuata za Kishirika kwa nuru ya Mikutano Mikuu miwili.  Kwa hiyo   katika hotuba yake ameanza kusema wao wamepata fursa ya kuzungumzia mada kama vile kuwekwa wakfu, utambulisho wa karama, ushirika wa kidugu na utume, ambayo ni mambo ya kimsingi ya maisha ya kitawa,  na ambayo uchunguzi wake unahitaji uwezo wa kusikiliza, uwezo wa kupambanua, katika sala na kushiriki, na pia unahitaji dozi nzuri ya ujasiri, kuendelea kuwa waaminifu leo  hii kwa maongozi ya awali ya Mtakatifu Hannibal Maria wa Ufaransa na wakati huo huo makini na mahitaji ya ulimwengu unaobadilika. Kungekuwa na mambo mengi ya kusema juu ya masuala haya, lakini leo hii, Papa amependa kutafakari nao juu ya jambo moja tu, ambalo liko kwenye mzizi wa utume wao maalum katika Kanisa na ambalo pia linajumuisha nadhiri yao ya  nne ya Rogate, yaani  sala, kwa  ajili ya miito.

Papa amekutana na waroganisti
Papa amekutana na waroganisti

Sala ni uzi mwekundu unaopitia maisha ya Mtakatifu Hannibali. Wito wake mwenyewe ghafla, ulijikita hakika sana, kama alivyoshuhudia,  kunaonekana wazi kwake wakati anajikuta katika kuabudu mbele ya Sakramenti Takatifu. Huko aliangaziwa na akili ya Rogate yaani ya kusali. Kiukweli, wakati mtu anajiweka mwenyewe, kuwa mnyenyekevu na mpole, mbele ya Mungu, mara nyingi mtu hupokea ufahamu maalum wa maana ya maisha ya mtu: ni katika sala ya uaminifu na ya kudumu, hasa katika Kuabudu, kwamba kila kitu huja katika maelewano, kwamba mtu huona mambo kwa uwazi zaidi, malengo, kutafuta Bwana nguvu na mwanga wa kuyatekeleza kulingana na mipango  ya ishara zake.

Mtakatifu alisema: “Bila moto huu wa ndani, unaoitwa maisha ya kiroho, sala, kuabudu ma kitubio [...] hakuna kazi nzuri kabisa inayoweza kuzaa matunda...(Mtakatifu Hanibal Maria wa Ufaransa). Hii ilikuwa uzoefu wake, lakini inatumika kwa kila mtu; bila maombi huwezi kusimama na hujui wapi pa kwenda. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba kuwe na  mazungumzo ya muda mrefu na Bwana kila siku, na kisha maombi kwake kabla ya kila wakati muhimu, kila mkutano, na kila uamuzi. Mtakatifu Hannibali aliongozwa na kifungu fulani cha Injili, ambamo Yesu anasema: “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache! Basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake (Mt 9,37-38). Hatua hii ilijaza moyo wake kwa bidii. Huko Messina ya wakati wake, kuanzia umaskini wa kitongoji cha nyumba za Avignone, na kisha kwenda mbele zaidi, kwa mtazamo mpana na hatua pana zaidi, yeye pia alihisi, kama Yesu, mwenye huruma sana kwa wanadamu maskini wa mwili na roho.

Papa amekutana na wanashiriki  Waroganisti
Papa amekutana na wanashiriki Waroganisti

Na alielewa kwamba jambo la kwanza la kufanya ni kusali kwa hakika si kumshawishi Mungu kutuma wachungaji, kana kwamba hakuwajali watu wake, bali ajiruhusu zaidi kuzidiwa na uwazi wa upendo wake wa baba na mama, wa kujifunza, wa kusali,  na kuwa makini na mahitaji ya watoto wake! Hivyo kutokana na sala, roho ya shughuli zote za kitume na za upendo za Mwanzilishi, Shirika lao lilizaliwa, kwanza Mabinti wa Ari ya Kimungu na kisha Waombajiwa Moyo wa Yesu. Walizaliwa kutoka katika mikono iliyounganishwa  na kunuliwa ya Mtakatifu, ambaye aliwaweka wakfu kwa Kristo kwa maombi yake. Baba Mtakatifu Francisko akiendelea ameeleza kuwa Mtakatifu Paulo VI siku moja alitoa mwaliko kwao uliosema: “Waongofu wa Moyo wa Yesu, ambao jina lao linawastahilisha katika utume na kwa sura ya waabudu na waombaji kwa ajili ya utume wa juu na mzuri zaidi, kustahili na kujiandalia wito kwa Ufalme wa Kristo […]. Kuweni wataalamu wa Mungu, (Hotuba ya kwa Wakarmeli wa Maadhimisho ya kale, ya kumbukumbu za Augustiniano na wa Warogationisti wa Moyo wa Yesu, 14 Septemba 1968). 

Papa Francisko kwa hiyo amependa kupyaisha mwaliko wake kuwa: muwe wataalamu wa Mungu, sio hata wasomi wa mbinu, takwimu na nadharia, ingawa hizi zinaweza pia kuwa na manufaa, lakini hekima inayopatikana kwa kupata kwanza wito kwa kupiga  magoti na kisha kwa  kuinua mikono.” Kwa hiyo amewaomba wawe wataalamu katika sanaa ya sala na mapendo: mikono iliyoinuliwa mbele ya Mungu na mikono iliyonyooshwa kwa ajili ya ndugu. Na hivi ndivyo wanavyokuwa wataalamu wa Mungu, Papa amesisitiza. Huu ni utume wao. Hata leo hii kwa hakika Bwana anaita na vijana wengi wanahitaji mashuhuda wa kuaminika na viongozi ambao, kwa kuwaonesha uzuri wa maisha yaliyotumiwa kwa ajili ya upendo, huwasaidia kuitikia “ Tazama mimi hapa.” Kwa kuhitimisha Papa Fancisko amewashukuru kwa kile wanachofanya na kwa ajili ya ushuhuda wao. Amewashukuru kuinua mikono kusali na kuwaomba wasiishushe kwa sababu baadaye wanapaswa kwenda kufanya kazi, lakini mikono ikiwa imeinuliwa. Waendelee hivyo na kusali kwa ajili ya miito. Amewahasisha wasisahau pia kusali kwa ajili yake.

Papa na waroganisti
18 September 2023, 16:12