Papa kwa Makleri:Pandeni amani kwa jicho la huruma kwa wote
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 22 Septemba 2023 akiwa katika ziara yake ya 44 ya kitume kusini mwa Ufaransa, amefanya ishara ya kuweka chini ya vazi la Maria matunda ya Mikutano ya Mediterania, iliyofanyika kwa siku ya ziara fupi huko Marsiglia. Wakati wa maombi na mapadre, mashemasi wa kudumu pamoja na wake zao, waseminari, wakuu wamashirikia na jumuiya za kitawa zilizopo katika jimbo kuu, ambayo yalianza mara baada ya kukaribishwa rasmi katika uwanja wa ndege wa Marsiglia, lakini pia waliunganishwa na wasimamizi wa mahali patakatifu pa madhabahu za Bikira Maria za Mediterania.
Papa aliingia ndani ya Kanisa hilo akiwa katika kiti cha magurudumu, huku akiwabariki wale waliohudhuria katika madhabahu hiyo kwa maji ya baraka ishara ya ubatizo na baadaye alifika katikati ya altare na sanamu ya Mama Yetu Mlinzi wa madhabahu. Watawa wawili walishikilia mshumaa mkubwa, zawadi kutoka kwa Papa kwa Maria. Baada ya kuwasha mshumaa, Papa Francisko alisimama kwa muda wa maombi ya kimya mbele ya sanamu. Kisha Askofu Mkuu Jean-Marc Aveline alimkaribisha Baba Mtakatifu.
Baadaye ilifuatiwa usomaji wa kifungu kilichochukuliwa kutoka katika Kitabu cha Sefania. Baba Mtakatifu Fransisko alitoa neno ambapo alikumbusha wakuu wale ambao kwa wakati walikwenda kama mahujaji kwenye kanisa hilo na kuthibitisha kwamba ushauri wa kutumaini na kufurahi, uliokuwamo kwenye somo la kibiblia liliosomwa unarejea historia ya jengo takatifu, ambalo halijajengwa kumbuka muujiza au tokeo la Maria, lakini kwa sababu tangu karne ya 13 waamini walitafuta na kupata katika kilima kile uwepo wa Bwana kupitia macho ya Mama yake Mtakatifu.
Mwishoni mwa maneno ya Papa Francisko, waliokuwa ndani, walisali kwa pamoja sala kwa Bikira Maria, inayoheshimiwa katika mahali patakatifu isemayo: “Bikira Maria, ninakugeukia wewe katika sala, kwako, ambaye hapa ninamwita Mama yetu Mlinzi. Unamleta Mwanao. Ananiambia: Bikira Maria, ninakugeukia kwa maombi, Kwako, ambaye hapa ninakuita Mama yetu wa Mlinzi. Wewe unitambulishe kwa Mwanao. Unianiambie: "Huyu hapa mama yako."Mimi niko na ninataka kubaki mwanao. Ulinda afya ya roho yangu na mwili wangu pamoja na wale wote ninaowapenda. Utusaidie kujitolea kwa imani ya ubatizo wetu na kuheshimu yote ambayo Mwanao anatuomba. Utujalie kupenda kila mtu karibu nasi. Mapenzi yetu yalete wema, ufahamu na unyenyekevu. Tusaidie kuwatumikia ndugu zetu vizuri na bora. Tuunge mkono katika majaribio. Walinde wale wote wanaoteseka katika mwili na roho. Ee Bikira Mlinzi, ee Mama yangu wa mbinguni, ninakuelekea kwa moyo wa mtoto. Utuombee kwa Mwanao Yesu. Tupate neema ya kumpenda zaidi na zaidi na kufanana naye kila siku.
Kwa upande wa Kardinali Jean-Marc Aveline akimkaribisha Baba Mtakatifu katika Madhabahu hiyo na kutoa neno kwa niaba ya wote waliokuwa hapo alikuwa amemkaribisha kwa shangwe akisema kuwa watu wote wa Marsiglia, wa madhehebu ya dini wanakwenda hapo kujikabidhi Bikira Maria.
Akiendelea alisema: “Pamoja nawe, Baba Mtakatifu, pamoja na mahujaji wote waliopanda kilima hiki kwa zaidi ya miaka mia nane kuomba na kushukuru, tunamkabidhi Bikira Maria wakazi wote wa pwani ya Mediterania na wale wote, mabaharia au wahamiaji, wanaokabiliana nao hatari za bahari.” Na Kardinali huyo pia alikuwa amemwakikishia Baba Mtakatifu kusali kwa ajili yake.
Ifuatayo ni hotuba kamili ya kwanza ya Papa Francisko: “Ninayo furaha kuanza ziara yangu kwa kushiriki wakati huu wa maombi nanyi. Ninamshukuru Kadinali Jean-Marc Aveline kwa maneno yake ya ukaribisho na ninamsalimu Askofu Mkuu Eric de Moulins-Beaufort, ndugu zangu Maaskofu, Gombera na ninyi nyote, mapadre, mashemasi, waseminari, na wanaume na wanawake waliowekwa wakfu wanaofanya kazi katika Jimbo kuu hili kwa ukarimu na kujitolea kujenga jamii ya kukutana na Mungu na jirani. Asante kwa uwepo wenu, huduma yenu na maombi yenu! Katika kuja Marseille(Marsiglia), nimejikuta katika kundi la mahujaji wakuu: Watakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, Charles de Foucauld, na Yohane Paulo II, na wengine wengi sana waliokuja hapa kujikabidhi kwa “Notre Dame de la Garde” yaani Mama Yetu wa Ulinzi. Tunaweka chini ya vazi lake matunda ya Rencontres Méditerranéennes, Mkutano pamoja na matarajio na matumaini ya mioyo yenu.
Katika usomaji wa Biblia, nabii Sefania alituhimiza tuwe na furaha na ujasiri, akitukumbusha kwamba Bwana Mungu wetu hayuko mbali, yuko hapa, karibu nasi, ili atuokoe (rej. Ze 3:17). Kwa namna fulani, ujumbe huu unatukumbusha historia ya Kanisa Kuu hili na inawakilisha nini? Kiukweli, haikuanzishwa kwa kumbukumbu ya muujiza au tokeo fulani, lakini kwa sababu tu, tangu karne ya kumi na tatu, Watu watakatifu wa Mungu wamekuwa wakitafuta na kupata hapa, kwenye kilima cha La Garde, uwepo wa Bwana kupitia macho ya Mama yake Mtakatifu. Ndiyo maana, kwa karne nyingi, watu wa Marsiglia hasa wale wanaosafiri kwenye mawimbi ya Mediteranea, wamekuwa wakija hapa kuomba. Bado leo hii, (Bonne Mère)yaani Mama Mwema anawaletea watu wote makutano ya macho ya thamani sana: ya kwanza ni ya Yesu, ambaye Maria daima anaelekeza mawazo yetu na ambaye upendo wake unaonekana machoni pake; nyingine ni ile ya wanaume na wanawake wasiohesabika wa umri na hali zote. Anawakusanya wote pamoja na kuwaleta kwa Mungu, kama tulivyokumbuka mwanzoni mwa sala hii, wakati wa kukuleta mshumaha uliowashwa chini ya miguu ya Mama Yetu.
Marsiglia ni mahali pa kweli pa kukutana na watu, na ni kwenye makutano haya ya macho ambayo ningependa kutafakari nanyi, kwa sababu inaonekana kuelezea vizuri mwelekeo wa Maria wa huduma yetu. Kwa hakika, sisi makuhani na watu waliowekwa wakfu pia tumeitwa kuwasaidia watu kuhisi macho ya Yesu na, wakati huo huo, kupeleka macho ya kaka na dada zetu kwa Yesu. Hapo awali, sisi ni wenye rehema, na wa mwisho ni waombezi. Baba Mtakatifu akiendelea kwa njia hiyo amefafanua kuwa “Mtazamo wa kwanza ni ule wa Yesu anayebembeleza wanaume na wanawake wote kwa upole. Anatutazama kwa makini kuanzia kichwani hadi miguuni, si katika kuhukumu, bali kuwainua wale walio wa hali ya chini. Mtazamo wake umejaa huruma inayoangaza macho ya Maria. Na sisi, tulioitwa kutafakari mtazamo huo, tunalazimika kuwa wanyenyekevu, ili kwamba kwa huruma, tuweze kuifanya yetu wenyewe “fadhili zenye kutia moyo wa Mchungaji Mwema, ambaye hawakemei kondoo waliopotea, bali huwachukua mabegani mwake na kusherehekea kurudi kwake kundini.

Baba Mtakatifu kwa njia hiyo ameomba kuwa “tujifunze kutokana na mtazamo huu, tusiruhusu siku kupita bila kukumbuka ule wakati ambao sisi wenyewe tumehisi kwamba imetua juu yetu na tuifanye kuwa yetu ili tuwe wanaume na wanawake wa huruma. Na tufungue milango, si ya makanisa makuu na kanisa tu, bali hasa ya moyo, ili kuonesha kwa njia ya upole wetu, wema na kukubalika kwa uso wa Bwana wetu. Yeyote anayekukaribia lazima asipate upweke au hukumu, lakini apate ushuhuda wa furaha ya unyenyekevu, yenye matunda zaidi kuliko maonesho yoyote ya uwezo. Watu waliojeruhiwa na maisha wapate bandari salama machoni penu, kutiwa moyo katika kukumbatia kwenu, na kubembeleza mikononi mwenu ambayo inaweza kufuta machozi yao. Hata pamoja na mahangaiko mengi ya kila siku, Papa Francisko amewasihi, wasipunguze joto la mtazamo wa macho ya Mungu ya baba na mama. Ni ajabu kusambaza msamaha wake kwa ukarimu, yaani, daima kufungua minyororo ya dhambi kwa njia ya neema na kuwaweka huru watu kutoka katika vikwazo, majuto, kinyongo na hofu ambazo hawawezi kushinda peke yao. Inapendeza kugundua tena kwa mshangao, katika kila umri, katika nyakati za furaha na huzuni, furaha ya kuangazia maisha kupitia Sakramenti, na kuwasilisha, katika jina la Mungu, matumaini yasiyotazamiwa ya uwepo wake wa kufariji, huruma ya uponyaji, na huruma inayosonga mbele.
Papa amekazia kushauri wawe karibu na wote, hasa walio dhaifu na wasio na bahati, na kamwe wasiruhusu wale wanaoteseka wakose ukaribu wao wa uangalifu na wa busara. “Kwa njia hii, itakua ndani yao na pia ndani yenu imani inayohuisha sasa, tumaini linalofungua kwa siku zijazo na upendo unaodumu milele. Hii ndiyo hatua ya kwanza yaani ya kuwa na macho ya Yesu kwa ajili ya kaka na dada zao. Kisha, kuna mtazamo wa pili ambao Papa amefafanua kuwa ni “ ule wa wanaume na wanawake wanaomgeukia Yesu. Kama vile Maria, ambaye kule Kana alichukua na kisha akaleta mbele za Bwana mahangaiko ya vijana wawili walikokuwa katika harusi yao (taz. Yn 2:3), ninyi pia mmeitwa kuwa sauti ya kuwaombea wengine (Rm 8:34). Kwa njia hiyo, sala katika kitabu cha sala, tafakari ya kila siku ya Neno, Rozari na kila sala nyingine ambapo ninapendekeza hasa ile ya kuabudu iyokutana na nyuso za wale ambao Mtoaji atawaweka katika njia zenu. Mtapeleka macho yao pamoja, sauti na maombi yao kwenye Meza ya Ekaristi, mbele ya hema au kwenye ukimya wa chumba chenu, ambapo Baba anawaona (Mt 6:6). Mtakuwa mwangwi wao mwaminifu kama waombezi, malaika duniani, yaani, wajumbe, wanaoleka kila kitu mbele ya utukufu wa Bwana (Tob. 12:12). Papa Francisko amekazia kusema “Ningependa kufanya muhtasari wa tafakari hii fupi kwa kuvuta usikivu wenu kwenye picha tatu za Maria ambazo zinatolewa ibada katika kanisa hili. Ya kwanza ni sanamu kubwa inayosimama juu ya kilele chake; inamwonesha akiwa amemshika Mtoto Yesu katika tendo la baraka. Kama Maria, na tulete baraka na amani ya Yesu kila mahali, katika kila familia na moyo. Ni mtazamo wa huruma.
Picha ya pili iko chini yetu ya Kanisa: ni Bikira wa Bouquet", zawadi kutoka kwa mtu mkarimu. Yeye pia amembeba Mtoto Yesu kwa mkono mmoja na kutuonesha sisi, lakini kwa upande mwingine, badala ya fimbo, anashikilia shada la maua. Inatufanya tufikirie jinsi ambavyo Maria, kielelezo cha Kanisa, anapomkabidhi Mwanawe kwetu, pia anatuwasilisha kwake, kama shada la maua ambamo kila mtu ni wa kipekee, mzuri na wa thamani machoni pa Baba. Ni macho ya mwombezi. Hatimaye, sanamu ya tatu ni ile tunayoiona hapa katikati, kwenye madhabahu, ambayo inashangaza kwa ajili ya fahari inayoangaza. Sisi pia tunakuwa Injili iliyo hai kwa kadiri tunaotoka nje ya nafsi zetu kuishirikisha, tukiakisi nuru yake na uzuri wake kwa maisha ya unyenyekevu, ya furaha, yenye wingi wa bidii ya kitume. Wamisionari wengi waliotoka mahali hapa pa juu ili kutangaza habari njema ya Yesu Kristo ulimwenguni pote wawe chanzo cha kitiwa moyo kwetu.” Baba Mtakatifu aidha amebainisha kuwa “, tuweke mtazamo wa macho ya Mungu kwa kaka na dada zetu, tulete kiu yao kwa Mungu, tueneze furaha ya Injili. Haya ni maisha yetu, na licha ya ugumu na kushindwa, ni mazuri sana. Tumuombe pamoja na Mama Yetu, ili atusindikize na kutulinda. Ninawabariki kutoka moyoni mwangu. Na tafadhali, mniombee. Merci! Alihitimisha.