Tafuta

Maisha ya watoto lazima kulindwa.Na maisha yangekuwa mazuri duniani ikiwa wote tunaokutana nao ni uso wa Bwana. Maisha ya watoto lazima kulindwa.Na maisha yangekuwa mazuri duniani ikiwa wote tunaokutana nao ni uso wa Bwana. 

Papa kwa kituo cha ulinzi wa Watoto:dhuluma zimeathiri Kanisa na Ulimwengu

Jinsi gani ulimwengu ungebadilika ikiwa tungejisadikisha kwamba kila mmoja wa wadogo tunaokutana nao ni mwonekano wa uso wa Mungu!Ikiwa tungeona katika mateso ya kila mtoto,ya kila mtu aliye hatarini,kuna tabia iliyochapishwa katika leso ya Veronica aliyofuta uso wa Kristo.Ni katika hotuba ya Papa alipokutana na wawakilishi kutoka Amerika Kusini wa masuala ya Ulinzi wa Watoto.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 23 Septemba 2023 amekutana na wawakilishi  kutoka Amerika ya Kusini wa Kituo cha Uchunguzi wa habari za masuala ya Ulinzi wa Watoto ambao wamekutanika siku hizi jijini Roma katika mkutano wao. Papa  katika hotuba yake amesema inashangaza kwamba mkutano huu umefanyika mnamo Septemba 25, tarehe ambayo, kwa mujibu wa tamaduni ya kale, kumbukumbu ya shahidi wa mtoto huadhimishwa katika mahali padogo patakatifu nchini Hispania. Bila kujali ukweli unaozungumziwa, kinachofanya hadithi hiyo kuvutia ni kwamba mkasa wa mtoto huyo umehusishwa na ule wa Yesu mwenyewe, na katika uwakilishi wake anaonekana amevaa kama nguzo za Bwana, wakati akitembea kuelekea Kalvari na huku akiteseka Mateso yake mwenyewe.

Ulimwengu ungebadilika

Baba Mtakatifu amesema ukweli huu, ambao unaweza kuonekana kuwa wa kawaida, ulimkumbusha hsitoria ya Injili ya Hukumu ya Mwisho ambamo tunasikiliza maneno ya kufadhaisha ya Mfalme mkuu: "Amin, nawaambia, kila wakati ulipomtendea mmoja tu wa hawa ndugu aliye mdogo kuliko wote, mlinitendea mimi” (rej. Mt 25, 40). Jinsi gani ulimwengu ungebadilika ikiwa tungejisadikisha kwamba kila mmoja wa wadogo tunaokutana nao ni mwonekano wa uso wa Mungu! Ikiwa tungeona katika mateso ya kila mtoto, ya kila mtu aliye hatarini, tabia iliyochapishwa katika laso ambayo Veronica alifuta uso wa Kristo!, Papa Francisko amesema.

Dhuluma zimeharibu Kanisa na Ulimwengu

Kwa njia hiyo Papa amebainisha jinsi ambavyo wao wanajua vyema, na wanajaribu kufanya kazi na kutumia mbinu zinazozidi kufaa ili kutokomeza janga la unyanyasaji, katika Kanisa na ulimwenguni. Hatupaswi kusahau hilo kwamba dhuluma ambazo zimeathiri Kanisa ni kielelezo kidogo cha ukweli wa kusikitisha unaohusisha wanadamu wote na ambao, juu ya yote, hauzingatiwi.” Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anaamini kuweza kusema kwamba Kanisa limefanya maendeleo ya kutosha katika njia hii na kwamba halitaacha kufanya hivyo. Mengi ya sifa zinaweza kuhusishwa na juhudi kama hizo wanazofanya.  Ametoa shukrani kwa kazi hiyo yote. Lakini pia wanapaswa kuwa kazi muhimu kwa ajili ya jamii, ili hatua na mafanikio ya Kanisa katika njia hiiyo yawe kichocheo kwa taasisi nyingine kuendeleza utamaduni huu wa kujali.

Lazima kuwatambua walio dhaifu na wadogo

Papa Francisko aidha amesema zaidi ya hayo, ametaka kupendekeza kwao kuanzia kwenye muktadha wao  wa Picha unaowatambulisha  kila mmoja wa watoto wadogo na Kristo mwenyewe, kwamba jitihada yetu haikomei tu kwa matumizi ya itifaki, lakini kwamba tuwakabidhi kwa Yesu katika maombi. Kwa unyenyekevu na ukweli, lazima tuweze kuwatambua kati ya hao ‘wadogo’. Na, mbele ya Mkombozi, Papa amesema “sisi pia tunatafakari katika uso huo wenye hasira mateso ambayo tumepokea na kusababisha, ili tusijisikie mbali na watu tunaowakaribisha, lakini ndugu, hata katika maumivu.”

Tupendane na tujipende kwa kufahamu majeraha yetu na udhaifu wetu

Papa amekazia kisema kuwa “Tujadiliane na Yesu, tusikilize hilo Neno linalotusamehe, linalotuponya, linalotukomboa sote. Hakuchukua dhambi ya ulimwengu ili kuihukumu, bali kuiokoa, na alitufundisha kwamba hakuna upendo mkubwa zaidi kuliko ule unaotoa uhai kuliko ule unaouacha chapa katika Uso wake Mtakatifu.” Kwa hyo Yesu alituambia: “Tupendane,  na tujipenda wenyewe, yaani, kufahamu majeraha yetu, udhaifu wetu, hitaji letu la msamaha na faraja. Na tuombe, kwa imani ambayo Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu anatufundisha, katika siku hizi zinazotangulia sikukuu yake, kwa ajili ya wenye dhambi wasio na furaha na kukata tamaa, kwa uongofu wao, ili waweze kuona kwa macho ya wengine Yesu ambaye anawauliza: “Je kwa nini unanitesa.”

Papa na wawakilishi wa AMERIKA YA KUSINI
25 September 2023, 14:15