2023.09.06 La sfida di Gerusalemme yaani Changamoto ya Yerusalemu ni kichwa cha kitabu kilichoandikiwa na mwandishi Mfaransa Éric-Emmanuel Schmitt 2023.09.06 La sfida di Gerusalemme yaani Changamoto ya Yerusalemu ni kichwa cha kitabu kilichoandikiwa na mwandishi Mfaransa Éric-Emmanuel Schmitt  

Papa Francisko:wito wa wakristo ni udugu!

Gazeti la Avvenire limechapisha barua mapema iliyotiwa saini na Papa ambayo inafunga kitabu cha mwandishi Mfaransa Éric-Emmanuel Schmitt,kuhusu ‘Changamoto ya Yerusalemu-Safari ya kuelekea Nchi Takatifu',kilichochapishwa na Nyumba ya Vitabu ya Vatican.Yafuatayo ni maandishi kamili ya barua ya Papa.

FRANCESCO

Mpendwa Éric-Emmanuel, ndugu mpendwa, ukisoma kitabu chako Changamoto ya Yerusalemu ulinikumbusha siku za mwezi  Mei 2014, nilipopata neema ya kuhiji Nchi Takatifu katika kumbukumbu ya miaka 50 ya mkutano kati ya mtangulizi wangu mtukufu Paulo VI na mzalendo Athenagoras. Tukio, lile la 1964, ambalo liliashiria hatua mpya katika safari ya kukaribiana kati ya Wakristo, lililogawanyika na kutengana kwa karne nyingi, lakini lililopokea mwelekeo mpya kwa usahihi katika nchi ya Yesu. Bethlehemu, Kaburi Takatifu, Gethsemane... maeneo ambayo umetembelea na kuelezea kwa uzito wa kishairi katika kurasa hizi yamenirudia kwa nguvu. Kwa sababu imani yetu pia ni imani ya ‘kumbukumbu’, ambayo inathamini maneno na ishara ambazo Mungu hujidhihirisha. Na, unapoandika, kuwa watu huenda kwenye Nchi Takatifu ili ‘kutembelea mahali ambapo yote yalianzia’.

Katika Galilaya ya Nazareti na Kapernaumu, mahali ambapo Yesu alikulia na kuanza utumishi wake akiwa mtangazaji wa Ufalme wa Mungu; katika Uyahudi wa Bethlehemu na Yerusalemu, alikozaliwa na ambapo mfano wake wa kidunia ulitimia; katika maeneo haya ukawa msafiri wa kugusa fumbo lisiloeleweka la Ukristo. Unachofafanua kwa maneno ambayo yananigusa sana ni  “Kufanyika mwili. Mungu alichukua mwili, mfupa, sauti, damu ndani ya Yesu”. Ndiyo, Nchi Takatifu inatupatia zawadi hii kuu: kupata uzoefu halisi kwamba Ukristo si nadharia wala itikadi, bali ni uzoefu wa ukweli wa kihistoria. Tukio hili, la Mtu huyu, bado inawezekana kukutana leo hii  huko, kati ya vilima vya jua vya Galilaya, upana wa jangwa la Yudea, vichochoro vya Yerusalemu. Si kama tukio la kimafumbo kama mwisho lenyewe bali kama uthibitisho halisi wa kupinga kwamba Injili zimetukabidhi ufunuo halisi wa ukweli wa kihistoria, ambamo ufunuo wa hakika wa Mungu umekuwa ukifunuliwa kwa wanaume na wanawake wa nyakati zote: Mungu alifanyika mwili katika mtu, Yesu wa Nazareti, ili kututangazia kwamba Ufalme wake uko karibu nasi.

Umeangazia wazi hilo katika pendekezo la upya la Njia ya Msalaba wakati kwa wakati fulani unathibitisha: “Ubinadamu wa Mungu wangu sio sanamu. Hapana! Mungu kweli alijifanya mwili na damu ndani ya Yesu, na kama mwanadamu aliishi, alipenda, aliteseka kwa ajili ya upendo wetu, wa kila mtu, akatoa maisha yake msalabani. Kiukweli hii ndiyo habari njema ambayo sisi sote tunangojea: kwamba Mungu si kiumbe cha ajabu kilichofichwa mawinguni bali ni mtu anayekuja karibu nasi na kutujua. Vipengele vingine vya historia yake ya kusisimua vilinipatia changamoto. Kutajwa, kwa mfano, kwa Mtakatifu Charles de Foucauld ambaye, kama ulivyoweza kuniambia katika moja ya mikutano yetu, ilikuwa asili ya uangalizi ya kukutana kwake na Mungu katika usiku wa dhiki jangwani. Baada ya kuona na kugusa mahali ambapo Ndugu Charles aliishi Nazareti, akikomaza huko hali ya kiroho iliyomfanya kuwa ‘ndugu wa ulimwengu wote’, pia ilimfungulia ukaribu wa maono ya kitaalimungu ambayo anafupisha kama ifuatavyo: “Kushuhudia. Sio kugeuza.”

Nimerudia hilo mara kadhaa, nikirejea kauli ya Papa Benedikto XVI: “Kanisa halikui kwa kugeuza imani bali kwa mvuto”. Mkristo hamwongoi mtu yeyote, ikiwa kuna chochote, anashuhudia ukweli kwamba Mungu amemfikia na kumwokoa kutoka katika shimo la dhambi zake na amemwonesha huruma isiyo na kikomo. Huu ndio wito wa Mkristo wa kushuhudia wokovu uliomfikia. Na nikimkumbuka Charles de Foucauld, alivyochukua uhuru wa kufunga kwa kuazima jina ambalo umechagua kutoa kwenye kichwa cha kitabu cha safari, Changamoto za Yerusalemu ambayo kwa maoni yangu ni, kwa uhalisia, changamoto ambayo sote tunakabili, ile ya udugu wa kibinadamu. Huko Yerusalemu, umeona na kusema juu yake, umekutana na tamaduni  kuu ya kidini ambayo inarudi kwa Ibrahimu: Uyahudi, Ukristo na Uislamu.

Na sio kwa bahati mbaya kwamba wakati wa ziara yangu ya kitume mnamo mwaka 2014 nilitaka kusindikizana na watu wawili muhimu wa Kiyahudi na Kiislamu, Mkuu wa kiyahudi Abraham Skorka na mwakilishi wa Kiislamu Omar Abboud. Kwa sababu nilitaka kuonesha, hata kwa mtazamo hai, kwamba waamini wameitwa kuwa ndugu na wajenzi wa madaraja, na si maadui tena au watengeneza wa  vita. Wito wetu ni udugu, kwa sababu sisi ni watoto wa Mungu mmoja. Changamoto ambayo Yerusalemu bado ipo  na katika  ulimwengu leo ​​ni hii hasa ya kuamsha ndani ya moyo wa kila mwanadamu hamu ya kumwangalia mwenzake kama ndugu katika familia moja ya kibinadamu. Ni kwa dhamiri hiyo tu na ufahamu huo tutaweza kujenga wakati ujao unaowezekana, kunyamazisha silaha za uharibifu na chuki, na kueneza ulimwenguni pote harufu nzuri ya amani ambayo Mungu hutupa bila kuchoka.

Barua ya Kipapa katika kitabu mwandishi Schimitt
06 September 2023, 18:27