Tafuta

Papa Francisko:Msamehe ndugu daima kama anavyosemehe Mungu!

Yesu alisema si kusemehe mara saba bali saba mara sabini.Ujumbe wa Yesu huko wazi.Mungu anasemehe namna isiyohesabika,hana kipimo.Yeye ndivyo alivyo anatenda kwa ajili ya upendo na bure.Sisi hatuwezi kumlipa,lakini tunapomsamehe kaka au dada,tunamwiga.Ndivyo Papa amesema katika tafakari ya Injili ya Dominika tarehe 17 Septemba 2023.

Na Angella Rwezaula; -  Vatican.

Katika Dominika ya 24 ya Mwaka A wa Kanisa, Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 17 Septemba 2023. Baba Mtakatifu akianza tafakari yake amesema: “Leo Injili inatuzungumza juu ya msamaha (Mt 18,21-35). Petro aliuliza Yesu kuwa: “Bwana ni mara ngapi ninapaswa kumsamehe ndugu yangu ikiwa ananikosea? Hadi mara saba?  Saba katika Biblia ni namba ambayo inaelekeza utimilifu na hivyo Petro alikuwa mkarimu kwa kupendekeza swali lake. Lakini Yesu alikwenda zaidi, maana alimjibu:  “Si kwambii mara saba, bali hadi saba mara sabini” (Mt 18, 22). Yaani  alitaka kumwambia kwamba unaposamehe usihesabu na kwamba ni vyema kusamehe yote na daima! Na ndiyo anavyofanya Mungu kwetu sisi, na kama anavyoitwa kufanya, yule anayetoa huduma ya msamaha wa Mungu, yaani kusamehe daima.”  Papa ameongeza “hayo mimi huwaleza sana mapadre, waungamishi, kuwa msamehe daima kama anavyosamehe Mungu”.

Baba Mtakatifu amesema Yesu  aidha anafafanua  baadaye ukweli huu kupitia msemo ambao unahusiana na idadi. Kuhusu mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na mtumwa wake. Baada ya kumsamehe talanta elfu kumi. Ni thamani ya kutia cumvi, kubwa ambayo inatofautiana kati ya tani 200 na 500 za fedha! Ilikuwa ni deni lisilowezekana kulipa, hata kwa kufanya kazi maisha yote: lakini yule mfalme  ambaye anatwambia Baba Yetu, alimsamehe kwa sababu ya huruma yake safi (Mt 18, 27).  Huo ndiyo moyo wa Mungu. Husamehe daima kwa sababu Mungu ni mwenye huruma. Tusisahau jinsi alivyo Mungu ya kwamba ni Mungu wa karibu, wa hurruma na mpole. Ndiyo namna yake, ya kuwa Mungu,  Papa amesisitiza.

Waamini wengi katika sala ya Malaika wa Bwana
Waamini wengi katika sala ya Malaika wa Bwana

Lakini yule mtumwa aliyesamehewadeni lile, hakutumia huruma yote kwa mtazamo wa mjoli wake aliyekuwa amrudishie dinari mia. Hata hii pia kilikuwa ni kiasi kikubwa, kinachofanana karibu mshahara wa miezi mitatu, kwa kutaka kusema kwamba kusehemehana kati yetu kuna gharama, lakini kwa haikuwa na ulinganifu wa msamaha ule  ambao alikuwa amesahewa na Bwana wake. Kwa hiyo Papa  Francisko ameongeza kusema ujumbe wa Yesu huko wazi. Mungu anasemehe kwa namna isiyohesabika, kwa kuacha kila vipimo. Yeye ndivyo alivyo anatenda kwa ajili ya upendo na bure. Mungu hanunuliwi. Huwezi kumnunua Mungu. Mungu ni wa bure na kila kitu chake ni bure. Sisi hatuwezi kumlipa, lakini tunapomsamehe kaka au dada, tunamwiga. Kusamehe, siyo tendo jema  tu ambalo linawezekana kufanya au kuacha, bali kusamehe ni hali ya lazima kwa aliye mkristo. Kila mmoja wetu kiukweli amesamehewa. Tusisahau hili kuwa sisi tulisamehewa. Mungu alitoa maisha kwa ajili yetu na hakuna namna ambayo tunaweza kumrudishia huruma yake, na ambayo kamwe hairudishi rohoni mwake.

Waamini katika sala ya Malaika wa Bwana 17 Septemba
Waamini katika sala ya Malaika wa Bwana 17 Septemba

Lakini kwa kujibu utoaji wake bure, yaani kusamehana sisi kwa sisi, tunaweza kumpatia ushuhuda, kupanda maisha mapya yanayotuzunguka. Nje ya msamaha, kiukweli hakuna matumaini; nje ya msamaha hakuna amani. Msamaha ni oksjeni ambayo inasafisha hewa iliyochafuliwa na chuki; ni dawa ambayo inaponesha sumu za hasira, ni njia ya kukomesha ghadhabu na kuponesha magonjwa katika moyo ambao unachafua jamii. Papa ametoa maswali: je mimi ninaamini kuwa nimepokea kutoka kwa Mungu zawadi ya msamaha mkubwa? Yeye anasemehe: je ninaamini kwamba Yeye anasemehe?

Je ninahisi furaha ya kujua kuwa Yeye daima yuko tayari kunisamehe ninapoanguka, hata wakati wengine hawafanyi, hata wakati ninashindwa hata kujisamehe? Na kisha je ninajua kusamehe mwingine aliyenitendea vibaya? Katika mantiki hiyo Papa amependa kupendekeza zoezi moja la kufanya: ambalo ametaka lifanyike muda huo huo kuwa: kila mmoja wetu afikirie mtu ambaye alimjeruhi na kumuomba Bwana nguvu ya kumsamehe, amekazia Papa. Na kumsamehe kwa upendo wa Bwana, itakuwa vizuri kwetu sisi na kuturudishia amani katika moyo. Maria Mama wa Huruma, atusaidie kupokea neema ya Mungu na kusameheana mmoja na mwingine.

Tafakari ya Papa Angelus 17 Septemba 2023
17 September 2023, 12:21