Tafuta

2023.09.09  Papa amekutana na chama cha Mkutano wa wanandoa 2023.09.09 Papa amekutana na chama cha Mkutano wa wanandoa  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko:Ndoa ni daraja na fursa ya kukuza miito sio bwawa la ubinafsi

Papa amekutana na wajumbe wa chama cha Familia.Katika hotuba yake amewahimiza wahamasishe uhusiano kati ya miito miwili tofauti na ya kukamilishana:maisha ya Ndoa na maisha ya kichungaji.Ndoa na Daraja Takatifu,sakramenti zote zilizoanzishwa kwenye kifungo cha mke na mume ni miito ya kuishi maisha ya uinjilishaji zaidi ya njia za bwawa la ubinafsi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika hotuba ya Baba Francisko kwa wajumbe wa Chama cha Kuhamasisha Familia  kiitwacho (Mkutano wa Kindoa) aliokutana nao Jumamosi tarehe 9 Septemba 2023 katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, amehamasisha udugu na si unyanyasaji, bali kujikita katika njia ya kuzalisha ubinadamu mpya. Kwa njia hiyo akianza hotuba yake,  Baba Mtakatifu ameshukuru kwa ziara yao, ambayo imefanyika wakati wanapitia siku chache za kutafakari juu ya tukio la kumbukumbu yao ya miaka arobaini na tano tangu kuanza chama hicho na  hivyo amewatakia matashi mema. Katika miaka hii yote, wakiongozwa na amri ya upendo wa Yesu (taz. Yohana 15:12), wamejitolea kwa ugunduzi upya wa sakramenti ya Ndoa na ile ya Maagizo, wakitafuta sio tu kuimarisha utajiri wao kwa njia tofauti; lakini pia kuleta uhusiano kati ya miito hii miwili muhimu. Ndoa na Daraja Takatifu, kiukweli, ingawa kwa njia tofauti na kulingana na karama ya kila mmoja, zinaunganishwa kwa karibu kwa sababu zote mbili zinadhihirisha upendo wa Mungu, zikijenga Mwili wa fumbo la Kanisa.

Papa akutana na wanachama wajumbe wa Mkutano wa kindoa
Papa akutana na wanachama wajumbe wa Mkutano wa kindoa

Sakramenti hizi mbili, kwa kweli, kwa njia tofauti lakini zinazokamilishana, zinazungumza juu ya ndoa: kwa upande mmoja mchango kamili, wa kipekee na usioweza kufutwa wa wanandoa, kwa upande mwingine sadaka ya kuhani ya maisha kwa ajili ya Kanisa, ni ishara za upendo wa wanandoa ya Mungu kwa ajili yetu. Tukirejea mada waliyoichagua kwa ajili ya tukio hilo isemayo: “Sisi ni ndoto ya Mungu”, Papa  Francisko amependa kuwaleza kwamba “karama ya mwenzi wa ndoa ” ni unabii wa utimilifu wa ndoto ya Mungu. Na ndoto ya Mungu ni nini? Akiwaalika wanafunzi kubaki wakiwa wameshikana naye kama matawi kwenye mzabibu (rej. Yh 15:4) na kusali kwa Baba ili awaweke katika upendo, Yesu mwenyewe anatufunulia hilo, akiomba kwamba sisi sote tunaweza kuwa “kitu kimoja” (Yh 15:4). Yh 17:21).

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu alisema kuwa:“Ndoto ya Mungu kwetu ni hii: kutuunganisha katika upendo wake, katika ushirika wake, atufanye tugundue uzuri wa uwana wa kimungu na udugu kati yetu. Hii ndiyo sababu Yesu aliomba kwa bidii. Na anatutuma kwenye barabara za ulimwengu kutangaza kwamba njia ya kutokeza ubinadamu mpya inategemea udugu, matunda ya upendo, si juu ya unyanyasaji na ubinafsi. Kwa maana hiyo, huduma wanayoitoa kwa Kanisa, lakini pia kwa jamii, yaani kuambatana na wanandoa na mapadre, inawakilisha kipande cha thamani ambacho kinachangia kutimiza ndoto ya Mungu, lakini juu ya yote kwa kuingia kwa upendo katika ukweli wa maisha halisi ya watu. Kwa hivyo wao unatukumbusha kuwa imani kwanza kabisa ni uzoefu wa uhusiano na kukutana. Ni historia ya upendo na Mungu, pamoja na kaka, na dada wanaotazama kwa karibu mazungumzo ya wakati mwingine magumu kati ya wanandoa na wakati mwingine hali ngumu ambazo makuhani wanaitwa kushughulikia, kuhimiza kubadilishana matunda, kujifunza pamoja sanaa ya uhusiano, sanaa ya ushirika. Kwa hivyo wanaendeleza ndoto ya Mungu, ndoto ya ushirika wa wenzi wa ndoa, katika wakati ambao wakati mwingine wanapendelea kukanyaga njia zenye ubinafsi,  badala ya kujitosa kuelekea vilele vya kupendeza vya upendo.

Baba Mtakatifu kwa kukazia zaidi amesema wao pia ni ishara kwa maisha ya Kanisa, ambayo wanaitwa kufuata njia ya usawa zaidi kati ya karama, yaani karama na huduma. Mabadilishano kati ya wanandoa na wachungaji yanapendelea hatua ya uinjilishaji ambayo leo hii yanahitajika sana. Kwa hakika, ni kwa njia ya mahusiano, kwanza kabisa kwa kutoa ushuhuda wa uzuri wa mahusiano, ndipo wanaweza kutangaza utajiri wa Injili na kuonesha upendo ambao Mungu anao kwa kila kiumbe. Kwa hiyo Papa Francisko amewahimiza waendeleze kujitolea kwao kwa ukarimu na shauku: kusambaza uzoefu wa wanandoa, mapadre na wa kitawa; kufungua milango ya safari yao kwa vijana na watu wanaohusika; kutoogopa kufuata njia mpya zinazosaidia jumuiya za Kikristo kuzidi kufikia muunganiko kati ya wanandoa na wachungaji wao. Na zaidi ya yote, Baba Mtakatifu amewaomba kujiachia wenyewe kuongozwa na Roho Mtakatifu ambaye ni upendo wa Mungu, na bila kuwa na roho hiyo shughuli zetu ni tasa na bure. Ni Roho anayefungua mioyo na akili; - ni Roho anayefanya hivyo  na  ambaye hutufanya kuwa wahusika wakuu, sisi sote, wa ndoto ya Mungu! Papa amewashukuru kwa huduma yao muhimu. Amewatakia wandelee mbele na sio kwa huzuni, bali kwa furaha! Hatimaye amewabariki na kuwaomba wasisahau kumuombea.

09 Septemba 2023, 14:29