Papa Francisko na wanahija wa Korea:Vijana wadanganywa na ufanisi
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 16 Septemba 2023 amekutana na kukndi cha hija wa wakorea katika fursa ya maadhimisho ya kifodini cha Mtakatifu Andrea Kim Taegon. Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu amewakaribisha kwa furaha kukutana nao katika siku ya kuuawa kwa Mtakatifu Andrew Kim Taegon, ambayo ilitokea miaka 177 iliyopita, na wakati wa fursa ya kubaraki sanamu yake, iliyowekwa katika moja ya eneo la nje ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Papa amemshukuru Bwana kwa ushuhuda wa maisha na ushuhuda wa imani ya mtakatifu wao mkuu na wamekuwapo pia, kwa sababu watu wa Korea hutoa ushuhuda mzuri wanapomfuata Yesu Kristo. Na shukrani za pekee Papa amependa ziwaendee kwa wale wote waliojitolea katika utekelezaji wa mpango huo, hasa kwa Kardinali Lazzaro. Na kwamba ni mzuri kwa kwa Heung-sik, kwa Askofu Mathias Ri Iong-hoon, Rais wa Baraza la Maaskofu, Korea na kwa ndugu Maaskofu wa Korea. Pia amewasalimu kwa upole viongozi wa serikali waliokuwapo, mapadre, wanaume na wanawake waliowekwa wakfu, na waamini walei: wengi wao ambao walifika kama mahujaji kutoka Korea na sehemu nyingine za dunia! Papa Francisko alitoa shukrani za dhati kwa Bw. Joseph Han Jin-seop, mke wake na Profesa Maria Ko Jong-hee, waliochongia utengenezaji wa sanamu hiyo.
Mnamo Agosti 2014 Papa Francisko ameeleza alivyopata furaha ya kutembelea nchi yao kukutana na washiriki vijana katika Siku ya VI ya Vijana wa Bara la Asia. Katika hafla hiyo alikwenda kwenye Madhabahu ya Solmoe, karibu na nyumba ambayo Mtakatifu Andrew Kim alizaliwa na alikaa kwa utoto wake. Huko alisali kimya-kimya, hasa kwa ajili ya Korea na kwa ajili ya vijana. Papa amesema anapofikiria maisha makali ya mtakatifu huyo mkuu, msemo wa Yesu unarudi moyoni mwake kuwa: “ikiwa chembe ya ngano, ikianguka chini, haifi, hubaki peke yake; bali ikifa, hutoa matunda mengi” (Yh 12:24). Ni maneno ambayo yanatusaidia kusoma kwa akili ya kiroho historia nzuri ya imani ya watu wa Korea ambayo Mtakatifu Andrew Kim ndiye mzao wa thamani: yeye, padre wa kwanza wa Kikorea shahidi, aliuawa katika umri mdogo muda mfupi baada ya kupokea daraja la upadre. Papa amesisitiza kuwa kielelezo chake kinatualika kugundua wito uliokabidhiwa kwa Kanisa la Korea, kwao wote wameitwa kwa imani changa na imani harakati ambayo, inayohuishwa na upendo wa Mungu na jirani, inakuwa zawadi. Kwa maana hiyo, pamoja na unabii wa kifo cha kishahidi, Kanisa la Korea linatukumbusha kwamba mtu hawezi kumfuata Yesu bila kukumbatia msalaba wake na kwamba hawezi kujitangaza kuwa Mkristo bila kuwa tayari kufuata njia ya maisha ya Upendo.
Kanisa lao kwa hiyo, linalotokana na walei na kurutubishwa kwa damu ya mashahidi, linafanywa upya kwa kuchota kutoka katika mizizi yake msukumo wa ukarimu wa kiinjili wa mashahidi na kuthaminiwa kwa nafasi na karama za walei. Kwa mtazamo huo Papa amebainisha kuwa, ni muhimu kupanua nafasi ya ushirikiano wa kichungaji, ili kuendeleza utangazaji wa Injili kwa pamoja; makuhani, wanaume na wanawake watawa na walei wote: wote kwa pamoja, bila kufungwa. Shauku ya kuupatia ulimwengu tumaini la Injili inafungua moyo wa shauku na kusaidia kushinda vikwazo vingi. Injili haigawanyi, hapana, bali inaunganisha; inatusukuma kupata mwili na kuwa karibu ndani ya tamaduni zetu wenyewe, ndani ya historia yetu wenyewe, kwa upole na kwa roho ya huduma, bila kuunda migogoro, lakini daima kujenga ushirika. Kujenga ushirika. Fikiria kwa makini kuhusu hili. Kwa hiyo Papa Francisko amependa kuwaalika wagundue tena wito wao kama “mitume wa amani” katika kila eneo la maisha. Andrea Kim alipokuwa akisoma taalimungu huko Macau, ilimbidi ashuhudie maovu ya Vita vya Afyuni; hata hivyo, katika mazingira hayo ya kinzani, aliweza kuwa mbegu ya amani kwa wengi, akionesha nia yake ya kukutana na kila mtu na mazungumzo na kila mtu.
Kwa hiyo ni lazima wao kuwa kichocheo cha chachu ya wasafiri na mashahidi wa upatanisho; ni ushuhuda wa kuaminika kwamba siku zijazo hazijengwi kwa nguvu kali za silaha, bali kwa nguvu ya upole ya ukaribu. Papa amesema tumkabidhi Mtakatifu Andrew Kim ndoto ya amani kwenye Peninsula ya Korea, ambayo huwa katika mawazo na maombi yake kila wakati. Na kama wajuavyo, Papa Francisko amesema jinisi ambavyo alitangaza kwamba mji wa Seoul utakuwa mahali pa Siku ya Vijana Duniani ijayo mwaka wa 2027, katika maandalizi ambayo natumaini kwamba watajitolea kwa bidii kwa ajili ya kueneza Neno la Mungu kwa vijana wa Kanisa la Korea. Licha ya historia yao ya ajabu ya imani na kazi kubwa ya uchungaji ambayo wanaifanya kwa shauku, vijana wengi, ikiwa ni pamoja na kati yao, wanajiruhusu kushawishiwa na historia za uongo za ufanisi na utumiaji hovyo, na kuvutiwa na udanganyifu. Lakini mioyo ya vijana inatafuta kitu kingine, imeundwa kwa upeo mpana zaidi: watunze, watafute, waendee, wasikilize, watangaze uzuri wa Injili ili, wawe huru ndani. mashahidi wenye furaha wa ukweli na udugu.Kwa kuhitimisha Papa amewashukuru tena kwa mkutano huo. Anawaombea na wao pia anawaomba kwa maombezi ya Mtakatifu Andrew Kim na Mashuhuda Watakatifu wa Korea, kuwalinda na kuwaonesha njia. Amewabariki kutoka ndani ya moyo wake na wasisahahu kumuombea.